BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

ACT-WAZALENDO WAIBUA UCHAFU SOKO LA MAWENZI KAMPENI ZA UDIWANI MORO.


Juma Mtanda, Morogoro.
Chama cha ACT-Wazalendo kimeeleza kuwa wananchi kushindwa kutatuliwa kero muhimu kunatokana na baadhi ya viongozi serikalini kunatokana na Tanzania kutokuwa na utamaduni wa mfumu bora wa kuandaa viongozi wa kulitumia taifa ipasavyo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghira alisema kuwa Tanzania haina mfumo bora wa kuandaa viongozi wa kutumikia taifa katika nyanja mbalimbali na hali hiyo ndio inayochangia kuwa na kero lukuki kila kona.

Mghira alisema kuwa ameshangazwa kuona uchafu uliozagaa katika soko la Mawenzi bila kuzolewa baada ya kulitembelea soko hilo ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kupitia chama hicho, Rahim Elias katika mtaa wa Nkota.

“Ni jambo linaloshangaza kuona viongozi wanaohusika wakishindwa kujali afya za watu wanaotembelea soko la Mawenzi kwa taka kushindwa kuzolewa huku bidhaa kama nyanya, mihogo, magimbi na bidhaa nyingine zikipangwa chini tena kwenye hali hiyo usalama na uchafu tele na viongozi wanaona.”alisema Mghira.

Mghira alisema kuwa tatizo la Tanzania sio kuwa na rasilimali, fedha au mazingira, isipokuwa tatizo kubwa la Tanzania ni kupata viongozi wenye uzalendo wa kweli wa kulitumikia taifa kwa moyo mmoja.

“Sijui ni kwa sababu gani..? Tanzania hatujapata nafasi ya kutengeneza viongozi dhabiti wa kuwatumia wananchi na hii ni tangu tupate uhuru kutoka kwa wakoloni lakini serikali ianze sasa kutengeneza mazingira mazuri ya kuandaa viongozi madhubuti wa kulitumikia taifa ili kuondoa kero ndani ya jamii.”alisema Mghira.

Inakuwaje soko kama Mawenzi lenye kuingiza kipato kikubwa ndani ya halmashauri alafu wafanyabiashara na wateja wao wanazungukwa na uchafu na viongozi wapo ?... au ni kweli halmashauri haina fedha za kulisafisha uchafu…?.alihoji Mghira.

Mghira aliongeza kwa kusema kuwa soko ndio linaloingiza fedha nyingi ndani ya halmashauri hapa nchi ukiachana na vyanzo vingine vya mapato lakini hata utawala wake ni kitu rahisi lakini tu endapo kiongozi ataweza kuweka utaratibu nzuri wa kuwapangia wafanyabiashara zamu za kuzoa taka eneo lao na kuhifadhi katika chombo maalumu kabla ya gari kuzoa.

“Chagua sahihi kwa wakazi wa kata ya Kiwanja cha Ndege katika uchaguzi huu mdogo ni kumchagua mgombea wa ACT-Wazalendo, Rahim Elias ili awe diwani wa kata hii na kusukuma kero ndani ya halmashauri, kiamini chama cha ACT-Wazalendo kinaweza katika uongozi na kipo imara.alisema Mwenyekiti huyo Anna Mghira.

Kwa upande wa mgombea udiwani kata ya Kiwanja cha Ndege chama cha ATC-Wazalendo, Rahim Elias alisema kuwa ameingia katika kinyang’anyiro hicho ili kuomba ridhaa ya wananchi wamchague na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.

“Naomba kura ya ndio siku ya januari 22 mwezi huu ili niweze kupata kura nyingi na kuibuka mshindi ili miradi iliyoshindikana niisimamie nikishirikiana na mbunge wa sasa, Abdullaziz Abood ili tusimamie vyema miradi iliyodorora kwa kipindi kirefu bila kumalizika kwani CCM wameshindwa.”alisema Elias.

Elias alisema kuwa soko la Mawenzi limekuwa likiingiza fedha nyingi kutokana na ushuru wanaotozwa wafanyabiashara lakini cha kushangaza soko hilo limekuwa soko chafu na kipindi cha mvua limekuwa halitamaniki kununua bidhaa kero hiyo ataishughulikia vizuri na kuitatua.

“Kuna mambo endapo nitakuwa diwani nitafuatilia kwa ukaribu na jambo langu la kwanza ni kuhoji mapato na matumizi ya soko la Mawenzi lakini ujenzi wa zahanati ya kata yetu iliyodumaa kwa zaidi ya miaka sita ambapo kwa sasa imeishia kusimama nguzi pekee.”alisema Elias.

Uchaguzi mdogo wa kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro unafanyika baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, God Nkyondya kufariki dunia huku vyama vya Chadema, CCM, Cuf na ACT-Wazalendo vikisimamisha wagombea katika uchaguzi huo unaotarajia kufanyika januari 22 mwezi huu.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads