BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JESHI LA POLISI HALINA MWAMKO KATIKA KUWALINDA WAANDISHI WA HABARI WAKATI WA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO



Mratibu wa Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengulumwa.
 
Dar es Salaam. Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umelitaka Jeshi la Polisi nchini kubadilisha mtazamo na kuwaona waandishi wa habari kama wadau muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Akizungumza leo (Jumatano), wakati wa warsha maalumu ya kujadili usalama wa waandishi wa habari, Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengulumwa amesema polisi hawana mwamko katika kuwalinda waandishi wa habari wanapotekeleza majukumu yao bali wao ndiyo wanaohatarisha usalama wao.

Amesema jeshi la polisi lina uwezo wa kulinda usalama wa waandishi wa habari lakini mwamko wao ni mdogo, hivyo wanahitaji kupata mafunzo maalumu ya kuwawezesha kubadili mtazamo wao juu ya tasnia ya habari.


"Tumeona katika nchi mbalimbali kwamba polisi hawawapendi waandishi wa habari. Hilo linatokana na mawazo hasi waliuonayo juu yao, tunahitaji kutoa elimu kwao ili watusaidie kuwalinda waandishi wanapotekeleza wajibu wao," amesema Olengulumwa.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: