BannerFans.com BannerFans.com
MSHAMBULIAJI WA WILAYA KILOSA KIBWANA RAMADHANI AKIPIMANA UBAVU NA MSHAMBULIAJI WA MOROGORO VIJIJINI JOHN KASHINJE WAKATI WA MASHINDANO YA UMISSETA NGAZI YA MKOA WA MOROGORO KWENYE UWANJA WA JAMHURI MKOANI HAPA AMBAPO KATIKA MCHEZO HUO ULIMALIZIKA KWA SARE YA BAO 1-1.


MASHINDANO ya umoja wa michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) 2012 yameanza kulindima kwa michezo mbalimbali ambayo yanashirikisha wanamichezo kutoka wilaya sita zinazounda mkoa wa Morogoro Mei 29 mwaka huu katika viwanja vya ndani vya jamhuri mkoani hapa.

Katika michezo ya ufunguzi mabingwa watetezi kwa upande wa mchezo wa soka timu ya wilaya Kilombero iliweza kuanza vema mashindano hayo hasa baada ya kuitandika Manispaa bila huruma kwa bao 6-0 katika mchezo mkali ambao washindi walitawala kila idara ya mchezo huo.

Licha ya timu ya soka ya Manispaa kukubali kichapo hicho cha bao hizo 6-0 waliweza kuonyesha kandanda safi na kuvutia hasa kwa pasi zao ambazo zilikuwa zikiishia katika miguu ya walinzi wa Kilombero ama mlinda mlango kufuatia safu ya ushambuliaji yao walishindwa kutumia vizuri nafasi za wazi za kufunga mabao walizopata katika lango la wapinzani wao.

Wilaya ambazo zimeleta wanamichezo wake ni pamoja na Manispaa, Mvomero, Morogoro Vijijini, Kilombero Ulanga na Kilosa.

Katika mchezo huo mabao ya washindani yaliweza kupachikwa wavuni na washambuliaji, Abogasti Mutalemo alifunga mabao mawili huku wachezaji, Ammy Bangaseka, Iman Petrol, Thomas Hamis na Salum Ramadhani wakifunga bao moja moja na kufikisha idadi hiyo ya bao 6-0 dhidi ya Manispaa.

Timu ya wilaya ya Ulanga iliweza kuanza vibaya michezo hiyo hasa baada ya kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa vijana wa wilaya ya Kilosa wakati katika mchezo soka kwa wasichana Manispaa walifanikiwa kuilalua Kilombero kwa kuilaza bao 1-0 lililofungwa na Christina Daud akifunga baada ya kuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Kilombero Elizabert Amos.

Naye Mratibu wa mashindano hayo ngazi ya mkoa, Maxmilliam Lipingu alisema kuwa licha ya vijana kuonyesha ushindani lengo kuu ni kuchagua wachezaji kwa kila mchezo ambao wataunda vikosi imara kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kanda ya mashariki yatayoanza mara baada ya kumalizika kwa michezo ya mikoa.

Lipingu alisema kuwa katika matokeo ya michezo mingine ya ufunguzi kwa upande wa mchezo wa netiboli timu ya Manispaa waliweza kuifunga Mvomero kwa vikapu 37-3 huku wilaya ya Ulanga ikitambia Kilosa kwa kuilaza kwa idadi ya vikapu17-11.

Alitaja matokeo ya michezo mingine kuwa wilaya ya Kilombero iliibuka kidedea katika mchezo wa basketiboli kwa kuilaza Morogoro Vijijini kwa vikapu 47-45 kwa upande wa wavulana wakati mchezo wa wavu wavulana Kilombero iliitambia Manispaa kwa seti 2-0 kabla ya wasichana nao wakiwalaza Manispaa kwa seti 3-2.

Lipingu alisema kuwa katika mashindano hayo kuna jumla ya michezo saba ikiwemo soka wavulana na wasichana, netiboli kwa wasichana, riadha wavulana na wasichana kuanzia mita 100 hadi 5000, basketiboli wavulana na wasichana, wavu wavulana na wasichan na tufe ambapo michezo hiyo itakuwa kifanyika kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi 11:30 jioni kwenye viwanja hivyo vya Jamhuri mkoani hapa.

UMISSETA NGAZI YA MKOA WA MOROGORO 2012 KUTAFUTA TIMU ZA KUSHIRKI MASHINDANO HAYO NGAZI YA KANDA YA MASHARIKI MKOANI PWANI

admin
,
Mshambuliaji wa timu ya soka ya wasichna Manispaa ya Morogoro Christina Daud jezi ya blue akimtoka mlinzi wa wilaya ya Kilombero Averine Linyamala kushoto wakati wa mashindano ya ufunguzi ya umoja wa michezo shule za sekondari Tanzania ngazi ya mkoa wa Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa, katika mchezo huo Manispaa iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

                                    
Mshambuliaji wa timu ya soka wasichana ya Manispaa ya Morogoro Withness Adolf kushoto akiwania mpira na mlinzi wa wilaya ya Kilombero, Rose Wilbrod katika mchezo huo.MASHINDANO YA MICHEZO YA UMOJA WA SHULE ZA SEKONDARI TANZANIA (UMISSETA) NGAZI YA MKOA WA MOROGORO 2012.

admin
,
Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa miaka 50 jela na makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.

Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80.

Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa.

Mwandishi wa BBC aliyeko The Hague Anna Holligan anasema rufaa dhidi ya hukumu hii huenda ikachukua miezi sita.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu.

Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.

Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani.

Charles Taylor amelalamikia upande wa mashtaka kwa kuwatisha mashahidi katika kesi dhidi yake.

Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kuwapa silaha waasi na kubadilishana na almasi.

Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo.
 
Taylor anatarajiwa kuhudimia kifungo chake nchini Uingereza.

RAIS WA ZAMANI WA LIBERIA CHARLES TAYLOY AFUNGWA JELA MIAKA 50.

admin
,
Tingatinga la Manispaa ya Morogoro likibomoa kipaa cha nyumba iliyoko katika hifadhi ya barabara ya Kikundi wakati wa zoezi la kubomoa vibanda na vipaa vy nyumba zilizopo ndani ya hifadhi ya barabara hiyo kwa lengo la upanuzi wa barabara mkoani hapa. 

TINGATINGA LIKIONDOA KIPAA CHA BALAZA LA NYUMBA KUPISHA UPANUZI WA BARABARA MTAA WA KIKUNDI MOROGORO

admin
,
 Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood (mwenye sharti la maua) akiangalia maji yaliyochanganyikana na kinyesi cha mifugo katika machinjio ya Mtawala ambapo maji hayo yamekuwa yakitiririka na kuingia katika makazi ya wananchi eneo la mtaa wa Mtawala hali ambayo inatokana na miundombinu mibovu ya mfumo wa majitaka ya machinjio hayo kuharibika kwa muda mrefu bila kutengeneza wakati wa ziara ya mbunge huyo iliyohusisha viongozi wa afya wa Manispaa ya Morogoro ya kuangalia namna ya kutatua kero hiyo mkoani hapa.  
 Hapa Mhe Abood akiruka mtaro huo eneo la machinjio hayo ambao unaelekea katika makazi ya wananchi eneo la Mtawala.
Huu ndiyo mtaro ambaro una maji machafu ambayo yanatoa harufu kali unaokatiza katikati ya makazi ya watu mtaa wa Mtawala mjini hapa.

MTARO WA MAJI MACHAFU YA MACHINJIO YA MTAWALA KERO TUPU MOROGORO.

admin
,
Mfanyabiashara wa kuuza vikapu akiwa amebeba vikapu na mapambo ya ndani akisaka wateja katika mtaa wa Kitope Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kuwauzia bidhaa hizo mkoani hapa.


BIASHARA YA MAPAMBO YA NDANI NA VIKAPU.

admin
,
A BANANA VENDER SALES THE COMMODITY HER COSTUMERS AT FUNDOGOLO STREET IN MOROGORO TOWN, A SINGLE BANANA COST BETWEEN SH 100 AND SH 200 DEPENDING ITS ZISE.

BANANAS FORM A SIGNIFICANT PART OF THE DIET

admin
,
Msanii wa kucheza salakasi katika Manispaa ya Morogoro, Dymond Senyagwa akionyesha uhodari wake wa kuvikunja viungo vyake wakati wa ufunguzi wa tamasha la sanaa la watoto la paukwa 2012 linaloshirikisha wanafunzi wa shule za msingi katika Manispaa hiyo ya Morogoro kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

KIPAJI CHA SALAKASI

admin
,
MWANAMKE mmoja nchini Uchina ambaye ni mwanaharakati wa kutetea wasichana kubaki bikra hadi waolewe, ametoa tangazo kwenye mtandao akitafuta mume.

Mtandao wa rednet.cn umeripoti kuwa mwanamama huyo mwenye umri wa miaka thelathini na nane aliandika tangazo hilo kwenye wavuti uitwao Sina Weibo.

Mwanadada huyo anayejulikana kwa jina la Tu, aliandika vigezo anavyovitaka ambavyo mume huyo awe navyo.

Amesema lazima awe mwanachama wa chama kinachotawala nchini China, au awe mfanyakazi wa serikali. Aidha amesema iwapo mchumba atapatikana, hakutakuwa na tendo la ndoa kabla ya ndoa, na vile vile hakuta kuwa na tendo hilo pia hadi miaka mitatu ya baada ya harusi.

Ujumbe huo wa Dada Tu, umezua sokomoko na kusomwa na zaidi ya watu elfu kumi katika kipindi cha saa moja tu. Baadhi ya wachangiaji wa sakata hilo wamesema kwa vigezo hivyo kamwe hatopata mchumba.

Kwa mujibu wa Mwanamama Tu ambaye anatokea jimbo la Hubei, amesema hana muda tena wa kusubiri mchumba kwa njia za kawaida na ndio maana ametoa tangazo hilo kwenye mtandao.

UKITIMIZA VIGEZO HIVI UNAPATA MCHUMBA MWENYE BIKRA RAIA WA CHINA MIAKA 38.

admin
,
YAZINDUA VUGUVUGU LA MABADILIKO, WANACHAMA CCM WAJIUNGA.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kiliteka jiji la Dar es Salaam kilipofanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Jangwani kwa lengo la kuzindua mkakati wake mpya unaojulikana kama ‘Movement For Change-M4C’ (Harakati za kuleta mabadiliko) ukiwa na lengo la kukiandaa chama hicho kuongoza dola mwaka 2015.


Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwaonya watu aliowaita wasaliti ndani ya chama hicho, kwa kuwataka wajirudi mara moja, vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu.

Hivi karibuni Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda amekuwa akizozana na viongozi wa chama hicho tangu pale alipotangaza nia yake ya kuwania urais huku akimtaja Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwa atakuwa meneja wake wa kampeni.

Bila kumtaja jina, Mbowe alianza kwa kutoa kauli zilionekana moja kwa moja kumjibu Shibuda, akisema wapo watu wanaodai kuwa Chadema ni chama cha udini na ukabila na kusisitiza kuwa huo ni uzushi.

Wakati akiendelea kusema hayo, umati uliokuwepo uwanjani hapo ulipokea kauli hiyo kwa kupaza sauti kwamba “Shibuda ang’olewe …Shibuda ang’olewe… Shibuda aondoke!’ hoja iliyojibiwa na Mbowe papo kwa hapo kwamba mkutano huo haukuwa na lengo la kumng’oa mtu.

“Sikuja hapa kumng’oa mtu…Tumng’oe?” Alihoji Mbowe na kuongeza: “Ngoja nitoe kauli ya chama. Chama chetu hakitayumbishwa na mtu yeyote msaliti. Tutatumia vikao vya chama. Tuzungumze mambo yenye maslahi ya taifa, siyo mtu mmoja mwepesi. Kama mtu hajui moto auchezee.”

Alisisitiza kuwa chama hicho kimejengwa kwa zaidi ya miaka 20 na kimeweza kujenga ngome katika mikoa ya Mwanza, Lindi na Mtwara. Huku akinukuu kauli ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyoitoia miaka ya 1960.

 Mbowe alilitaka Jeshi la Polisi kutowatisha wanachama wa Chadema na kuonya kuwa wakifanya hivyo, wananchi nao watajibu mapigo.

“Chadema kitakuwa chama cha mwisho kuvuruga amani nchini. Nawaonya kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na kama Mwenyekiti wa Chadema na kama Mbunge. Nawaomba polisi, waache kuwasumbua wana Chadema,” alionya Mbowe.

Licha ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya wanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani, watu walianza kufurika katika Viwanja vya Jangwani kuanzia saa 8:00 mchana. Kampeni ya Movement for Change(M4C).

Akizungumzia mkakati huo, aliwataka wanachama wa Chadema na wananchi kwa ujumla kujitolea kukichangia fedha ili kufanikisha kampeni hiyo kwani alisema kukiondoa CCM madarakani si kazi rahisi, inahitaji gharama kubwa.

“Kila mwananchi anawajibu wa kubadilisha maisha yake. Kila mtu anapaswa kuwa wakala wa mabadiliko.

Kuiondoa CCM kuna gharama kubwa, kule Arumeru watu walichanga kile walichokuwa nacho kuanzia Sh. 50 na kuendelea na tulishinda, au siyo?.

 Tusije tukapata viongozi kwa fedha chafu,” alisema.

Mbowe pia alisisitiza kuwa watakuwa makini na wanachama wa CCM wanaohamia Chadema akisema kuwa watatakaswa kwanza kabla ya kupewa uanachama. Kama hiyo haitoshi, chama hicho ‘kilitembeza bakuli’ kwenye mkutano huo, ambapo watu walichanga fedha kwa ajili ya kukisaidia katika utekelezaji wa mkakati huo ambao utafanyika nchi nzima.

 Awali, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliwapa somo wananchi kuhusu mchakato wa kuandikwa Katiba mpya.

Alisema kuwa katiba ya sasa ni mbovu na kwamba inatakiwa ipatikane mpya ambayo haitachakachuliwa kwa ajili ya maslahi ya Watanzania huku akihoji mfumo wa utawala na suala zima la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 “Je, kuna nchi ngapi katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna Amiri Jeshi wangapi katika Jamhuri hii? Hivi hii ni nchi moja au tunataka kuwa na katiba itakayojibu haya yote?” Alihoji Lissu.

Aliwataka wananchi kuhoji Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba mpya kuhusu masuala hayo kwa kuwa Katiba mpya ya Zanzibar, inakinzana na Tanzania Bara na kwamba imefumua dhana nzima ya Muungano.

 “Watanzania wanatakiwa kupewa mamlaka ya kuamua kwa kupiga kura ya maoni ili kuona kama kuna haja ya kuwepo kwa Muungano au kuendelea na hiki kiini macho,” alisema Lissu.

Alisema kuwa hata Bunge la Katiba ambalo litaundwa kwa ajili ya kujadili rasimu ya katiba itakayoandaliwa na Tume ya Katiba, linaweza kuchakachuliwa kwa kuwa na wabunge wengi wa CCM ambao watapitisha baadhi ya vipengele kwa maslahi ya chama hicho.

“Kwa mtindo huu hatutapata Katiba mpya, yatakuwa yale yale, Sheria ya Marekebisho ya Katiba inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili wabunge wa Bunge la Katiba wachaguliwe na wananchi” alisema Lissu.

Alisema kuwa sheria hiyo inaeleza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ndio itakayosimamia kura za maoni na kwamba hali hiyo haitaleta Katiba mpya kwa kuwa Nec imegeuka kuwa Tume ya Taifa ya Uchakachuaji.

Aliwataka wananchi kuhoji mamlaka aliyonayo rais kwa kuwa katiba ya sasa inampa mamlaka makubwa kiongozi huyo mkuu wa nchi ambaye anaweza kuamua lolote analotaka. “Inatakiwa kuwe na mfumo wa utawala utakaowapa nguvu wananchi,” alisema Lissu na kufafanua,

“ Bunge limejaa zaidi ya wabunge 100 ambao hawajachaguliwa na wananchi, hivyo kazi yao ni kugonga meza tu, jengeni hoja zitakazoingizwa katika katiba mpya ikiwa ni pamoja na kulifanya Bunge kuwa na mamlaka ya kuiadabisha Serikali na ikiwezekana hata mkuu wa nchi”.

Lissu alimataka Rais Kikwete kuheshimu ahadi aliyoitoa kwa viongozi wa Chadema waliokwenda Ikulu kupeleka maoni ya chama hicho kuhusu katiba.

“Rais alitueleza wazi kuwa atafanyia marekebisho sheria ya mabadiliko ya Katiba kwa kuwa tuliilalamikia kwamba haikuwa sawa, ila naona hakuna alichokifanya, tunamuomba aheshimu ahadi yake,” alisema Lissu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa ambaye tofauti na ilivyozoeleka, hakuzungumza kwa muda mrefu. Aliwataka wabunge wa chama hicho kuzungumzia matatizo yanayowakabili wananchi watakapokuwa bungeni mwezi ujao.

“Maisha ya Watanzania si mazuri, vyakula vinauzwa kwa bei kubwa…, nitatumia nafasi hii kuwaeleza machache wabunge wangu ili wakayaseme bungeni, wabunge wetu hawana wa kuwafunga mdomo, maisha yanazidi kuwa magumu lakini yamekuwa mazuri kwa mafisadi, ”alisema Dk Slaa.

Alisema kuwa Serikali inatakiwa itumie kodi ya wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo na sio kuwalipa watumishi ambao nafasi zao hazina manufaa kwa wananchi.

“Kuongeza kodi katika mafuta ya taa ili watu wasichakachue mafuta ya dizeli ni mwiba kwa Watanzania…, hii ni sawa na hoja ya mwendawazimu, wanatakiwa kudhibiti uchakachuaji sio kupandisha bei,” alisema. Dk Slaa.

Pia aligusia mchakato wa Katiba mpya akiwataka wananchi kutoa maoni yao kuhusu mamlaka makubwa ya rais kwa kuwa ndio yanayochangia ugumu wa maisha kwa Watanzania.

“Inakuwaje rais anateua mawaziri 55 halafu wananchi wanashindwa kuhoji, Uingereza mawaziri wapo 20 tu,” alisema Dk Slaa. Shamra shamra mkutanoni.

Mbowe, Katibu wake Dk Slaa, wabunge na viongozi wengine walifika katika viwanja hivyo saa 9:30 na kufanya umati mkubwa uliokuwepo eneo hilo kulipuka kwa shangwe.
 
Wabunge waliotia fora katika mkutano huo ni pamoja na Mbunge wa Ubungo John Mnyika tangu alipoingia uwanjani hapo na hata alipopewa nafasi ya kusalimia alishangiliwa kwa nguvu.
 
Mnyika ambaye hivi karibuni alishinda kesi yake ya ubunge iliyofunguliwa na mpinzani wake kutoka CCM Hawa Ngh’umbi, alisema kesi hiyo imedhihirisha kuwepo kwa mfumo mbovu wa uchaguzi na kwamba madai yake kwamba CCM kimekumbatia mafisadi ni ya kweli.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema naye alishangiliwa kwa nguvu hasa pale aliposema ni heri kuwa na vita vya kudai haki kuliko kuwa na amani inayopumbaza. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na vyama marafiki kutoka nchi 16 za Afrika na baadhi ya viongozi kutoka chama tawala cha Ujerumani cha CDU.
 
Chadema pia kiliendesha kampeni za ‘Vua gamba vaa gwanda’ ambapo kilivuna wanachama wapya 3,120 waliorudisha kadi zao wengi wakitoka CCM. Awali Chama cha CDU kiliendesha semina kwa viongozi wa Chadema kuhusu matumizi ya vifaa vya elektroniki katika masuala ya uchaguzi.

CHADEMA KASI KUBWA.

admin
,
Kiongozi wa bendi ya Ngoma Afrika Morogoro, David Kitururu kushoto akisakata dansi na mwanafunzi wa shule ya msingi Bungo, Jonas Koba (15) wakati wa ufunguzi wa tamasha la sanaa la watoto la paukwa 2012 linaloshirikisha wanafunzi wa shule za msingi katika Manispaa ya Morogoro kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
                                 
Msaani maarufu wa kughani tenzi na mashairi nchini, Mrisho Mpoto akitumbuiza kwa kughani mashairi wakati wa ufunguzi wa tamasha la sanaa la watoto la Paukwa 2012 linaloshirikisha wanafunzi wa shule za msingi katika Manispaa ya Morogoro kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

TAMASHA LA SANAA LA WATOTO LA PAUKWA 2012

admin
,
ASKARI KANZU AMBAYE NI ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOA WA MOROGORO AKIWA AMEMSHIKA MWENDESHA PIKIPIKI MARA BAADA YA KUBAINIKA KUWA NA MAKOSA YA KUENDESHA PIKIPIKI BILA YA KUWA NA LESENI NA UVAAJI WA KOFIA NGUMU (ELMENT) KATIKA NMAKUTANO YA BARABARA YA OLD DAR ES SALAAM NA NKOMO MANISPAA YA MOROGORO WAKATI WA ZOEZI ENDELEVU YA UKAMATAJI WA MAKOSA HAYO MKOANI HAPA.

MFUMU WA UKAMATAJI WA WAENDESHA PIKIPIKI WALIOZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI MKOA WA MOROGORO NI HUU.

admin
,
Mkazi wa Manispaa ya Morogoro akikokta baiskeli iliyosheheni maboksi tupu mara baada ya kuyakusanya kutoka kwenye maduka kisha kwenda kuyauza katika soko kuu la mkoa huo kwa ajili ya kuwauzia wateja mbalimbali wanaotembelea soko hilo kujipatia mahitaji mkoani hapa.

MABOKSI BIASHARA KATIKA SOKO KUU LA MKOA WA MOROGORO.

admin
,
AKINAMAMA WAKAZI WA KIJIJI CHA MASEYU WILAYA YA MOROGORO VIJIJINI WAKIWA WAMEBEBA LUMBESA LA GUNIA LA MKAA WAKIELEKEA KWENYE LORI HALIPO PICHANI MARA BAADA YA MTEJA WAO KUNUNUA KATIKA KIJIJI HICHO KILICHOPO KANDO YA BARABARA KUU DAR ES SALAAM-MOROGORO AMBAPO GUNIA MOJA HUUZWA KIASI CHA 12,000 HADI SH 15,000 KULINGANA NA UKUBWA WAKE.

KAZI NI KAZI TU ILIMRADI MKONO UENDE KINYWANI, MWANAMKE KUJISHUGHULISHA.

admin
,
MSHAMBULIAJI WA KLABU YA TAIFA STARS YA TANZANIA SHOMARI KAPOMBE AKITAFUTA NAMNA YA KUMTOKA MCHEZAJI WA MALAWI MOSES CHAVULA KULIA WAKATI WA MCHEZO WA KIFARIKI ULIOFANYIKA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAPO ULIMAZIKA KWA SARE TASA YA 0-0.

MCHEZO WA TAIFA STARS DHIDI YA MALAWI HAKUNA MBABE.

admin
,
 
Mnyika akipongezwa na baadhi ya jamaa zake waliofika Mahakamani hapo.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika akiwa amebebwa na Wafuasi wake baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumtangaza jana kuwa mshindi halali katika matokeo yaliyompa ushindi katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010. Picha na Fidelis Felix.

NDEREMO na vifijo vya wapenzi na Chadema, jana viliitikisa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam baada ya Jaji Upendo Msuya kutupilia mbali madai ya aliyekuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia CCM, Hawa Ngh’umbi kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, John Mnyika wa Chadema.

Huu ni ushindi wa pili wa Mnyika dhidi ya Ngh’umbi baada ya kumshinda katika matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo la Ubungo, katika uchaguzi wa Oktoba 31, 2010.

Katika hukumu hiyo ya kurasa 57 aliyoisoma kwa saa 1:21 (kuanzia saa 4:10 hadi 5:31), Jaji Msuya alitupilia mbali hoja zote tano, ambazo pande zote ziliyakubali kama mambo yaliyokuwa tata, hivyo kuhitaji uamuzi  wa mahakama.

Jaji Msuya alitupilia mbali madai yote ya Ngh’umbi akisema ameshindwa kuyathibitisha mahakamani pasi na shaka, huku akidai kuwa ushahidi wa  shahidi wa kwanza (PW10 upande wa madai) ulikuwa ni maneno ya kusikia tu ambayo hakuyashuhudia.

Ngh’umbi alifungua kesi dhidi ya Mnyika akidai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa taratibu wakati wa mchakato wa kampeni na utangazaji matokeo.

Mbali na Mnyika ambaye alikuwa mdaiwa wa pili katika kesi hiyo wadaiwa  wengine walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambaye ni mshtakiwa wa kwanza na Msimamizi wa Uchaguzi (Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni).

Katika kesi hiyo namba 107 ya mwaka 2010, Ngh’umbi ambaye alikuwa akitetewa na Wakili Issa Maige, katika hati yake ya madai na wakati akitoa ushahidi wake mahakamani pamoja na mashahidi wake alidai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika uchaguzi huo.

Ngh'umbi alidai kuwa, ukiukwaji wa sheria ulifanywa katika mchakato wa ujumlishaji wa kura na utangazaji wa matokeo, hivyo uliathiri matokeo ya uchaguzi huo kwa ujumla wake.

Kutokana na madai hayo, Ngh'umbi aliiomba Mahakama pamoja na mambo mengine ibatilishe matokeo hayo na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo.

Hata hivyo, katika hukumu yake Mahakama ilitupilia mbali madai na maombi yote ya Ngh’umbi na kumthibitisha Mnyika kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Katika hukumu hiyo, Jaji Msuya alisema upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi wachache na kwamba, mlalamikaji huyo alipaswa kuwaita mahakamani baadhi ya watu kutoka upande aliokuwa akiulalamikia kwenda kumtetea.

Chadema walipuka
Hukumu hiyo ya Jaji Msuya iliamsha shangwe kubwa, makofi na miluzi miongoni mwa wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika ndani na nje ya mahakama hiyo, wakifuatilia hukumu hiyo kupitia kwenye spika zilizowekwa nje ya ukumbi wa mahakama.

Wakati Chadema wakichekelea, upande wa mlalamikaji Ngh’umbi na Wakili wake, Maige walielezea kutoridhishwa na hukumu hiyo huku wakielezea kushangazwa na sababu alizozitoa Jaji Msuya kutupilia mbali madai yao na kumpa ushindi Mnyika.

Kwa upande wao wafuasi wa Chadema walielezea kuridhishwa na hukumu hiyo huku Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe ambaye pia  alihudhuria mahakamani hapo akisema kuwa Mahakama imedhihirisha kuwa inatenda haki hata kwa wapinzani.

Katika hukumu yake, Jaji Msuya alisema  anatambua kuwa wingi wa mashahidi si kigezo cha kushinda kesi ila kuaminika na kukubalika kwa ushahidi wa mashahidi.

Alisema mlalamikaji alishindwa kuithibitishia mahakama madai yake kwa kushindwa kuwaita mahakamani mashahidi wengi zaidi ili kuunga mkono ushahidi wa mashahidi wake wawili.

Baadhi ya mashahidi ambao Jaji Msuya aliwataja kwamba walipaswa kuitwa  mahakamani na upande wa walalamikaji ni pamoja na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Lambart Kyaro na aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Rajabu Kiravu.

Kutokana na sababu hizo, Jaji Msuya alitupilia mbali madai yote ya Ngh’umbi akisema ameshindwa kuthibitisha madai yake katika hoja zote tano ambazo zilipaswa kutolewa uamuzi.

Hoja ambazo Ngh’umbi alipaswa kuzithibitisha mahakamani ni pamoja na kama mlalamikiwa wa pili (Mnyika), alitoa kauli za kashfa dhidi yake, kwa kumwita fisadi akimtuhumu kuuza jengo la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na iwapo kulikuwa na upungufu katika ujazaji wa fomu namba 21B ( fomu za matokeo ya kura za ubunge vituoni).

Hoja nyingine ni kama mlalamikiwa wa pili (Mnyika), aliingia na kompyuta (laptop) tano katika chumba cha majumuisho ya kura na kama ndizo zilizotumiwa na wasimamizi wa uchaguzi kuhesabu na kujumlishia kura pia kama Mnyika, aliingia na kundi la wafuasi wake katika chumba cha majumuisho kinyume cha sheria.

Hoja ya mwisho ambayo Ngh’umbi alipaswa kuithibitisha ni kama kulikuwa na makosa katika ujazaji wa Fomu namba 24B (fomu za matokeo ya jumla ya ubunge) hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi mzima.

Ushahidi
Akitoa ushahidi wake mahakamani, Ngh’umbi alidai kuwa matokeo hayo siyo sahihi kwa sababu pamoja na mambo mengine, katika fomu ya matokeo yaliyotangazwa kuna kura 14,854, zisizojulikana mahali zilikotoka huku Ngh’umbi na shahidi wake wakiziita kura hewa.

Alidai kuwa kwa mujibu wa fomu hiyo, kura halisi zilikuwa ni 119,823, kura halali zilikuwa ni 117,639 huku kura zilizokataliwa (zilizoharibika) zikiwa ni 2,184.

Lakini, wakati wakijitetea, mdaiwa Mnyika alikanusha madai hayo yote licha ya kukiri kuwepo kwa mkanganyiko wa usahihi na uwiano wa kura katika Fomu namba 24B. Hata hivyo, alidai kuwa dosari hizo zinaweza kurekebishwa na kwamba haziathiri matokeo kiasi cha kuyafanya yawe batili.

Mawakili wa utetezi, Justice Mulokozi kwa niaba ya AG na Edson Mbogoro kwa niaba ya Mnyika walidai kuwa mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha madai yake na hivyo, kuiomba mahakama iyatupile mbali.

Hata hivyo, wakili wa Ngh’umbi, Issa Maige alitamba kuwa wameweza kuthibitisha madai yao kwa kiwango kinachohitajika kisheria na kuiomba mahakama itengue matokeo hayo yaliyompa ushindi Mnyika.

Maige alisema madai mengine yameungwa mkono na mashahidi wa utetezi hususan DW1 aliyekiri Mnyika kuingia na kompyuta katika chumba cha majumuisho ingawa, alikanusha kuzitumia kufanyia majumuisho tofauti na Mnyika aliyekana kuingiza kompyuta hizo katika chumba hicho.

Pia wakili Maige alihoji sababu ya mawakili wa serikali kutokuwaita mahakamani baadhi ya mashahidi ambao walitajwa na upande wa madai na wa wadaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine, katika mchakato wa uchaguzi huo.

Wakili Maige aliwataja mashahidi hao ambao alidai walikuwa ni muhimu kuitwa mahakamani ili kujibu madai na kutoa ufafanuzi wa masuala yaliyowagusa kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mtaalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano wa Nec.

Mkurugenzi huyo alidaiwa kwamba ndiye alikagua kompyuta zilizotumika kufanyia majumuisho ya kura badala ya zile zilizotoka Manispaa ya Kinondoni kutokana na mfumo wa awali ulioandaliwa na Nec kuonekana kuwa haufai.

Maige alidai kuwa kitendo cha kushindwa kumwita mkurugenzi huyo mahakamani kutoa maelezo ya ukaguzi alioufanya na mbinu alizozitumia kuithibitishia mahakama kuwa katika kompyuta hizo isingewezekana kuingizwa taarifa za kughushi ni kinyume cha sheria.

Akirejea kesi ya Stanbic Bank (T) Ltd dhidi ya Woods (T) Ltd namba 48 ya mwaka 2002, alidai  Mahakama ilishatoa mwongozo kuwa ushahidi wa kitaalamu hauwezi kuthibitishwa kwa maneno matupu, pasipo mtaalamu kuitwa kuutolea ufafanuzi.

Wakili Maige alidai kuwa upande wa madai umethibitisha kuwa kompyuta zisizostahili kisheria ndizo zilizotumika kufanya majumuisho na kwamba, ndizo zilizosababisha kuwepo kwa mkanganyiko uliojitokeza katika fomu ya matokeo wa kura zaidi ya 14,000 zisizo na maelezo.

Hata hivyo, katika hukumu yake Jaji Msuya alisema jukumu la kuwaita mashahidi hao akiwemo mkurugenzi huyo na Kiravu lilikuwa ni la mlalamikaji na kwamba, kwa kushindwa kufanya hivyo ameshindwa kuthibitisha madai yake.

Kuhusu makosa katika ujazaji wa fomu namba 24, Jaji Msuya alikubaliana na hoja za utetezi  ni makosa ya kibinadamu akidai kuwa kulingana na mchakato wa jukumu hilo kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu ni jambo la kawaida kwa makosa kama hayo kutokea.

“Katika hitimisho langu nakubali kuwa hakuna hoja hata moja katika hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho kama ilivyodaiwa kuthibitishwa,” alisema Jaji Msuya na kuongeza:

“……ninatamka kuwa mdaiwa wa pili alichaguliwa kihalali kuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010 kwa kura 16, 198. Mdai atalipa gharama za uchaguzi”.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 31, Novemba 2, 2010 Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru  alimtangaza Mnyika kuwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho kwa kura 66,742 dhidi ya Ngh’umbi aliyepata kura 50,544 akimzidi Ngh’umbi kura 16,168.

Hata hivyo, Ngh'umbi hakuridhika na matokeo hayo ndipo alipofungua kesi hiyo Mahakama Kuu kupitia kwa Wakili wake Issa Maige akiiomba mahakama hiyo itengue matokeo ya uchaguzi huo.Polisi wazingira mahakama, shughuli zasimama

Waandishi Wetu


Aliyekuwa Mgombea ubunge jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Mapinduzi, Hawa Ngh’umbi akimshika kifuani kusikiliza mapigo ya moyo Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika kabla ya hukumu ya kupinga ushindi wake kusomwa na jaji katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix
JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dares Salaam jana liliimarisha ulinzi kwa kuweka askari zaidi ya 30 katika mahakama kuu kanda ya Dares Salaam wakati wa hukumu ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Ubungo, hukumu ambayo ilimpa ushindi  John Mnyika wa Chadema.

Wakati jeshi hilo likiimarisha ulinzi, baadhi ya shughuli katika eneo hilo zilisimama kwa muda. Katika viwanja vya mahakama hiyo, askari polisi zaidi ya 30 wakiwemo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walikuwa wametanda.

 Wafuasi wa CCM na Chadema walifika mahakamani hapo kuanzia saa 2.00 asubuhi na wengine wakiwa wamevalia sare za vyama vyao, lakini walilazimika kusubiri nje ya geti hadi saa 3:15 waliporuhusiwa kuingia ndani ya mahakama. Chadema waliongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

Mnamo saa 5:30 asubuhi baada ya Jaji Upendo Msuya kumaliza kusoma hukumu yake, wafuasi wa Chadema walianza kushangilia huku wafuasi wa CCM wakionekana kuwa na nyuso za huzuni na wengine waliangua kilio.

Wafuasi wa Chadema walikuwa wakishangilia huku wakiimba nyimbo mbalimbali na kunyanyua vidole viwili juu. Wafuasi hao walisikika wakisema, ‘peoples power (nguvu ya umma), mafisadi wameshindwa.’

Muda mfupi baadaye, Mnyika alitoka nje ya mahakama na kubebwa juu na wafuasi wa Chadema huku akishangiliwa. Wafuasi wa CCM walianza kuondoka taratibu katika viwanja vya mahakama hiyo na wengi wakionekana kuwa na nyuso za huzuni.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, Mbowe alisema “….lingekuwa pigo sana kama tungemkosa Mnyika kwasababu tunathamini kazi yake ndani ya chama, jimbo na taifa kwa ujumla”.

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema licha ya kuwepo kwa mahakimu na majaji wachache wasiokuwa waadilifu lakini ,bado wanaendelea kuiamini mahakama.

“Tunaishukuru mahakama imesimamia misingi ya sheria tunaiheshimu sana na tunaomba iendelee hivyo. Hii imeonyesha kuwa mahakama inaweza kutenda haki hata kwa wapinzani,”alisema Mbowe.

Alisema anakusudia kupeleka hoja bungeni kufanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi ili mtu anayefungua kesi bila hoja za msingi mbali na kulipa gharama za uendeshaji kesi pia aweze kuilipa Serikali kwasababu inatumia pesa nyingi kuendesha kesi. Mbowe alisema kesi hiyo imegharimu zaidi ya Sh1bilioni.

Hata hivyo, akitoa mchanganuo wa gharama za kesi hizo wakati kesi hizo zilipofunguliwa Jaji Kiongozi Fakih Jundu alisema kila kesi ingegharimu takribani Sh52milion na kwamba, kwa kesi zote 43 zilizokuwa zimeshafunguliwa zingegharimu zaidi ya Sh2bilioni.

 Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, alisema kesi hiyo ilifunguliwa kwa jazba bila kuwapo kwa ushahidi wowote na kushauri kuwa kama mtu hana ushahidi asikimbilie mahakamani.

Mwenyekiti huyo wa Chadema, alishauri pamoja na wadai kutakiwa kulipa faini pia wawe wanashtakiwa kwasababu wanaliingiza taifa katika hasara kubwa isiyokuwa ya msingi na kuchelewesha maendeleo.

Ngh’umbi kichwa chini
Saa 5:52 asubuhi baada ya hukumu hiyo,  Ngh’umbi alitoka nje ya mahakama akiwa ameongozana na wafuasi wachache wa chama chake. Akizungumza na waandishi wa habari alisema atakwenda kukaa na wakili wake ili wajipange.

“Sasa hivi bado ni mapema sana kusema nitafanya nini hadi nikae na wakili wangu nijipange,”alisema Ng’umbi huku akisindikizwa na wafuasi wake kwenda kupanda gari.
Mapema Saa 3:20 Ngh’umbi akiwa amevalia suti ya kijivu, alingia ukumbi namba moja wa mahakama Kuu, na kuketi kwenye benchi la mbele nyuma ya mawakili.

Dakika sita baadaye, saa 3:26 Mnyika aliingia ukumbini na kupokewa na wafuasi wa Chadema kwa kumpigia makofi. Mnyika alikuwa amevaa sare za chama chake zenye rangi ya khaki maarufu kama kombati.

Mnyika alijibu kwa kuwapungia mikono na kwenda hadi benchi alilokuwa amekaa Ngh’umbi ambako, walisamiliana kwa kupeana mikono kisha alikaa kushoto kwake na kuanza kuzungumza wakati wakisburi Jaji Msuya kuingia mahakamani.

Wakati fulani Ngh’umbi alionekana akimgusa Mnyika kifuani mithili ya mtu aliyekuwa akimpima mapigo ya moyo.

Mbowe ndiye aliyeonekana kivutio zaidi baada ya kuingia ukumbini humo, saa 3:45 naye akiwa amevaa kombati. Kuingia kwa Mbowe kuliwafanya wafuasi wa Chadema kulipulika kwa shangwe kubwa huku wakimpigia makofi na kelele.

Mbowe alikwenda kwa Mnyika wakasalimiana kisha alikaa kwenye benchi lililokuwa nyuma ya benchi, walilokaa Mnyika na Ngh’umbi na kusubiri kusomwa kwa hukumu.

Dakika 11 baadaye baada ya Mbowe kuingia ukumbini, saa 4:08, Jaji Msuya aliingia mahakamani na kukaa kwenye kiti chake. Alianza kusoma hukumu hiyo saa 4:10 hadi saa 5:30 alipohitimisha.

Shughuli zasimama
Ushindi huo wa Mnyika ulisababisha shughuli mbalimbali katika baadhi ya mitaa ya jiji kusimama kwa muda kutokana na maandamano yalioyoanzia Barabara ya Kivukoni hadi eneo la Kimara kona, zilipo ofisi za Mbunge huyo.
Maandamano yalikuwa yakiongozwa na Mbunge huyo huku magari ya FFU yakifuatilia kwa karibu.

Awali, polisi walimshauri Mnyika apande gari ili kuzuia maandamano yasiendelee, lakini wafuasi wake walikataa na kumwambia Mbunge wao asikubali na kusisitiza: ”tunakuomba Mheshimiwa utusikilize sisi hakuna kupanda gari tutatembea na wewe mpaka kwenye ofisi zetu”.

 Wakati msafara huo ulipokuwa njiani, ulizuiwa na wafanyabishara ndogondogo eneo la Manzese na eneo la  Big Brother lililopo njia panda ya Mabibo waliotaka kuongea na Mnyika ili kumpongeza.

Hata hivyo, ombi hilo halikuwezena badala yake walishauri kujiunga katika  msafara huo kuelekea katika ofisi za mbunge huyo.

 Hali kama hiyo ilijitokeza pia katika eneo la Ubungo stendi ya mkoa ambako, vijana walijaa barabarani na kuzua msafara wakitaka aingie ndani stendi ili wampongeze hata hivyo, nao pia walishauriwa wajiunge kwenye msafara.  Mbunge huyo baada ya kufika katika Ofisi za Chadema jimbo la Ubungo, alipanda juu ya gari  na kuanza kuwahutubia wafuasi wake waliofurika katika ofisi hizo.

 “Napenda kuwapongeza wananchi wa jimbo langu na wapenzi wa Chadema,vijana ,wanawake na wazee mliojitokeza kwa wingi kuanzia mahakamani hadi hapa tulipo kwa kujitolea muda wenu na kuacha kazi zenu na kuungana na mimi.Na hiyo haikuanza leo bali mlifanya hiyo tangu  kesi ilipoanza hadi leo tumeisha, nawapongeza sana,” alissema Mnyika.

Aliongeza: “Nilikuwa katika kipindi kigumu cha kushughulikia matatizo ya jimbo langu na wakati huo, kushughulika  kesi kitu ambacho kilikuwa kinaniweka katika wakati  mgumu.”

“Sasa Mahakama imeishatenda haki na mimi Mbunge halali, nitaanza kushughulikia matatizo ya wananchi ….nitaanza na mpango wa kuanzisha mfuko wa elimu wa jimbo ambao utasomesha watoto ambao wazazi hawana uwezo. Katika mpango huo nategemea kufanya harambee na kukusanya kiasi cha Sh.100milioni.”

Wakati akihitimisha hotuba yake, aliwataka wafuasi kutoondoka eneo hilo bali wauungane naye katika hafla fupi ya kusherekea ushindi ambapo aliagiza ng’ombe mzima kuchinjwa huku wengi wakijitolea michango kwa ajili ya kununulia vinywaji.
Mmoja wa wake wa Osama Bin Laden.
Wakili wa wajane wa Osama Bin Laden na mabinti zake Atif Ali Khan ameeleza kuwa familia hiyo imepewa kifungo cha siku 45 kila mmoja kwa kuishi nchini Pakistan pasipo bila kibali. 

Khan aliyasema hayo wakati akizungumza na shirika la habari la BBC na kueleza kuwa wanawake hao wameanza kutumikia vifungo vyao na wanatarajiwa kurejeshwa nyumbani kwao katika majuma mawili yajayo.

Wajane wawili ni raia wa Saudi Arabia huku mwenzao wa tatu akiwa mzaliwa wa yemen. 
Wakili huyo alisema kuwa wameshauriana na serikali ya Saudi Arabia kuwakubalia wajane wawili kurejea nyumbani huku mjane anayetoka Yemen akikubaliwa kurudi nyumbani.

Wajane watatu walichukuliwa na maafisa wa usalama baada ya Osama Bin Laden kuuawa katika operesheni ya kikosi maalum cha Marekani nchini Pakistan hapo mwezi Mei.

WAKE WA OSAMA BIN LADEN WATUMIKIA KIFUNGO CHA SIKU 45.

admin
,

TAARIFA YA KUSIKITISHA.

 
Mbunge wa Rombo-Kilimanjaro Mhe, Joseph Roman Selasini amepata ajali ya ya gari huku mama yake mzazi akiripotiwa kupoteza maisha iliyotokea katika eneo la Boma Ng'ombe mkoani Kilimanjaro.

Taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma zinasema kuwa Mhe Selasini alikuwa akiendesha gari yake huku ikidaiwa kuwa na watu sita ambapo kati yao watu watatu hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya.


Kamanda huyo akiongea na waandishi wa habari kwa simu ya alisema kuwa kwa sasa hawezi kuthibitisha kwamba ni watu wangapi wamepoteza maisha katika ajali hiyo na kuongeza kuwa majeruhi wote wamekimbizwa katika hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma.

Mwakyoma alisema kuwa taarifa zaidi atazitoa muda mfupi  baada ya kujua hali halisi ya tukio hilo kwani kwa sasa yuko njiani akielekea eneo la tukio kisha kwenda hospitali kuangalia majeruhi wa ajali hiyo.

HABARI MPYA !!!!!!!! MBUNGE WA ROMBO APATA AJALI, MAMA YAKE ADAIWA KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO.

admin
,
KWA UHONDO WA KATUNI: ZENYE UJUMBE MBALIMBALI IKIWEMO KUELIMISHA, KUCHEKESHA, KUKOSOA N:K TEMBELEA: WWW.SIDYMIC.BLOGSPOT.COM.

KATUNI

admin
,
FUNDI WA KUKARABATI MIAMVU KATIKA MANISPAA YA MOROGORO AKIFANYA KAZI HIYO HUKU MTEJA WAKE AKISUBIRI ILI AKATUMIA KUJIKINGA NA JUA WAKATI AKIFANYA BIAHSRA NDOGO NDOGO KATIKA MTAA WA ISLAMA MKOANI HAPA.

MWAMVULI NATENGENEZA.

admin
,
Vifaru vya AMISOM katika shughuli zake za kijeshi dhidi ya kundi la Al-Shabab nchini Somalia.

Kikosi cha AMISOM kimezindua kampeni katika wilaya ya Daynile na magharibi ya Mogadishu dhidi ya wanamgambo wa kundi la Al-Shabab.

 Vikosi vya Somalia kwa kuungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika yamezindua  kampeni kali  ya kutimua wanamgambo wa al-Shabab katika vitongoji vya Mogadishu  hususan kwenye ukanda wa Afgoye.

Maafisa wa ulinzi wanasema lengo la kampeni hiyo ni kuleta uthabiti  na amani kwa watu 400,000 waliofurushwa makwao katika eneo la Afgoye lililoko magharibi ya mji wa Mogadishu.  

Hii ni mara ya kwanza vikosi vya Umoja wa Afrika  na majeshi ya kitaifa ya Somalia  kuungana pamoja kushambulia vituo vya wanamgambo wa al-Shabab nje ya Mogadishu.

Msemaji wa kikosi cha Umoja wa Afrika kinachojulikana kama AMISOM- Paddy Ankunda, aliiambia Sauti ya Amerika kuwa  kampeni dhidi ya al-Shabab ilizinduliwa katika wilaya ya Daynile na kuelekea magharibi mwa Mogadishu kuingia katika eneo la Afgoye.


Alisema wilaya ya Daynile sasa imo mikononi mwa majeshi ya AMISOM na kwamba wanapigania kijiji kidogo kiitwacho Elasha Biyaha kilichoko karibu na Afgoye na ripoti za hivi karibuni alizopata  ni kwamba majeshi ya Umoja wa Afrika  sasa yanadhibiti asilimia 85 ya kijiji hicho.

Eneo la Afgoye lina watu 400,000 waliofurushwa makwao kwenye eneo la kilomita 30 mraba kutoka mji mkuu wa Mogadishu.

 Ni mahala ambapo watu wengi  kutoka Mogadishu wamepiga kambi katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya mji huo mkuu kushambuliwa kwa risasi kila siku katika mapigano baina ya  vikosi vya serikali na wanamgambo wa al-Shabab.

Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yameeleza wasiwasi wao juu ya raia wanaojeruhiwa  katika mtafaruku huo na kuziomba pande zote kuepuka kutumia nguvu na kupigana kiholela  ambapo raia wanajikuta wamenaswa kwenye mapigano hayo.

Vikosi vya Umoja wa Afrika vilifanikiwa kiasi kikubwa kutimua wanamgambo hao wa Kiislam mwaka jana mjini Mogadishu  na kuimarisha kwa kiwango kikubwa mji huo mkuu. 

Lakini eneo la Afgoye ni mojawapo ya maeneo yaliyobaki mikononi mwa wanamgambo wa al-Shabab.

Wanamgambo hao walilifanya eneo hilo kuwa ngome yao ambapo walikuwa wakiwaandikisha wanachama wapya na hata kuwapa mafunzo na pia kulifanya eneo kuwa la mkutano wa viongozi wake ambapo  wanaeneza propaganda zao.

KAMPENI KALI YAZINDULIWA DHIDI YA AL-SHABAB

admin
,

Rais wa Mpito wa Mali, Dioncounda Traore.

 WAKUU wa serikali nchini Mali wamesema kuwa Rais wa Mpito, Dioncounda Traore, amepelekwa eneo salama baada ya kupigwa hadi kuzirai na mamia ya waandamanaji nchini humo.

Mamia ya waandamanaji walimshambulia Rais Traoure wakipinga mkataba ulioafikiwa na Tume ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika, ECOWAS, ambapo Traoure ataendelea kutawala kwa hadi mwaka mmoja badala ya siku 40 pekee zilizokubaliwa miezi miwili iliyopita. 

Mwandishi wa BBC amesema kuwa shambulio hilo litawashtua wanadiplomasia waliokuwa wakifanya kila juhudi kurejesha amani na utangamano nchini humo.

Muda wa kuongoza aliopewa kiongozi huyo, Djouncounda Traore ulitarajiwa kukamilika Jumatatu.

Lakini viongozi wa nchin za Magharibi mwa Afrika, waliafikia mkataba na kiongozi wa mapinduzi Kapteni Amadou Sanogo kwamba BwTraore asalie mamlakani ili aweze kuongoza harakati za uchaguzi na kumaliza harakati za waasi wa Tuareg.

Mkataba huo pia ulijumuisha mpango wa kukubalia Sanogo atajwe kama kiongozi wa zamani alipwe mshahara wa rais na apewe nyumba ya kifahari.

Mapinduzi hayo pamoja na harakati za waasi kuteka Kaskazini mwa Mali, yamesababisha maelfu ya watu kutoroka makwao.

Mashirika ya misaada wanasema wana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu nchini Mali nchi ambayo pia inakumbwa na baa la njaa.

Mwandishi wa BBC mjini Bamako, Martin Vogl amesema kuwa wanajeshi waliwaruhusu baadhi ya waandamanji kuingia katika ikulu ya rais ingawa bwana Traore hakuwepo wakati huo.

RAIS WA MPITO WA MALI YUPO SALAMA BAADA YA KIPIGO CHA WANANCHI WALIOVAMIA IKULU YA NCHINI HIYO..

admin
,

Mwanafunzi wa darasa la awali kitengo cha viziwi katika shule ya msingi Kilakala Manispaa ya Morogoro, Benadetha Gaudence (7) akijifunza namna ya kuunganisha vipande kwenye ubao ili kuunda ramani ya Afrika kwa wanafunzi wenye ulemavu huo wakati wa somo la vitendo vya montesor shuleni mkoani hapa.

MAFUNZO KWA VITENDO SHULE YA AWALI KITENGO CHA VIZIWI SHULE YA MSINGI KILAKAKA MANISPAA YA MOROGORO.

admin
,
JUMUIYA ya kujihami ya NATO imesema kuwa itakabidhi jukumu la ulinzi wa Afghanistan kwa nchi hiyo katikati ya 2013 pamoja na kutangaza kuanza mfumo wake mpya wa kinga ya makombora barani Ulaya utakaokamilika 2020.


Kutangazwa kwa hatua hiyo kumezusha hali ya kutoelewana baina ya NATO na Urusi ambayo imeendelea kusisitiza ipatiwe uhakika wa kisheria unaothibitisha kuwa mpango huo hauilengi nchi hiyo. Marekani yenyewe imeweka bayana shabaha yake katika mpango huo ni kuwa ni kujilinda dhidi ya Iran.Akizungumza baada ya kutangazwa rasmi kwa mpango huo kwenye mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo unaoendelea mjini Chicago Marekani, Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa Urusi haina haja ya kuhofia hatua hiyo.Baadae Rasmussen aliwaambia waandishi wa habari kwamba jumuiya hiyo ina lengo la kuendelea na mazungumzo na Urusi ikiwa na matumaini kuwa nchi hiyo itaielewa hatua yake hiyo kuwa ni sehemu ya mpango wake muhimu na wa muda mrefu katika kujihami na makombora.Mapema siku ya Jumapili Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Anatoly Antonov aliionya NATO kuhusu hatua hiyo ya kuendelea na mpango wake wa kutengeneza mfumo mpya wa kujikinga na makombora kwa nchi za ulaya akisema kitendo hicho kitavuruga amani ya dunia.

Antonov alitishia pia kuwa nchi yake itachukua hatua za kijeshi kama mpango huo utaendelezwa.

Mpango wa kuondolewa vikosi vya NATO Afghanistan.


Mkutano huo wa kilele wa NATO umezungumzia pia suala la kuondoka kwa vikosi vya kigeni vinavyolinda amani nchini Afghanistan ambapo maamuzi yaliyofikiwa ni kwamba nchi hiyo itakabidhiwa jukumu la kujilinda katikati ya mwaka 2013.Mkutano wa NATO mwaka 2012 , Chicago Marekani.Katika siku yake ya pili leo, mkutano huo utajadili mbinu ya kuondolewa taratibu vikosi vyao nchini Afghanistan, kama ilivyopendekezwa na Marekani .

Lengo ni kuziunganisha nchi zote zinazoshiriki katika kulinda amani nchini Afghanistan, kutimiza lengo hilo kwa pamoja baada ya Ufaransa kuonyesha nia ya kuviondowa vikosi vyake kabla ya muda uliopangwa mwaka 2014.

Kufikia wakati huo vikosi vyenye jumla ya wanajeshi 130,000 vitakuwa vimeshaondoka.


Hata hivyo, Rais wa Ufaransa Francois Hollande baadae alitangaza kuwa amefikia makubaliano na wenziwe wa NATO kuhusu uamuzi wake wa kujiondoa mapema akisema wameelewa hali aliyonayo.


Hali ya kutaka kuziridhisha pande zote mbili.Nchi wanachama wa NATO wanataka kuwaonyesha wananchi wao wanaopinga serikali zao kujiingiza kwenye vita kuwa hali hiyo inafikia kikomo, lakini pia kwa upande mwingine wanataka kuwaambia Waafghan kuwa hawatawatelekeza.Mataifa hayo yanapata upinzani mkali kutoka kwa wapiga kura ambao wanaona kuwa kujihusisha kwao kwenye vita hivyo kunazigharimu serikali zao kiuchumi.


Rais wa Afghanistan Hamid Karzai akizungumza na Rais Barack Obama wa Marekani.Rais wa Afghanistan Hamid Karzai akizungumza na Rais Barack Obama wa Marekani.

Kwa upande wake Rais wa Afghanistan Hamid Karzai amesema kuwa anaisubiri siku ambayo nchi yake haitakuwa tena mzigo kwa jumuiya za kimataifa, kauli aliyoitoa wakati akizungumza na Rais Barack Obama wa Marekani pembezoni mwa mkutano huo.

NATO KUKABIDHI JUKUMU LA ULIZNI AFGHANSTAN 2013

admin
,
HALI bado siyo shwari Ikwiriri wilayani Rufiji, baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba ya Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), kuivunja na kuharibu mali huku wengine wakichoma moto magari na nyumba wananchi.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilidai kuwa, vurugu hizo ziliibuka usiku wa kuamkia jana kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji eneo hilo.

Wakati hayo yakiendelea, watu 49 kutoka jamii ya wafugaji wamehamia na kuishi na familia zao Kituo cha Polisi Ikwiriri, kuepuka vurugu zinazoendelea mitaani ambazo juzi ziliripotiwa kupoteza maisha ya mkulima mmoja.

Ingawa polisi wanasema hali ni shwari, taarifa zilizothibitishwa na watendaji wa chini zinaeleza siyo shwari na wakati wowote vurugu zinaweza kurudi tena.

Katika eneo la Ikwiriri inakopita barabara kuu ya Dar es Salaam- Mtwara, jana biashara ya maziwa iliyokuwa ikifanywa na wake wa wafugaji haikuwapo, inadaiwa wamehofia usalama wao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema hadi saa 4:00 asubuhi jana hali ilikuwa shwari na kwamba, wanaendelea kufanya doria za ili kujiridhisha.

Pia, Mangu alisema lengo la doria hizo pia ni kuhakikisha kinachosemwa na baadhi ya watu kuwa, kuna dalili za kurejea vurugu iwapo ni kweli au la.

Mangu alisema hadi jana asubuhi walikuwa wanashikilia watu 50 kwa tuhuma za kufanya vurugu, ikiwamo kufunga barabara na kuharibu mali kadhaa.

Alisema wanaoshikiliwa siyo wafugaji wala wakulima, hivyo kama kuna taarifa za kuwapo ulipizaji kisasi siyo sahihi kwani kati ya makundi hayo hakuna kundi lililochukuliwa zaidi ya vijana wa mjini waliokuwa wakifanya vurugu.

“Sisi hatujawakamata wafugaji au wakulima, katika operesheni ilikuwa ya kukamata watu waliokuwa wakifanya vurugu ndiyo tunaowashikilia, sasa ukisema kuna madai ya wafugaji kutaka kulipiza kisasi hapo nashangaa kwa maana mbili, kwanza siku ya fujo hakuna hata mfugaji mmoja aliyelipiza kisasi kwa mkulima,” alisema Mangu na kuongeza:

“Kweli wafugaji walionyesha kutii walau sheria kwa sababu, licha ya baadhi ya watu kudai wakulima wanawashambulia, wao walikuwa hawajajibu mashambulizi ndiyo maana vurugu hizi tumeweza kufanikiwa kuzizima mapema, lakini kama wafugaji nao wangeenda kuwapiga wakulima hapo sasa kazi ingekuwa ngumu.”

Kuhusu madai ya ofisa mmoja wa jeshi hilo kuhamishwa kituo cha kazi siku hiyo ya tukio, Mangu alisema hana taarifa hizo.

NYUMBA YA MKUU WA POLISI WILAYA YA RUFIJI (OCD) YAVUNJWA BAADA YA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI.

admin
,

Mshambuliaji wa kanda ya Kihonda B, Emelina Aman kulia akiwania mpira dhidi ya beki wa kanda ya Sua, Emelina Aman wakati wa mchezo wa soka kwa wasichana katika mashindano ya kusaka wachezaji wakuunda vikosi vya umoja wa michezo shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 yanayoendelea katika uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

 Moja wa wasichana wakichuana katika mbio za mita 400 kwenye uwanja huo wa Jamhuri.
 Wanafunzi wa kanda ya Mjini Kati wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa mashindano ya umoja wa shule za sekondari Tanzania ambapo wanafunzi zaidi ya 750 wanashiriki mashindano hayo kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Wanafunzi wa kanda ya SUA
Wanafunzi wa kanda ya Tungi

 Wanafunzi wa kanda ya Kihonda B

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo amewataka wakufunzi na walimu wa michezo mbalimbali katika mashindano ya umoja wa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) kuwa makini wakati wa kuchagua wachezaji wa wilaya ya Morogoro ili kusaidia kupata wachezaji wazuri wataowakilisha vema mashindano ngazi ya mkoa huo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ngazi ya halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika uwanja wa jamhuri mjini hapa, Nondo alisema kuwa ili kupata wachezaji wazuri wa kuwakisha michezo ya Umisseta ngazi ya mkoa ipo haja kwa wakufunzi na makocha kuwa makini wakati wa kuangalia wachezaji ambao wataunda vikosi vya michezo mbalimbali katika mashindano hayo.

Nondo alisema kuwa mashindano hayo ni mazuri sana na lengo la kuanzishwa kwake ni kuibua vipaji vilivyojificha na kuviendeleza hivyo wakufunzi hapo wanahitajika kuwa makini katika kuangalia vijana hao kwa kila mchezo ili timu zitakazoundwa za wilaya ya Morogoro ziwe imara na kutwaa ushinda na hiyo itasaidia sana wachezaji wengi wenye vipaji kupata nafasi ya kuendeleza kwenye hatua zinazoendelea.

“mashindano haya ya Umisseta ni mazuri sana kwani yamekuwa yakiibu wachezaji wenye vipaji vingi vya kila aina ya mchezo hivyo umakini wa wakufunzi na makocha wa kuchagua wacvhezaji unahitajika sana ili Manispaa tupate timu imara” alisema Nondo.

Aliongeza kuwa ukiwa na wachezaji wazuri lazima utakuwa na timu imara lakini itakuwa faida kubwa  kwa wachezaji hao kupata nafasi mzuri ya kuendelea kuonyesha vipaji vyao.

Naye Afisa Michezo Manispaa ya Morogoro, Asteria Mwang’ombe alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha jumla ya kanda sita ambazo katika kanda zao tayari zilifanya michezo na kupata wachezaji ambao wameunda vikosi vya timu mbalimbali.

Mwang’ombe alitaja michezo ambayo inashindaniwa ni pamoja na soka, netiboli, baskeboli, bao, mpira wa wavu, meza, riadha, na taaluma ambazo washiriki wanatoka katika kanda sita za shule za sekondari za Mjini kati, Bigwa, Kihonda A, Sua, Kihonda B, na Tungi.

UMISSETA UNAVYOIBUA VIPAJI VYA MICHEZO MBALIMBALI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO.

admin
,Mbunge wa Mufindi Kusini Bw. Mendrad Kigola akingaliwa na Muhuguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Oliva Msimbwa baada ya kupata ajari eneo la Ieme mkoani humo  hali ya Mbungo huyo inaendelea vizuri na ana tarajiwa kulusiwa wakati wowote ule.

MBUNGE WA MUFINDI KUSINI APATA AJALI.

admin
,
RAIS wa Malawi, Joyce Banda amesema kuwa anataka nchi hiyo ibatilishe sheria inayoharamisha ndoa za jinsia moja na kuifanya nchi ya kwanza ya kiafrika kufanya hivyo tangu mwaka 1994.

Wananume wawili raia wa nchi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani mwaka 2010 baada ya kutangaza kuwa wanataka kuoana.

Baadhi ya viongozi wa nchi za magharibi, hivi karibuni wametishia kusitisha msaada kwa nchi za kiafrika ambazo hazitatambua haki za mashoga.

Rais Banda alichukua hatamu za uongozi mwezi jana kutoka kwa mtangulizi wake, Bingu wa Mutharika, aliyeaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo.

Hadi sasa rais huyo amegeuza baadhi ya sera zake ikiwemo kushusha thamani ya sarafau ya nchi kwa lengo la kuanza kupata msaada .

Wafadhili wengi walisitisha msaada chini ya utawala wa Mutharika, wakimtuhumu kwa uongozi duni pamoja na ukandamizaji.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge la anchi Banda alisema kuwa baadhi ya sheria zilizopitishwa na bunge, zitafutiliwa mbali kama hatua ya dharura ikiwemo sheria zinazopinga vitendo visivyo vya kawaida.

Mwandishi wa BBC Raphael Tenthani mjini Blantyre, anasema kuwa rais anaungwa mkono na wabunge wengi, na kwa hivyo ataweza kuwashawishi wabunge kubatilisha sheria hiyo.

RAIS BANDA: KUBATILISHA SHERIA YA NDOA YA JINSIA MOJA

admin
,
 Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akitoa heshima za mwisho wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu, Patrick Mafisango.
 Mlezi wa klabu ya simba, Prof. Philimon Sarungi akimfariji Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage kushoto.
KIUNGOWA MSHAMBULIAJI WA SIMBA  HAROUN MOSHI (BOBAN).

KIUNGO wa Azam, Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema kifo cha Patrick Mafisango ni pigo kubwa kwake kutokana ndiye alimtaka aondoke Maisha Club ili akalale muda mfupi kabla ya kifo chake.

Redondo aliyekuwa na marehemu Mafisango kwenye ukumbi wa Maisha Club hadi saa 7 usiku ambako Mafisango alimtaka aondoke kwa madai kuwa muda ulikuwa umekwisha.

Akizungumza kwa shida kutokana na kuelemewa na uzito wa msiba huo alisema haelewi ni nini kimetokea na kwa nini alimfukuza pengine wangekuwa wote kwenye safari ya kurudi.

"Tulikuwa wote hadi mwisho kwenye ukumbi wa maisha klabu, lakini ilipofika muda ya saa saba nane kasorobo  Mafisango alinifukuza na kunichukulia taxi nirudi nyumbani na kuniaambia muda umeisha yeye atarudi na jamaa zake ambao alikuwa nao akiwemo mtoto wa dada yake,"alisema na kuongeza

"Nilikubali nikaondoka cha kushangaza napata taarifa alfajiri kuwa Mafisango amefariki Mungu amefanya kazi yake kumchukua, lakini mimi imeniathiri kutokana na mambo mengi niliyoongea nae"alisema na kushindwa kuendelea kuongea.

Alifafanuwa kuwa aliongea mambo mengi na Mafisango ambayo akiyakumbuka haamini kilichotokea, na bado haelewi nini aseme kuhusu kifo hiki cha ghafla cha rafiki yake huyo.

Tangu kutokea kwa msiba huo Redondo amekuwa hajielewi na muda mwingi anakuwa kama amezimia ingawa baadae hurudi kwenye hali ya kawaida.

Wakati huohuo; Kwa siku ya pili mfululizo kiungo wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' ameendelea kuwa 'Bubu' huku akilia muda wote kufuatia msiba wa swahiba wake Patrick  Mafisango.

Boban aliyeguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huo tangu kufariki kwa mchezaji huyo amekuwa katika hali isiyo ya kawaida huku akikataa kabisa kuzungumza na mtu na muda wote akionekana mwenye huzuni kubwa na machozi yakimtoka mfululizo.

Wakati taratibu za kusoma risala kwa watu mbalimbali zikiendelea Boban alishindwa kujizuia na kuinuka kutoka alipokuwa amekaa na kwenda moja kwa moja karibu na jeneza na kukaa chini huku akilia na kushindwa kuzungumza lolote mpaka alipoletewa kiti.

Aidha baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa waliiambia Mwananchi jana kuwa Boban hakuwa katika hali nzuri tangu aliposikia kifo cha Mafisango ambaye wamedai alikuwa wawili hao walikuwa ni zaidi ya rafiki kutokana na ukaribu wao wakati wote akiwa hapa nchini.

"Tangu tukio litokee Boban amekua katika hali hii hii na amekua hazungumzi lolote, hivi tunavyokwambia asubuhi ameamka akaja moja kwa moja bila kuaga mtu na amekuja huku bila ya viatu 'pekupeku' hata mswaki hakupiga tulichofanya ni kumnunulia viatu na tumejaribu kuwa naye karibu ili kumwondolea hali hii," walisema wachezaji wenzake.

Boban ndiye mchezaji aliyependekezwa kwenda kumzika Patric Mafisango jijini Kinshasa,Congo ambapo anataraji kuondoka leo alfajiri na mwili pamoja na baadhi ya viongozi wa Simba ambao wataambatana pamoja.

KIUNGO WA KLABU YA AZAM, RAMADHAN CHOMBO AELEZA KUWA KIFO CHA MAFISANGO NI PIGO KUBWA.

admin
,
GARI ALILOPATA NALO AJALI HADI KUPELEKEA KIFO KWAKE KIUNGO MSHAMBULIAJI WA KLABU YA SIMBA PATRICK MUTESA MAFISANGO MAJIRA YA SAA 8:45 USIKU MEI 17 ENEO LA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM.
                                                          
          BEKI WA SIMBA JUMA NYOSO PAMOJA NA HOHN BOKO WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LENYE MWILI WA KIUNGO MSHAMBULIAJI WA KLABU HIYO YA SIMBA PATRICK MAFISANGO VIWANJA VYA TCC CLUB KWA AJILI YA KUAAGA KABLA YA KWENDA NCHINI KONGO DRC AMBAPO ATAZIKWA KIPENZI CHETU.
                                      
PATRICK MUTESA MAFISANGO ENZI ZA UHAI WAKE.

SIMANZI, huzuni na vilio viliwatawala wanamichezo nchini baada ya kupata taarifa za kifo cha kiungo wa kimataifa wa Rwanda na Simba, Patrick Mutesa Mafisango (32) aliyefariki dunia jana alfajiri kwa ajali ya gari.

Mafisango anatarajiwa kuagwa leo kwenye Uwanja TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es Salaam kabla ya kesho kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao DR Congo kwa mazishi .


Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema taratibu za kuuaga mwili wa marehemu zitaanza saa nne asubuhi mpaka saa 10 jioni.

Mafisango alipata mauti hayo eneo la Veta Chang'ombe usiku wa kumkia jana saa 8.45 alipokuwa akiendesha gari akitokea Maisha Club akiwa na wenzake wanne na alipofika maeneo ya Veta wakati akijaribu kumkwepa mwendesha baiskeli ya miguu mitatu 'Guta' gari lilimshinda na kugonga mti uliosababisha gari yake kuingia mtaroni na mauti kumkuta hapo hapo.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo mtoto wa dada yake Orly Ilemba (24) aliyekuwamo katika gari hilo alisema jana wakati wanavuka mataa ya Veta, marehemu alikuwa katika mwendo kasi mara mbele akakutana na Guta na katika jitihada za kulikwepa akagonga mti na gari kupinduka na kutumbukia mtaroni na mauti kumkuta hapo hapo.

"Tulitoka salama Maisha Club tunarudi nyumbani marehemu alikuwa akiendesha gari katika mwendo wa kasi, tulipovuka mataa ya Veta wakati akiwa 'spidi' tuliona guta kwa mbele yetu pamoja na pikipiki sasa wakati marehemu anakwepa kwa bahati mbaya aligonga mti na gari ikadumbukia ndani ya mtaro huku nikishuhudia kichwa cha ndugu yangu kikigeukia chini kwenye sehemu ya breki na miguu kuja juu kumbe tayari alishafariki......ndipo tukaanza taratibu za kumkimbiza hospitali," alisema Ilemba.

Aliongeza kuwa,"ndani ya gari hiyo aina ya Gx100 tulikuwa watu jumla ya watano mimi, Gaspar Karemera, Bozy na mwanamke mmoja ambaye yeye hatukumfahamu jina lake mara moja akiwa amekaa mbele na marehemu ambaye mpaka sasa bado yupo hospitali akiendelea na matibabu baada ya kuumia sana maeneo ya kichwani,"alisema Ilemba.

Akithibitisha kifo cha mchezaji huyo, Mkuu wa Trafiki katika mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Prackson Lugazia alisema ajali hiyo ilitokea wakati Mafisango aliyekuwa akiendesha gari aina ya GX 100 akitoka Maisha Club akiwa na familia yake akijaribu kumkwepa mwendesha Guta.

Alisema hali hiyo ilisababisha gari hilo kuacha njia na kuingia mtaroni na kugonga miti mitatu kisha kugeuka na kuangalia lilikokuwa likitoka na baadaye kupinduka.

"Baada ya kupata taarifa za ajali hiyo majira ya saa 10 asubuhi tulifika eneo la tukio haraka iwezekanavyo, lakini hatukukuta mtu yeyote zaidi ya gari lililokuwa limepinduka,"alisema Lugazia.

Alisema,"kufatia hali hiyo ndipo tulipoanza taratibu za kumtafuta marehemu na tulianzia hospitali ya Amana, tulikwenda hospitali ya Mwananyamala na baadaye Muhimbili ambako tuliukuta mwili wake pamoja mwanamke mmoja ambaye alikuwa na majeraha mbalimbali sehemu za mwili wake," alisema Lugazia.

Akizungumza jana alfajiri jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema,"ni kweli Mafisango hatunaye tena, kwa sasa siwezi kuzungumza chochote huyu ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda, ndiyo nafanya mawasiliano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na lile la Rwanda (FERWAFA) kuangalia namna ya kuusafirisha mwili wake."

Mafisango amefariki akiwa amemaliza mkataba wake na Simba na alitarajiwa kusaini mkataba mpya juzi na leo alitarajiwa kwenda Rwanda tayari kujiunga na kikosi cha timu hiyo 'Amavubi' kinachojiandaa kwa ajili ya mechi za mchujo za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2014, zitakazochezwa mwezi ujao.

Kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda, Sredojevich Millutin 'Micho' akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu alisema,"nimeshtuka sana, siamini Mafisango amefariki, niliongea naye jana (juzi) na nimemtumia tiketi ya ndege kwa ajili ya kujiunga na timu na nilikuwa namsisitiza asichelewe na alinihakikishia Ijumaa (leo) atakuja."

"Ukiniambia amefariki sikuelewi hapa nilipo nimechanganyikiwa, kuna vikao vinaendelea (jana), nitakupigia baadaye,"alisema Micho huku sauti yake ikionekana kuwa na majonzi.

Wakati huohuo; Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Patrick Mafisango kilichotokea leo (jana) alfajiri kwa ajali ya gari Dar es Salaam.

TFF ilisema msiba huo ni mkubwa kwa familia ya mpira wa miguu kwani Mafisango kwa kipindi chote alichocheza mpira hapa nchini akiwa na timu za Azam na baadaye Simba, aliifanya kazi yake (kucheza mpira) kwa bidii.

Kifo chake ni pigo kubwa sio tu kwa familia yake na timu alizochezea, bali Ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati ambapo changamoto za Mafisango zilikuwa dhahiri uwanjani.

BOBAN:
 
Rafiki mkubwa wa Mafisango kiungo Haruna Moshi 'Boban' alikuwa kwenye majonzi makubwa huku machozi yakimtoka bila kuzungumza lolote.

Wakizungumzia ukaribu wa mchezaji huyo na marehemu baadhi ya wachezaji wa Simba walidai Boban ndiye alikuwa rafiki mkubwa wa Mafisango na walikuwa kila mara wakiongozana pamoja katika starehe na hata wakiwa kambini.

"Boban ndio alikuwa mtu wa kwanza kusambaza habari za kifo cha Mafisango kwetu na hata aliposikia taarifa hizo alichofanya alikwenda moja kwa moja Muhimbili kwenye chumba cha maiti na kuomba kuonyeshwa mwili wa marehemu na baada ya hapo hakuzungumza lolote mpaka hapa mnavyomuona,"alisema Juma Jabu.

Mafisango alijiunga na Simba akitokea Azam Fc, mwaka jana alizaliwa Machi 7, mwaka 1987, nchini Rwanda na alikuwa akiichezea timu ya Taifa ya nchi hiyo kabla ya kusimamishwa kwa muda mrefu kutokana na utovu wa nidhamu na amerudishwa kundini na kocha Micho, lakini hata hivyo hajaweza kuitumikia timu hiyo ya Taifa lake.

Mchezaji huyo atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika timu ya Simba msimu huu uliomalizika hivi juzi na kung'aa zaidi katika Ligi hiyo kwa kupachika mabao na kutoa pasi za mwisho, ambapo Mechi ya mwisho ya Mafisango ilikuwa ni kati ya Simba dhidi ya Al Ahly Shandy Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penati 9-8, kufuatia sare ya jumla ya mabao 3-3.

Wakati mechi ya kwanza kati ya Simba na Wasudan hao iliyochezwa hapa nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Mafisango aliifungia timu yake bao moja kati ya matatu yaliyoiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo huo.

KIFO CHA KIUNGO MSHAMBULIAJI WA SIMBA,PATRICK MAFISANGO AACHA SIMANZI.

admin
,
Next PostNewer Posts Previous PostOlder Posts Home