BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHERIA NO 5, KIFUNGU NO 15 (1) NA (2) YASABABISHA AFUNGWE KIFUNGO CHA MAISHA JELA TABORA

 
MAHAKAMA ya Wilaya ya Urambo, imemhukumu kifungo cha maisha jela, Jumanne Maulid (35), mkazi wa kijiji cha Kaliua Magharibi, kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilogramu 30 zenye thamani ya Sh. milioni 36.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Hamis Momba, baada ya mshtakiwa huyo kukiri kosa lake alipopandishwa kizimbani na kusomewa shtaka lake.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Momba alisema kwa kuzingatia sheria namba 5 ya dawa za kulevya kifungu namba 15 (1) na (2) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015, adhabu kwa mshtakiwa ni kifungo cha maisha jela.

Awali kabla ya hukumu hiyo kutolewa, upande wa mashtaka ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi, Philibert Pimma, uliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa vile dawa za kulevya zimekuwa zikiathiri vijana wengi hivyo kuathili nguvu kazi ya taifa.

Alidai kuwa, Oktoba 28, mwaka huu, saa 4:00 asubuhi, mshtakiwa alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa akiwa na bangi hiyo bila ya kuwa na kibali cha kumruhusu kuimiliki.

Katika utetezi wake ili asipewe adhabu kali, Jumanne aliiambia mahakama hiyo kwamba amekubali kuhusika na bangi hiyo kwa vile tu ilikutwa katika nyumba yake baada ya mpangaji wake kukimbia asikamatwe na polisi.

Katika kesi nyingine, Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo, Berth Sivonke, alimhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, Magina Mhoja, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha.

Magina ilidaiwa alitenda kosa hilo Machi 28, mwaka huu katika kijiji cha Busungi, alipomvamia Masunga Magadula na kumjeruhi kwa mapanga kisha kumpora Sh. 590,000 pamoja na simu mbili za mkononi zenye thamani ya Sh. 90,000.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: