BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BODABODA, BAJAL KUZUILIWA KUFANYA BIASHARA YA KUBEBA ABIRIA TA

BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra-CCC), limeitaka serikali kusitisha usafiri wa bodaboda na bajaji, hadi mtaala wa kuwafundisha madereva wa vyombo hivyo utakapotungwa na kuanza kufundishwa.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk. Oscar Kikoyo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, wakati wa mashindano ya vilabu vya wanafunzi wa Sumatra-CCC vilivyokuwa vikichuana kuonyesha umahiri wa sheria za barabarani.

Dk. Kikoyo alisema wakati serikali ikiruhusu bodaboda na bajaji kufanya biashara, ilikuwa haijajiandaa kuwa na mfumo wa kutoa huduma hiyo.

“Hapakuwa na mtaala wa kuwafundisha, kwa hiyo mtu akitaka kuendesha bodaboda anajifunzia mtaani mwenyewe siku moja au mbili, akijiona ameweza anaingia barabarani kubeba abiria.

"Kwa hali ilivyo hivi sasa ajali ni nyingi watu wanapoteza maisha tunaiomba serikali isimamishe kwanza utoaji wa huduma kwa vyombo hivi ili tufanye maandalizi ya kina kuhusu mfumo wa utoaji mafunzo kwao," alisema.

Alieleza kuwa hiyo ni changamoto kubwa ambayo imesababisha watanzania wengi kila siku kupoteza maisha kutokana na ajali zinazosababishwa na kundi hilo.

“Vifo hivi sio tu vinatokea kwa abiria wanaowapandisha kwenye vyombo hivi, pia na wenyewe wamekuwa wakipoteza maisha,” alisema.

Aliongeza kuwa wahusika wanaandaa mtaala huo ambao ukikamilika utatumika kufundishia kwenye nyuo pamoja na kutoa elimu mbalimbali kwao kama ilivyo kwa madereva wa vyombo vingine vya moto.

Pia alisema sababu nyingine inayowasukuma kuitaka serikali isitishe usafiri huo ni pale inapotokea dereva amefanya kosa bila kujali usalama wake, hukimbia na kusababisha ajali nyingine.

Kuhusu elimu kwa wanafunzi, Dk. Kikoyo alisema wamemua kuitoa kwa wanafunzi ili wawe madereva wazuri hapo baadaye.

Alisema tayari wameshaifikia mikoa tisa kupitia shule mbalimbali ambapo kote wanamabalozi wao ambao ni wanafunzi wanaofanya kazi ya kuelimishana.

Alitaja mikoa hiyo kuwa ni Mtwara, Tanga, Arusha, Mwanza, Kagera, Kigoma, Mbeya, Tabora na Dar es Salaam.

Mratibu wa bajaji na bodaboda Manispaa ya Ilala, Renatus Mpatili, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, alisema vyombo vinavyoongoza kusababisha ajali hivyo ili kukabiliana na tatizo hilo wilaya hiyo imejiwekea utaratibu wa kuwatambua ili kuwaelimisha.

“Kila kata tuliwataka wawe na kiongozi wao wa bodaboda lengo ni kuturahisishia kuwafikia ili tuwape elimu ya usalama barabarani, wengi wanajifunza uchochoroni tena siku moja na kuingia barabarani,” alisema.

Katibu wa Walimu Walezi wa Vilabu vya Sumatra CCC mkoa wa Dar es Salaam, George Mapunjo, aliishukuru baraza kwa kuanzisha mpango wa utoaji elimu ya haki na wajibu wa mtumiaji barabara. Alisema kutumia vilabu hivyo shuleni kutasaidia kuwaepusha vijana na ajali kwani wana uelewa wa sheria.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: