BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAMAMBE YAFANYA KWELI HATUA YA ROBO FAINALI NETIBOLI.

TIMU ya netiboli ya Hamambe kutoka wa mkoa wa Mbeya imeendeleza ubabe kwa timu zinazoshiriki kwenye mashindano ya ligi daraja la pili baada ya kupata vikapu 120 katika michezo mitatu kwenye mashindano ya robo fainali inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Hamambe ambayo haijawahi kupoteza michezo yake tangu kuanza kwa mashindano hayo yaliyoanza februari 15 mwaka huu iliendeleza ubabe huo hadi katika hatua ya robo fainali kwa kuzitandika timu za Tigo ya Dar es Salaam kwa bao 47-19 huku ikiendeleza vimbi la ushindi kwa timu za Polisi Pwani kwa bao 36-16 kabla ya timu ya kuwaendesha Polisi Arusha kwa bao 34-13.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Polisi Arusha Mwenyekiti wa bodi ya michezo ya netiboli Emanuel Kimbe alisema kuwa lengo lao la kuwania ubingwa wa michuaano hiyo bado inaendelea vizuri kutokana na wachezaji wake kutekeleza majukumu yao hasa katika hatua hiyo ya robo fainali katika ligi hiyo.

“kwa kweli timu inaendelea vizuri katika mashindano haya na wachezaji wanatekeleza wajibu wao kwani mpaka sasa tunashukuru mungu hatujaweza kupoteza mchezo hata mmoja na nimeongea na wachezaji waendeeleze vimbi la ushindi ili tuweze kutimiza lengo ambalo tujmejiwekea ya kutwaa ubingwa bila ya kupoteza na kuiwezesha kuipandisha hadi ligi daraja la kwanza msimu ujao” alisema Kimbe.

Wakati timu ya Hamambe ikijivunia kwa kutopoteza mchezo kutoka hatua ya makundi hadi hatua ya robo fainali nayo timu ya Polisi Arusha inashikilia nafasi ya pili katika mafanikio hayo kwa kujikusanyia vikapu 71 huku ikipoteza mchezo wake dhidi ya Hamambe ya Mbeya katika hatua ya robo fainali katika mashindano hayo.

Timu ya Polisi Arusha iliweza kujikusanyia vikapu hivyo baada ya kucheza michezo mitatu kwa kuzitandika Tigo Dar es Salaam 27-16 kabla ya kuifunga timu ya Ruangwa ya mkoani Lindi bao 27-24 huku ikipoteza mchezo wa tatu dhidi ya Hamambe.

Katika mashindano hayo timu ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani iliweza kutoa kipigo kwa timu ya Ruangwa ya mkoa wa Lindi baada ya kuwaendesha mchamcha kwa kuifunga kwa bao 34-21 huku wenyeji timu ya Alliance One iliweza kuifunga timu ya Tigo ya Dar es Salaam kwa bao 26-16 na Kurugenzi Tandahimba ya mkoa wa Mtwara iliweza kuchapwa na Polisi Pwani bao 25-13.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: