BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UPDATE YA AJALI YA HELIKOPTA YA CCM KUANGUKA NDANI YA HIFADHI YA SELOUS IKIWA NA MGOMBEA UBUNGE DEO FILIKUNJOMBE MKOANI MOROGORO.


Picha ya maktaba ikionekana helikopta ikiwa imeanguka chini hivi karibuni.


Oktoba 15 mwaka 2015 nchi ya Tanzania imetawaliwa na tukio la kutokea kwa ajali ya Helikopta taarifa zilizosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii ikihusisha kuanguka na kulipuka katika hifadhi ya wanyama ya Selous mbuga na Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kuthibitisha na mmoja wa abiria aliyekuwemo ndani ni Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).

Kwa upande wa CCM taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba naye alieleza kuwa wana taarifa ya wamesikia ‘Tumesikia habari za chopa kuanguka huko Selous. Mungu aepushe kusiwe na majeruhi na Chopa zote zinazotumiwa na CCM kwenye kampeni ziko salama".

Lakini Makamba alieleza tena kupitia ukurasa wake wa TWITTER kuwa  "tulifuatilia/kubaini/kuripoti kuwa Chopa tulizokodi kama Chama hakuna iliyoanguka‘ hiyo ndio ilikua twitter ya mwisho kuandika Mhe January Makamba kwa usiku usiku wa jana kuamkia leo Oktoba 16/ 2015.


Kwa upande wa mwanasiasa mwingine Zitto Zubery Kabwe yeye aliandika kuwa ‘Naomba utulivu.1) ajali ya helkopta imethibitishwa 2) kuwaka hakujathibitishwa 3) ndugu yangu Deo alikuwamo 4) hakuna uthibitisho wa madhara, naomba utulivu mpaka tupate taarifa rasmi zilizothibitishwa na mamlaka husika, naomba sana hilo ili kuepuka sintofahamu".

Bado tunaendelea kukusanya taarifa mbalimbali kutoka mamlaka husika husika ili kuweza kujua ukweli wa jambo hilo ambalo kwa sasa linasemekana limetokea upande wa mkoa wa Morogoro.

Tutaendelea kupeana taarifa kadiri tukakavyozipata.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: