BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAMAMBE YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI MASHINDANO YA LIGI YA DARAJA LA PILI NETIBOLO NGAZI TAIFA MORO.

TIMU ya netiboli ya Hamambe kutoka jiji la Mbeya imezidi kuendeleza wimbi la ushindi katika mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa ya netiboli dhidi ya timu ya mwenyeji ya Mzinga katika michuano inayofanyika kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri kwa kuwatandika mabao 36 kwa 15 yanayoendeelea mkoani Morogoro.


Katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo timu hiyo ya Haamambe iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 31 dhidi ya Alliance One iliyoambulia mabaio 17 huku Hamambe ambayo ilianza mchezo huo kwa kasi iliweza kwenda mapumziko ya kipindi cha kwanza ikiongoza kwa idadi kubwa ya mabao dhidi ya Mziga ikiwa na bao 21 kwa bao 7.


Ilikuwa safu kali ya ufungaji iliyokuwa ikiongozwa na Subira Ally aliweza kutumbukiza jumla ya mabao 35 huku Martha William akichangia bao moja katika ushindi huo huku timu ya Mzinga ikiwa na wafungaji Rehema Kassam aliweza kufunga jumla ya mabao 11 naye Jamilla Sabu akifunga mabao nne kwa upande wa timu yao ya Mzingaa katika mchezo huo.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Mwenyekiti wa timu ya Hamambe Vicent Msolla aliwasifu wachezaji wake kwa ushindi huo na kuwataka kuendeleza ushindi kwa kila mchezo kwani kufanya hiyo watakuwa wamejiwekea nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa na kuipandisha daraja timu yao ili waweze kutimiza ndoto yao ya kutwaa ubingwa wa michuano hayo na kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao na ikiwemo kuiletea sifa mzuri mkoa wa Mbeya.


Baada ya mchezo huo jumla ya timu nane zilitelemka dimbani kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri ili kusaka ushindi na kusonga mbele katika mashindano hayo ambapo timu ya Tigo kutoka Jijini Dar es Salaam iliweza kusawazisha makosa katika mchezo wa pili baada ya kuwaadhibu timu ya akinadada wa Black Sisters ya mkoani Pwani kwa bao 28 kwa 13 ikiwa baada ya mchezo wao wa kwanza kufungwa na timu ya Polisi Arusha kwa bao 25 dhidi ya mabao 15.


Matokeo mengine kwa michezo iliyochezwa na matokeo yake katika mabano ni timu ya Polisi Pwani iliweza kushinda kwa kuifunga timu ya Tupendane ya mkoa wa Lindi kwa bao 32 kwa bao 15, timua ya Alliance One nayo iliweza kurekebisha makosa ya mchezo wa pili kwa kuishinda timu ya Ruangwa ya mkoani Lindi kwa bao 22 kwa 21 baada ya mchezo wao wa awali kupoteza kwa timu ya Hamambe ya Mbeya kwa kufungwa bao 31 kwa 17 na Kurugenzi Tandahimba ya Mtwara ililala kwa maafande wa Polisi Arusha kwa 26 kwa bao 6 na Mzinga iliishinda Ruangwa kwa bao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: