BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTOTO WA MBUNGE WA CCM ANUSURIKA KIFUNGO CHA MIAKA 20 JELA KWA KOSA LA KUKAMATWA NA NYAMAPORI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, imemhukumu mtoto wa Mbunge wa Mbarali, Haroon Mulla Pirmohamed (CCM) kulipa faini ya Sh138,390,000 au kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kukiri kosa na kutiwa hatiani kwa kumiliki nyara mbalimbali za Serikali.

Katika kesi hiyo, mtoto huyo Pirmohamed Haroon alikutwa akimiliki kilo 46 za nyama ya tandala, mbawala, swala pala, tohe, njiwa pori, kanga pori na pembe za tandala na tohe vyote vikiwa na thamani ya Sh138,390,000.

Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alimhukumu mshtakiwa huyo kulipa faini hiyo ambayo ni mara 10 ya thamani ya nyara alizokutwa nazo na iwapo atashindwa atumikie kifungo cha miaka 20. 


Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Haroon alikwepa adhabu ya kifungo kwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kupatiwa risiti ya malipo ya Serikali namba 8870022.MWANANCHI
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment