BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AJALI YA GARI YAUA NDUGU SABA LINDI.

AJALI ILIYOTOKEA JANA KATIKA KIJIJI CHA MAVUJI WILAYANI KILWA IMESABABISHA VIFO VYA WATU WATANO WA FAMILIA MOJA AMBAO PIA WALIKUWA WANATOKA KUZIKA NDUGU ZAO WAWILI WALIOZIKWA JUZI MJINI LINDI BAADA YA MAREHEMU HAO PIA KUPATA AJALI.

Waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Bi Saida ambae ni mama Mzazi wa Marehemu, Shiraz Jack Magongo aliezikwa Juzi, Shirin Jack Magongo ambae ni Mama Mzazi wa Marehemu Samia (MRS Lupanda) pamoja na Marehemu Shiraz.


Marehemu wa awali walipata ajali ambayo ilitokea majuzi katika Kijiji Cha Chipite.

Marehemu Mwingine ni Ajira Shiraz Jack Magongo, Nargis Ambae Ni Dada yao wa Mama Mkubwa na Mdogo Ambae Kwa Walio Kuwa Lindi ndie Mmiliki wa Nyumba ya GIFT Guest na walio Dar Yupo Livingstone str Maarufu kwa Uuzaji wa Chumvi PAMOJA Na Meja Hussein Bhatia ambae ndie alikuwa Dereva wa Gari Hilo Ambae alifariki baadae.

Maiti ya Marehemu Bi Saida, Shirin na Nargis zinatarajia kuzikwa Dar huku maiti ya Marehemu Meja Hussein Bhatia na Ajira Shiraz ikiwatarajiwa nayo kuzikwa mkoani Lindi.


Katika Ajali Hiyo Dada Mkubwa wa marehemu Shiraz na Shirin,Yasmin Jack Magongo walikimbizwa katika hospitali jijini Dar es Salaam kwa Matibabu.


Mwingine ambae Salma Mohamed Zaid Mtoto wa Mama Malaika HOTEL, Ambae ni mama Mzazi wa Marehemu Ajira shiraz Aliyefariki katika ajali hiyo ametoka salama katika ajali hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha ajali hiyo ni kutanda kwa moshi barabarani na gari lililopelekea watu hao kufariki dunia kuligonga basi la SB lililokuwa limesimama kando ya barabara.


Moshi huo ulikuwa unatoka mashambani kwa ajili ya maandalizi ya mashamba ambapo gari lilikuwa na namba ya usajili Noah T594 DDH.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: