BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO SC YAJIGAMBA KUIBUKA NA USHINDI MBELE YA KMC FC LIGI DARAJA LA KWANZA UWANJA WA MABATI MLANDIZI

Mshambuliaji wa klabu ya Polisi Moro SC, Ramadhan Kapera "Pires" akifurahia mara baada ya kupachika bao katika moja za michezo za ligi daraja la kwanza Tanzania bara dhidi ya wapinzania wao uwanja wa jamhuri Morogoro.Picha Juma Mtanda.

Benchi la ufundi la klabu ya Polisi Moro Sc lipo katika mahesabu makali ya kuibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya KMC Fc ya Dar es Salaam katika ligi daraja la kwanza Tanzania bara 2016/2017 unaochezwa leo katika uwanja wa Mabati Mlandizi mkoani Pwani.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa na MTANDA BLOG leo, Kocha Msaidizi wa Polisi Moro SC, John Tamba alisema kuwa kwa upande wa benchi la ufundi la timu hiyo tayari wameelekeza akili, mbinu, maarifa na ufundi kwa wachezaji wao kuelekea katika mchezo wao dhidi ya KMC Fc na lengo likiwa kuibuka na ushindi ili kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Tamba alisema kuwa wachezaji wa Polisi Moro FC wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi dhidi ya wapinzani wetu na lengo la kudhamiria kupata ushindi ni kuendelea kuongiza kundi hilo.

Kutokana na michezo mitano iliyochezwa Polisi Moro ndio inayoongoza kwa pointi 12 ikifuatiwa na timu ya KMC FC yenye pointi 11 hivyo umchezo huo utakuwa na ushindini kutokana na kila timu ikitaka kupata ushindi ili kujiimarisha katika nafasi nzuri huku Polisi Moro SC ikitamba kuongeza spidi na kasi kwenye michezo hiyo.

“Wachezaji wa timu ya Polisi Moro tumewaandaa kisaikolojia katika michezo yetu yote ile ya nyumbani ama ugenini hivyo, leo hatuna wasiwasi na sio jambo la ajabu kwetu kuibuka na ushindi japo tutapata ushindi dhidi ya wapinzani wetu kwani nao watatamani washindi mchezo huu, tusubiri dakika 90.”alisema Tamba.

“Tuna michezo miwili ya kumaliza mzunguko wa kwanza kati ya KMC FC na mchezo dhidi ya Mbeya Warriors FC ya Mbeya na malengo yetu kukusanya pointi sita ili kumaliza mzunguko huo tukiwa pointi 18 na baada ya hapo tutaanza hesabu nyingine mzunguko wa pili”alisema Tamba.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: