BannerFans.com BannerFans.com
KAMANDA wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro (SACP) Adolfina Chialo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa netiboli wakati wa ufungaji michuano hiyo februari 24 katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Mjumbe wa Kamati ya Utendaji katika chama cha Netiboli Tanzania Chaneta, Mwajuma Kisenga alisema kuwa mgeni rasmi wa kufunga mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa netiboli anatarajiwa kuwa Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro Sacp, Adolfina Chialo katika mchezo ambao utawakutanisha timu zinazomilikiwa na jeshi la polisi hapa nchini baina ya timu ya Polisi Arusha na timu ya Polisi Pwani ambao utachezwa majira ya saa 9 alasiri katika uwanja huo wa Jamhuri mjini hapa.


Kisenga alisema Kamanda Chialo ndiye aliyepitishwa na kamati ya mashindano hayo kuwa mgeni rasmi na anatarajia kuingia mapema katika uwanja huo hivyo na kuwaomba wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake kufika katika uwanja wa Jamhuri kuangalia michezo ya ufungaji kwani kufanya hivyo itakuwa jambo la busara kwao hasa akinamama na wasichana wajitokeze kwa wingi ili kuweza kushuhudia wenzao wakicheza mchezo huo ambao utakuwa na ufundi wa hali ya juu katika kutoa pasi na kuonyesha uhodari wa kufunga mabao na hii inatokana na timu hizo kuwa na wachezaji wenye wengi wenye vipaji vya hali ya juu katika mchezo huo huo ambao utakuwa kufunga mashindano hayo.


Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Chama cha Netiboli Tanzania Chaneta Mary Protasi alisema kuwa katika michezo iliyochezwa majira ya saa 10 jioni jana katika muendelezo wa mashindano hayo katika hatua hiyo ya robo fainali ligi hiyo ilishuhudia timu kutoka mikoa ya kanda ya kusini zikionyeshana kazi kwenye uwanja wa Jamhuri baada ya Kurugenzi Tandahimba ya Mtwara kukubali kipigo kutoka kwa ndugu zao wa mkoa wa Lindi timu ya Kurugenzi Ruanga kwa kufungwa bao 45-13.


Protasi alisema timu ya Kurugenzi Ruangwa ilionyesha dalili za ushindi mapema baada ya kuwadhibiti Tandahimba kila idara na kushinda kupenyeza mipira kwa wafungaji wao katika mchezo huo hasa katika kipindi cha kwanza baada ya kwenda mapumziko Ruangwa wakiongozajumla ya bao 21-5.


Mfungaji Khadija Othuman wa timu ya Ruangwa aliweza kutumia vema nafasi alizopata wakati alipokaribia langoni mwa wapinzani wao baada ya kufanikiwa kufunga jumla ya bao 24 katika huo huku Naima Ramadhan akifunga bao 21 wakati wa wafungaji wa timu ya Tandahimba Nasra Selemani aliweza kufunga jumla ya bao 10 na wenzake Magedalena Luambano akichangia bao tatu katika timu yao na kufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 45-13. alisema Protasi.


Pia Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ufundi katika chama cha Netiboli Chaneta alitaja matokeo ya michezo mingine iliyochezwa jioni hiyo ya februari 22 kuwa Hamambe ya mkoa wa Mbeya iliweza kuibuka na ushindi mnono wa bao 32-19 dhidi ya timu mwenyeji wa mashindano hayo Allianve One ya mkoani Morogoro nayo Tigo ya Dar es Salaam iliweza kupoteza mchezo wake kwa Polisi Pwani baada ya kukubali kutandikwa bao 42-15 wakati JKT Ruvu ilipokea kichapo kutoka kwa akinadada wa jeshi la Polisi Arusha cha bao 22-13.


Protasi alisema katika michezo mingene itayochezwa katika uwanja huo wa Jamhuri februari 24 itakuwa kati ya timu za Hamambe ya Mbeya ambayo itajitupa uwanjani kucheza na Tandahimba huku Alliance One ikionyeshana kazi na JKT Ruvu wakati Tigo ya Dar es Salaam nayo itapambana na Ruangwa michezo ambayo inatarajiwa kucheza mapeama kabla ya mchezo wa kufunga dimba ya mashindano hayo mjini hapa kati ya Polisi Arusha na Polisi Pwani.

CHIALO KUFUNGA MASHINDANO YA LIGI DARAJA LA PILI NETIBOLI FEBRUARI 24.

admin
,
TIMU ya netiboli ya Hamambe kutoka wa mkoa wa Mbeya imeendeleza ubabe kwa timu zinazoshiriki kwenye mashindano ya ligi daraja la pili baada ya kupata vikapu 120 katika michezo mitatu kwenye mashindano ya robo fainali inayofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Hamambe ambayo haijawahi kupoteza michezo yake tangu kuanza kwa mashindano hayo yaliyoanza februari 15 mwaka huu iliendeleza ubabe huo hadi katika hatua ya robo fainali kwa kuzitandika timu za Tigo ya Dar es Salaam kwa bao 47-19 huku ikiendeleza vimbi la ushindi kwa timu za Polisi Pwani kwa bao 36-16 kabla ya timu ya kuwaendesha Polisi Arusha kwa bao 34-13.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Polisi Arusha Mwenyekiti wa bodi ya michezo ya netiboli Emanuel Kimbe alisema kuwa lengo lao la kuwania ubingwa wa michuaano hiyo bado inaendelea vizuri kutokana na wachezaji wake kutekeleza majukumu yao hasa katika hatua hiyo ya robo fainali katika ligi hiyo.

“kwa kweli timu inaendelea vizuri katika mashindano haya na wachezaji wanatekeleza wajibu wao kwani mpaka sasa tunashukuru mungu hatujaweza kupoteza mchezo hata mmoja na nimeongea na wachezaji waendeeleze vimbi la ushindi ili tuweze kutimiza lengo ambalo tujmejiwekea ya kutwaa ubingwa bila ya kupoteza na kuiwezesha kuipandisha hadi ligi daraja la kwanza msimu ujao” alisema Kimbe.

Wakati timu ya Hamambe ikijivunia kwa kutopoteza mchezo kutoka hatua ya makundi hadi hatua ya robo fainali nayo timu ya Polisi Arusha inashikilia nafasi ya pili katika mafanikio hayo kwa kujikusanyia vikapu 71 huku ikipoteza mchezo wake dhidi ya Hamambe ya Mbeya katika hatua ya robo fainali katika mashindano hayo.

Timu ya Polisi Arusha iliweza kujikusanyia vikapu hivyo baada ya kucheza michezo mitatu kwa kuzitandika Tigo Dar es Salaam 27-16 kabla ya kuifunga timu ya Ruangwa ya mkoani Lindi bao 27-24 huku ikipoteza mchezo wa tatu dhidi ya Hamambe.

Katika mashindano hayo timu ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani iliweza kutoa kipigo kwa timu ya Ruangwa ya mkoa wa Lindi baada ya kuwaendesha mchamcha kwa kuifunga kwa bao 34-21 huku wenyeji timu ya Alliance One iliweza kuifunga timu ya Tigo ya Dar es Salaam kwa bao 26-16 na Kurugenzi Tandahimba ya mkoa wa Mtwara iliweza kuchapwa na Polisi Pwani bao 25-13.

HAMAMBE YAFANYA KWELI HATUA YA ROBO FAINALI NETIBOLI.

admin
,

MCHEZAJI WA HAMAMBE YA MBEYA DOTTO DOTTO AKITAFUTA MBINU YA KUMTOKA MCHEZAJI WA IMMAKULATA CHARLE WA POLISI PWANI WAKATI WA LIGI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA NETIBOLI UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO NA HAMAMBE ILISHINDA KWA BA0 31-16.JUMLA ya timu nane zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali katika mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa michezo itayochezwa februari 21 katika uwanja wa ndani wa Jamhuri yanayoendeelea mkoani Morogoro.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika uwanja wa Jamhuri mara baada ya kumalizika kwa michezo ya makundi Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi kutoka chama cha mchezo huo taifa Mary Protasi alisema kuwa baada ya kumalizika kwa michezo ya makundi jumla ya timu nane zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali michezo itayochezwa februari 21 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.


Protasi alitaja timu ambazo zimefuzu katika hatua hiyo kuwa ni Hamambe ya mkoani Mbeya ambayo imeongoza katika kundi A huku timu ya Polisi Pwani kishika nafasi ya pili wakati Ruangwa ikishika nafasi ya tatu na mwenye wa michuano hiyo Alliance One ikishika nafasi ya nne.


Katika kundi B Mwenyekiti huyo alizitaja timu ya Polisi Arusha kuwa ndiyo iliyongoza ikifuatiwa na JKT Ruvu ya mkoani Pwani huku timu ya Tigo ya Dar es Salaam ikiwa na nafasi ya tatu huku timu ya Kurugenzi Tandahimba ya mkoanbi Mtwara ikishika nafasi ya nne katika kundi hilo.


“timu nane zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali na tutatumia mfumo wa ligi na baada ya kumalizika kwa michezo yote tutampata mshindi wa kwanza na wane ambao watapanda hadi ligi daraja la kwanza lakini wakati huo huo itategemea na timu ambazo hazikushiriki ligi daraja la kwanza mwaka jana na kati ya timu hizo kama hatadhibitisha tutakuwa na uwezo wa kuzipatisha timu nyingine kucheza ligi daraja hilo, alisema Protasi.


Aidha Mwenyekiti huyo wa kamati ya Ufundi kutoka chama cha netiboli taifa alisema kuwa katika msimu wa mashindano ya ligi daraja la kwanza mwaka 2010/2011 zaidi ya timu nne hazikuweza kucheza ligi hiyo kutokana na matatizo mbalimbali ambapo mwaka huu itawalazimu chama chicho kuandikia barua ya kuthibitisha ushiriki wao mapema ili wasifuruge utaratibu wa kuwa na timu 18 katika ligi daraja la kwanza mara baada ya ligi daraja la pili kuisha.


“tayari tumewandikia barua timu zote ambazo hazikuweza kushiriki mashindano ya ligi daraja la kwanza kwa msimu wa 2010/2011 na sababu kubwa ya kufanya hivi ni kutaka tuzifuruge utaratibu uliopo kwa kuwa na timu 18 na timu ambayo itashindwa kuthibitisha kushiriki ligi daraja la kwanza msimu huu tutaangalia kati ya timu zilizofanya vizuri kuzipandisha hadi ligi daraja la kwanza”.alisema Protasi.


Pia alizitajata timu ambazo hazikushiriki katika ligi daraja la kwanza kwa mssimu wa 2010/2011 kuwa ni Polisi Mara, Polisi Kigoma, Magereza Tabora Maganga ya jiji la Dar es Salaam pamoja na F11 Quens ya Gongo la Mboto katika jiji la Dar es Salaam.


Pia alitaja timu ambazo hazikuweza kucheza hatua ya robo fainali kuwa ni timu mwenyeji ya Mzinga Morogoro, Black Sisters kutoka mkoani Pwani na Tupendane ya mkoa wa Lindi.

NANE ZAFUZU ROBO FAINALI LGI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA NETIBOLI

admin
,

KOCHA WA TIMU YA NETIBOLI YA MKOA WA PWANI YA JKT RUVU ARGENTIBA DAUDI AKIELEKEZA JAMBO KWA WACHEZAJI WAKE KATIKA MASHINDAO YA LIGI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA YANAYOFANYIKA KWENYE UWANJA WA JAMHURI KUTAFUTA TIMU NNE ZITAKAZOPANDA DARAJA LA KWANZA MSIMU UJAO KWA KUSHIRIKISHA TIMU 11 MKOANI MOROGORO.

MKIINGIA FUNGENI MABAO MENGI !!!!!

admin
,
TIMU ya netiboli ya Hamambe kutoka jiji la Mbeya imezidi kuendeleza wimbi la ushindi katika mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa ya netiboli dhidi ya timu ya mwenyeji ya Mzinga katika michuano inayofanyika kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri kwa kuwatandika mabao 36 kwa 15 yanayoendeelea mkoani Morogoro.


Katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo timu hiyo ya Haamambe iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 31 dhidi ya Alliance One iliyoambulia mabaio 17 huku Hamambe ambayo ilianza mchezo huo kwa kasi iliweza kwenda mapumziko ya kipindi cha kwanza ikiongoza kwa idadi kubwa ya mabao dhidi ya Mziga ikiwa na bao 21 kwa bao 7.


Ilikuwa safu kali ya ufungaji iliyokuwa ikiongozwa na Subira Ally aliweza kutumbukiza jumla ya mabao 35 huku Martha William akichangia bao moja katika ushindi huo huku timu ya Mzinga ikiwa na wafungaji Rehema Kassam aliweza kufunga jumla ya mabao 11 naye Jamilla Sabu akifunga mabao nne kwa upande wa timu yao ya Mzingaa katika mchezo huo.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Mwenyekiti wa timu ya Hamambe Vicent Msolla aliwasifu wachezaji wake kwa ushindi huo na kuwataka kuendeleza ushindi kwa kila mchezo kwani kufanya hiyo watakuwa wamejiwekea nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa na kuipandisha daraja timu yao ili waweze kutimiza ndoto yao ya kutwaa ubingwa wa michuano hayo na kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao na ikiwemo kuiletea sifa mzuri mkoa wa Mbeya.


Baada ya mchezo huo jumla ya timu nane zilitelemka dimbani kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri ili kusaka ushindi na kusonga mbele katika mashindano hayo ambapo timu ya Tigo kutoka Jijini Dar es Salaam iliweza kusawazisha makosa katika mchezo wa pili baada ya kuwaadhibu timu ya akinadada wa Black Sisters ya mkoani Pwani kwa bao 28 kwa 13 ikiwa baada ya mchezo wao wa kwanza kufungwa na timu ya Polisi Arusha kwa bao 25 dhidi ya mabao 15.


Matokeo mengine kwa michezo iliyochezwa na matokeo yake katika mabano ni timu ya Polisi Pwani iliweza kushinda kwa kuifunga timu ya Tupendane ya mkoa wa Lindi kwa bao 32 kwa bao 15, timua ya Alliance One nayo iliweza kurekebisha makosa ya mchezo wa pili kwa kuishinda timu ya Ruangwa ya mkoani Lindi kwa bao 22 kwa 21 baada ya mchezo wao wa awali kupoteza kwa timu ya Hamambe ya Mbeya kwa kufungwa bao 31 kwa 17 na Kurugenzi Tandahimba ya Mtwara ililala kwa maafande wa Polisi Arusha kwa 26 kwa bao 6 na Mzinga iliishinda Ruangwa kwa bao.

HAMAMBE YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI MASHINDANO YA LIGI YA DARAJA LA PILI NETIBOLO NGAZI TAIFA MORO.

admin
,
CHINI MFUNGAJI WA TIMU YA MZINGA REHEMA KASSAM AKIJIANDAA KUFUNGA GOLI HUKU AKIWA AMEZONGWA NA WACHEZAJI WA TUPENDANE YA MKOANI LINDI WAKATI WA MASHINDANO HAO YA NETIBOLI TAIFA.


MCHEZAJI WA TUPENDANE LINDI ZUHURA KASSIM KULIA AKIMILIKI MPIRA DHIDI YA LUCY THOMAS WA TIMU YA MZINGA MOROGORO WAKATI WA MASHINDANO HAYO.


MASHINDANO ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa netiboli yameanza kutimua vumbi kwa timu mwenyeji ya Alliance One kupokea kipigo katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya timu ya Hamambe kutoka jiji la Mbeya kwa kupoteza kwa kufungwa bao 31 kwa 17 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri mjini Morogoro.

Katika mchezo huo walinzi wa timu ya Hamambe waliweza kuwadhibiti washambuliaji wa Alliance One katika mchezo huo huku wageni hao wakitawala sehemu ya kiungo na kuzidisha mashambulizi dhidi ya wapinzani wao.

Hamambe ilionyesha dalili za ushindi mapema baada ya kipindi cha kwanza kuweza kutumbukiza mabao 16 dhidi ya mabao 6 ya Alliance One huku mabao ya Hamabe yakifungwa kwa ushirikiano na washambuliaji Martha William na Subira Ally wakati ya Alliance One yakitumbukizwa katika nyavu na Vida Mengo na Mariam Juma na hadi kipindi cha kwnza kinamalizika kufanya matokeo kuwa 31 kwa 17.

Katika pindi cha pili Hamambe iliweza kufunga mabao 16 huku timu ya Alliance One iliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa wapinzani wao na kufanikiwa kufunga 11.

Wakati mchezo wa kwanza wa ufunguzi ukimalizika kwa wenyeji kupoteza mchezo huo dhidi ya Hamambe kutoka jiji la Mbeya kwa bao 31 kwa 17 timu ya JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani ilicheza mchezo wa pili kwa kuonyeshana kazi na akinadada wa Kurugenzi Tandahimba na kuwashushia kichapo cha bao 40 kwa 20.

Kikosi cha kocha mkuu wa timu ya JKT Ruvu Argentina Daudi kilionyesha nia ya kutaka kutwaa ubingwa huo na panda ligi daraja la kwanza msimu ujao kwa kuwang’uta bila huruma timu ya Kurugenzi Tandahimba kutoka mkoani Mtwara baada ya wafungaji wenye uchu wa bao Jawa Iddi kufunga bao 32 huku Ashura Sadiki akifunga mabao 8.

Timu ya Kurugenzi Tandahimba iliweza kupata mabao kupitia kwa washambuliaji wake Nasra Seleman na Magreth Mrekoni kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa JKT Ruvu 40 na Kurugenzi Tandahimba kuambulia 20.

Katika mfululizo wa mashindano yao yanayaoendelea kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa ilichezwa michezo mingine kwa timu nne kushuka dimbani kutafuta pointi kwa timu ya Polisi Pwani kuonyeshana kazi na timu ya Kurugenzi Ruangwa kutoka mkoa wa Lindi kumalizika kwa Polisi Pwani kuibuka na ushindi wa bao 26 kwa 22 ya Ruangwa.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa upinzani mkali kipindi cha kwanza Polisi Pwani waliweza kuongoza kwa bao 10 dhidi ya mabao 9 ya Ruangwa ambapo timu hizo zilionyesha kiwango cha juu katika kiopindi cha kwanza hadi kinamalizika.

Kipindi cha pili kiungo wa timu ya Polisi Pwani Gaudencia Cliton alifanya kazi ya ziada ya kuhahakisha anatafuta mipira kila kona ya uwanja na kutoka pasi za mwisho kwa washambuliaji wake ili kuweza kufunga kwa urahisi.

Washambuliaji wa timu ya Polisi Pwani, Fatuma Ahmed na Pasifika Salanga walitumia udhaifu wa walinzi wa Kurugenzi Ruangwa ambao walimezidi ujanja kwa kushindwa kuwakaba ipasavyo na kutoa mwanya washambuliaji hao hasa katika kipindi cha pili kufunga mabao hao 26 huku Ruangwa wakiambulia bao 22 yaliyofungwa na Amina Mussa na Naima Ramadhani.

Timu ya Polisi Arusha iliweza kuisambaratisha timu ya akinadada wa Tigo kutoka kudni B baada ya kuwaendesha mchakachamka na kuwafungwa bao 25 kwa 15 wakati timu mwenyeji ya Mzinga nayo ilianza vema michuano hiyo baada ya kuwatandika timu ya Tupenda kutoka mkoa wa Lindi kwa bao 25 kwa 13.

Katika mchezo huo wenyeji timu ya Mzinga iliweza kupata mabao hayo kupitia kwa washambuliaji Jamilla Sabu na Rehema Kassamu katika katika mchezo mungine wa kundi B JKT Ruvu iliweza iliweza kuwapigisha kwata ndugu zao wa Black Sisters ya Kibaha zote za mkoa wa Pwani kwa kuzifunga mabao 47 dhidi ya 10.

JKT Ruvu ambayo ilitawala kila idara ya mchezo huo iliweza kuwadhibiti ndugu zao hao kwa kipindi cha kwa kuwafunga mabao 23 mabao yaliyofungwa na Jawa Iddi aliyefunga jumla ya bao 26 huku Ashura Sadiki akifunga bao 21 wakati mabao ya Black Sisters yalifungwa na Kemmy Seleman 3 na Farida Juma akifunga bao 7.

Mashindano hayo yaendelea mchana huu katika kundi A kwa kuzikutanisha timu za Kurugenzi Ruangwa na Alliance Onne huku Hamambe ikionyeshana kazi na Mzinga wakati kundi B Polisi Arusha itacheza NA Tandahimba na Black Sisters ya Kibaha kutoka mkoa wa Pwani dhidi ya Tigo katika uwanja huo huo wa Jamhuri mkoani Morogoro.

NETIBOLI TAANZA KUTIMUA VUMBI MORO.

admin
,
PICHA TOFAUTI ZA KIJANA ANAYEDAIWA KUKWAPUA SIMU NA KUKIMBIA NAYE KABLA YA KUTIWA MBARONI BAADA YA MWENDESHA PIKIPIKI KUPATA AJALI ENEO YA BARABARA YA DDC NA LUMUMBA MKOANI MOROGORO.

ADAIWA KUKWAPUA SIMU BAADA YA AJILI YA PIKIPIKI.

admin
,
KOCHA mkuu wa timu ya mpira wa netiboli ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani, Argentina Daudi ameibuka na kauli ya kufanya vizuri sambamba na kutwaa ubingwa wa mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa katika michuano iliyoanza kutimua vumvi kwenye uwanja wa ndani wa Jamhuri februari 16 mjini Morogoro.

Mashindano hayo ambayo yanatarajia kushirikisha timu kumi na nane (18) na kupandisha timu nne ambazo zitaingia kucheza ligi daraja la kwanza msimu huu Kocha Mkuu huyo alisema anajivunia kuwa na timu yenye wachezaji vijana na wenye nguvu wanaoweza kukabiliana na mikiki mikiki ya mashindano hayo kutokana na kuwapa mazoezi ya kutosha na lengo la kuandaa vijana hao ni kutwaa ubingwa na kuipandisha timu yeake ili kucheza ligi daraja la kwanza.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yake katika uwanja wa ndani wa Jamhuri hapa na mwandihsi wa habari hizi Kocha mkuu huyo Argentina Daudi alisema lengo kuu walilojiwekea pamoja na uongozi mzima wa timu hiyo ni kuhahakisha inapanda daraja na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo kwani uwezo wa kufanya mambo hayo mawili wanayo huku akijivunia kuwa na wachezaji wenye vipaji vya mchezo huo ambao unashika kasi kwa kujizolea mashabiki.

“kwanza JKT Ruvu ina wachezaji ambao wapo tayari kwa ajili ya mashindano haya na tumefanya mazoezi ya nguvu kambini na tumeweza kucheza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvuy na timu bora kabisa iliyopo katika ligi daraja la kwanza ya Filbert Bayi lakini katika mchezo huo tulipoteza nasi tumepata faida kwa kusawazisha makosa ambayo yalikuwepo kipindi cha nyuma na sasa tupo tayari kwa mashindano haya”. Alisema Daudi.

Kocha huyo alisema kuwa kikosi chake kiko imara na kitu ambacho anajivunia ni kuwa na wachezaji wazuri walio katika kiwango cha juu cha mchezo huo hasa kwa kutegemea safu yake ya ulinzi ambayo ina uwezo na kuzuia washambuliaji kutoka timu pinzani kutoleta madhala kwenye lango lao ambapo aliwataja kuwa ni Zainabu Rukindo na Anna Masaga huku safu ya washambuliaji ikiongozwa na Mary Bayo na Jawa Iddy ambao washambuliaji hao wakipokea mipira kutoka kwa kiungo tegemeo wa timu hiyo Angela Anold kuwalisha mipira ili kuweza kutumbukiza mpira kwenye nyavu.

Katika mashindano hayo timu ya JKT Ruvu itafungua panzia ya michuano hiyo katika mchezo wa pili dhidi ya timu ya akinadada wa Halmashauri ya Tandahimba kutoka mkoani Mtwara huku timu ya Hamambe inayomilikiwa na Halmashauri ya jiji la Mbeya yenyewe ndiyo itakata utepe kwa mchezo wa kwanza kwa kuvaana na wenyeji timu ya Alance One ambayo yenyewe ikiwa na maskani yake katika kijiji ch Kinglwira ambayo yanaendelea kwenye uwanja wa ndani wa Jamhunri mjini hapa.

KOCHA WA JTK RUVU AIBUKA NA MAJIGAMBO LIGI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA NETIBOLI .

admin
,


Askari wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro wakichukua maelezo eneo la Msamvu Maproco baada ya kutokea ajli ya iliyohusisha gari lenye namba ya usajili T 823 BAJ na pikipiki ambapo mwendesha pikipiki alidaiwa kuvunjika mguu katika ajali hiyo na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa huo.

AJALI YA PIKIPIKI MSAMVU MAPROCO.

admin
,
MKUU wa wilaya ya Morogoro, Saidi Thabiti Mwambungu anatarajia kufungua mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa kwa ajili kutafuta timu nne zitakazopanda na kucheza ligi daraja la kwanza kwa mchezo wa mpira wa pete (Netball) yatayofanyika kufanyika februari 16 katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Akizungumza mjini hapa na mwandishi wa habari hizi Kaimu Katibu Mkuu wa chama cha mpira wa pete (Chanemo) Morogoro Rose Joseph alisema kuwa mkuu huyu anatarajia kufungua mashindano ya ligi hiyo ambayo timu 18 zinatarajia kushiriki katika michuano hiyo kwwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Kaimu huyo Rose Joseph alisema maandalizi kwa ajili ufunguzi ya ligi hiyo yamekamilika kwa asilimia 90 na kwamba baadhi ya timu kutoka mikoani zimewasili mkoani hapa ili kuanza kwa kindumbwendumbe kwa kuchuana akinadada hao.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi kutoka chama cha mchezo huo taifa Mary Protasi alithibitisha kwa kuwasili kwa baadhi ya timu saba katika mikoani kuwasili mkoani hapa kwa ajili ya mashindano hayo.

Mwenyekiti huyo alitaja timu zilizowasili kuwa ni JKT Ruvu, Black Sisters kutoka mkoani Pwani, timu ya Hamambe ambayo inamilikiwa na Halmashauri ya jiji la Mbeya, timu ya Rwangwa na Lindi Vijijini kutoka mkoa wa Lindi na timu mwenyeji katika mashindano hayo ambao ni Alance One na Mzinga.

Protasi alitaja baadhi ya timu ambazo zipo njia kuelekea mkoani Morogoro kuwa ni timu ya Tigo Scout za jiji la Dar es Salaam, timu ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba na Polisi Pwani.

Timu ya akidada wa jeshi la Polisi Arusha ipo katika hatihati ya kushiriki mashindano hayo kutokana na uongozi kushindwa kutoa uthibisho wa mashindano hayo na kuongeza kuwa mashindano hayo ya mwaka huu yatatarajia kuwa mazuri kutokana na kila timu kupania kuibuka kuwa mabingwa na kuwaomba wakazi wa Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri kushuhudia mashindano hayo ya pili kwa ukubwa kwa mchezo wa pete hapa nchini.

MWAMBUNGU MGENI RASMI MASHINDANO YA LIGI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA NETBALL.

admin
,


Mshindi wa kwanza katika mashindano ya Morogoro Open Champion Ship 2011 Godfray Leverian akiwa na vikombe mara baada ya kuibuka mshindi katika mashindano hayo mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Cargo Sters Ltd Dioniz Malinzi katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Morogoro Gymkhana mjini hapa.

MSHINDI WA MASHINDANO YA MOROGORO OPEN CHAMPION SHIP 2011

admin
,

MFANYABIASHARA WA MATUNDA AKIPANGA ZAMBARAU KWENYE KIKOMBE ENEO LA BARABARA YA WATEMBEA KWA MIGUU YA ZITUO CHA ZIMAMOTO MANISPAA YA MOROGORO HUKU AKISUBIRI WATEJA WAKE WANAOTUMIA BARABARA HIYO ILI WANUNUE KAMA ANAVYOONEKANA PICHANI.

MSIMU WA MATUNDA YA ZAMBARAU

admin
,

MKUU WA KITENGO CHA POLISI JAMII KATIKA MKOA WA MOROGORO ISACK MUSHI AKIFAFANUA JAMBO KWA WANAFUNZIA WA SEKONDARI YA MWEMBESONGO KIDATO VHA NNE WAKATI WALIPOFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO KIKUU CHA JESHI LA POLISI MKOANI KWA LANGO LA KUJIFUNZA SHUGHULI ZA JESHI HILO.

KITENGO CHA POLISI JAMII.

admin
,


VITUKO VYA SOKA DUNIANI.

admin
,

HII NAYO IPO.

admin
,PICHA NAMBA 1.
Mchezaji wa Golf kutoka Jijini Dar es Salaam Gymkhana Club, Mwanaidi Ibrahimu akiingiza mpira katika shimo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mchezo wa Golf Morogoro Open Championship ambayo yanayofanyika katika uwanja wa golf gymkhana ambapo zaidi ya washiriki 70 wanashirki katika mchezo huo mjini hapa.

PICHA NAMBA 2.
Mchezaji wa Golf wa Mufindi Gymkhana Club, Mike Gratwicke, kutoka mkoani Iringa akiingiza mpira katika shimo.

PICHA NAMBA 3.
Mchezaji wa Golf ya Lugala Gymkhana Club, Abdalla Ally, jijini Dar es Salaam akijindaa kupiga mpira wakati wa ufunguzi wa mashindano katika ufunguzi huo.

MOROGORO OPEN CHAMPIONSHIP

admin
,

MKUU WA WILAYA MOROGORO SAIDI MWAMBUNGU KULIA AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO YA ASKARI WA ULINZI SHIRIKISHI (POLISI JAMII)WA KATA YA TUNGI KATIKA MANISPAA YA MOROGORO ILIYOFANYIKA KWENYE UWANJA WA MWALIMU JULIUS NYERERE NANENANE KUSHOTO NI MKUU WA KITENGO CHA POLISI JAMII MKOA WA MOROGORO ASP ISACK MUSHI.

PICHA NAMBA MBILI.
MKUU WA MKOA WA MOROGORO SAIDI MWAMBUNGU AKIMKABIDHI CHETI REHEMA ALLY MARA BAADA YA KUFUNZO MAFUNZO YA ASKARI WA ULINZI SHIRIKISHI AMBAPO JUMLA WA WAHITIMU 80 WALIFAKIWA KUNUNUKIWA VYETI NA MKUU HUYO WA KWANZA KUSHOTO NI MKUU WA KITENGO CHZA POLISI JAMII MKOA WA MOROGORO ASP ISACK MUSHI.

PICHA NAMBA TATU.

MMOJA WA WAHITIMU WA MAFUNZO HAYO AKIWA AMEBEBWA BAADA YA KUZIMIA WAKATI WA GWALIDE.


PICHA NAMBA NNE.

DC MWAMBUNGU NA ASP ISACK MUSHI MARA BAADA YA KUGAGUA GWALIDE.

PICHA NAMBA TANO.

ASKARI WA ULINZI SHIRIKISHI WAKIFURAHIA JAMBO WAKATI WA KUMALIZA MAFUNZO HAYO

ASKARI WA ULINZI SHIRIKISHI 80 KATA YA TUNGI WAFUZU MAFUNZO.

admin
,
MKUU wa wilaya ya Morogoro Said Mwambungu amewataka wazazi kuchukua hatua thabiti kwa watoto wao wanapoanza tabia ya udokozi wakiwa wadogo, na kwamba tabia hiyo ikiachwa ndiyo mwanzo kikuu cha kuzalisha kundi la uharifu hapa nchini.

Akizungumza katika na wahitimu wa mafunzo ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa vijana 80 wa kata ta Tungi katika Manispaa ya Morogoro walioshiriki mafunzo hayo alisema tabia hiyo ikiachwa bila ya kukemewa na wazazi au walezi ndiyo kulizalisha kundi la vijana wanajiingiza katika vitendo vya uhalifu na kuleta athali ndani ya jamii.

Mwambungu aliwataka wazazi kuchukua hatua thabiti katika hatua za mwanzo kwa mtoto ambao wanaanza tabia ya udokozi wakiwa mdogo na kwamba anapoachwa bila kuthibitiwa tabia hiyo hukomaa na kuzalisha majambazi.

“ Wazazi mnatakiwa kuwathibiti watoto katika hatua za awali hatua za udokozi ndiyo mwanzo wa kuwa na jambazi mtoto anapoanza kidogo kidogo kudokoa vitu vidogo mwisho wake ni kuwa jambazi”. Alisema Mwambungu.

Alisema kuwa uhalifu unaweza kupungua ama kuisha kabisa ikiwa utachukiwa kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, kata hadi taifa, na kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia kutokomeza kabisa tabia hii mbaya katika jamii ya watu wastarabu.

Aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuwatetea watu kwa mambo maovu na badala yake wawatetee kwa mambo mazuri, na kwamba inapotokea mtu amefanya uhalifu aachwe ili sheria ifuate mkondo wake na kusiwe na tabia ya kuwatetea wahalifu.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha polisi Jamii Mkoa wa Morogoro (ASP) Isack Mushi, alisema kuwa kitengo hicho kimekuwa kikabiliwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi wanaopatiwa mafunzo hayo.

Aliitaja mmoja ya changamoto hizo kuwa ni ufinyu wa nauli kwa wananchi wanaopenda kuhudhuria mafunzo hayo wanaoishio mbali na kituo cha mafunzo.

Aidha alitoa wito kwa wananchi wanaopenda kupewa mafunzo hayo kutoa taarifa kwenye kitengo hicho ili waweze kuendesha mafunzo hayo katika maeneo husika kwa kukusanya watu waliopo maeneo hayo ili kuimarisha ulinzi katika ngazi ya kaya.

Akisoma risala Damson Chilongola ambaye ni mhitimu wa mafunzo hayo aliliomba jeshi la polisi kuendelea kutoa mafunzo hayo sehemu nyingine ambazo mafunzio hayo hayajatolewa ili iwe rahisi kwa kila mwananchi kufahamu jukumu lake la polisi jamii na ulinzi shirikishi.

DC MWAMBUNGUA AWATAKA WAZAZI KUCHUA HATUA KWA WATOTO WADOKOZI MAPEMA

admin
,

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bungo Manispaa ya Morogoro, Roman Luwoga kushoto (mwenye shati nyekundu) akiwa na baadhi ya mwalimu na wanafunzi wa shule hiyo wakisomba madawati yaliyotokana na michango ya wazazi baada ya kutengeneza madawati 70 ikiwa na lengo la kuondokana na tatizo la madawati yakiwa na thamani ya sh 4.7Mil.

KIASI cha sh 4.7Mil kimewezesha kuondoa tatizo la madawati katika shule ya msingi Bungo iliyopo katika kata ya Boma Manispaa ya Morogoro kupitia michango ya wazazi baada ya shule hiyo kununua madawati 70 ikiwa na lengo la kuondokana na kero ya wanafunzi katika shule hiyo kurundikana katika dawati moja na kuwawezesha wanafunzi wawili kutumia dawati mmoja mjini hapa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano shuleni hapo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Msingi Bungo Manispaa ya Morogoro, Roman Luwoga alisema kupitia kamati ya shule hiyo iliadhimia kuwepo kwa mpango wa kuondoa tatizo la wanafunzi kukaa katika dawati moja wanafunzi watatu hali iliyopelekea ununuzi wa madawati hayo 70 ikiwa na lengo la kuondoa kabisa kero hiyo wakati wa masomo kwa wanafunzi hao.

Luwoga alisema kuwa kupitia kamati ya shule hiyo wazazi waliweza kuchanga kiasi cha sh 4.7Mil kwa ajili ya ununuzi wa madawati hayo pamoja na matumizi mbalimbali ya shule hiyo.

“hizi ni nguvu za wazazi walioamua kuchangia fedha ili kuondoa tatizo la hilo kupitia kamati yao ya shule na kufanya wanafunzi kwa sasaa wanatumia dawati moja wanafunzi wawili badala ya awali ambapo dawati moja lilikuwa linakaliwa na wanafunzi watatu ambapo hali hiyo ilikuwa kero kwa wanafunzi wakati wa masomo yao.” alisema Luwoga.

Aidha Luwoga alisema kuwa kabla ya ununuzi wa madawati hayo 70 hakukuwa na tatizo la wanafunzi katika shule hiyo kukaa chini wakati wa masomo isipokuwa tatizo likukuwa kwa wanafunzi wa madarasa mawili ambayo yalikumbwa na tatizo la dawati moja kukaliwa na wanafunzi watatu lakini kupitia mpango huo shule hiyo imefanikiwa kuondoa tatizo hilo na kuwa na akiba ya madawati ya ziada.

Pia mwalimu mkuu huyo alisema kuwa amekuwa akiwapa ovyo wanafunzi kwa kupita kila darasa kuanzia watoto wa chekechea, darasa la kwanza hadi darasa la saba kuacha tabia ya kucheza juu ya madawati hasa pindi mwalimu anapotoka darasani na badala yake kama watakuwa wamemaliza kazi ya kuandika wafanya kuzipitia kazi za nyuma kwa kujikumbusha kwa kusoma badala ya kufanya vurugu darasani ambapo kutokana na kutoa somo hilo kwa wanafunzi madawati hayo yatadumu kwa muda mrefu.

“unajua wanafunzi ni watundu sana hasa hawa wa shule ya awali, darasa la kwanza hadi darasa la nne yaani mwalimu anapokosekana kwa dakika tatu au tano darasa linakuwa na vurugu tupu kutokana na utoto wao lakini tunajaribu kudhibiti hali hiyo kila siku na wanapofika darasa la tano na saba tabia hiyo huiacha kwani akili yao inakuwa tayari imekomaa katika masomo.” Alisema Luwoga.

Luwoga alisema baada ya yeye kupita kila darasa kutoa somo kwa wanafunzi juu ya utunzaji wa madawati pia kazi hiyo ametoa agizo kwa kila mwalimu wa shule hiyo kuwakemea wanafunzi juu ya kucheza kwa kupanda juu ya madawati kwani kufanya hivyo madawati hayo yatasababisha kuharibika mapema.

WAZAZI WACHANGA SH 4.7MIL KUONDOA KERO YA MADAWATI MORO.

admin
,


Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Mwambungu akifafanua jambo wakati wa siku ya shertia nchini iliyoadhimshwa kwenye uwanja wa hakimu mkazi mkoa wa Morogoro mjini hapa, kushoto ni Kaimu Kamanda wa mkoa huo Shabaan Kimea na kulia kwake ni Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa huo Richard Kabate.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Mwambungu akifafanua jambo katika kilele hicho na kulia ni Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa huo Richard Kabate.

MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI.

admin
,

Mwanafunzi wa shule ya sekondari katika Manispaa ya Morogoro akiwa ananing'inia katika mlango wa daladala lenye namba ya usajili T 226 AEG wakati akisafiri kutoka kituo kikuu cha daladala yaendayo nje ya Manispaa hiyo jambo ambalo nihatari.

MWANAFUNZI HUYU HAKUWEZA KUJULIKANA MARA MOJA KAMA NI KONDA AU LAA.

admin
,

Raia wa kigeni wakitoa msaada wa pesa kwa ombaomba laiyekaa chini katika eneo la daraja la mto Morogoro ambapo baadhi ya ombaomba wamekuwa wakikaa kwenye kingo za daraja hilo kuomba msaada wa pesa kwa wasamalia wema ili kujikimu na hali ngumu ya maisha mjini hapa.

MSAADA KWA OMBAOMBA.

admin
,PICHA YA KWANZA JUU:
Askari kanzu (mwenye fulana nyeusi) akijitahidi kumnasua kijana katika
nguzo ya umeme baada ya kung'ang'ania wakati akigoma kwenda kituocha
polisi katika mkoa wa Morogoro hata hivyo haikuweza kufahamika mara
moja sababu ya kijana huyo kupelekwa kituoni eneo la tuta la stendi
kuu ya daladala mjini hapa.

PICHA YA KATIKATI.
akimpeleka kituoni.

PICHA YA CHINI:

akiwa amewashika watuhumiwa wawili wakatai akiwapeleka kituoni kabla ya mmoja kumshinda na kubakiwa na mmoja ambaye alifanikiwa kumfikisha kituoni.

MTUHUMIWA ANAPO GOMA KWENDA KITUONI.

admin
,

Askari wa usalama barabara mkoa wa Morogoro akiwa amemshika mkono kikongwe wakati akimvusha katika barabara eneo la daraja la mto Morogoro hali ambayo inatokona na ongezeka la magari na kusababisha adha kwa makundi ya wazee na wanafunzi kupata kero wakati wa kuvuka barabara kunatokana na uwingi wa magari mjini hapa.

NAKUVUSHA

admin
,

Vijana wachuuzi wa bidhaa zinazotokana na maliasili wakiwa wamebeba vinu na upinde wakati wakisaka wateja wao katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro.

BIDHAA ZA ASILI

admin
,
Next PostNewer Posts Previous PostOlder Posts Home