BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA SIMU FEKI, KIBAO KIMEGEUKIA KWENYE SIMU ZA WhatsApp NAKO KILIO TU.

Huduma ya WhatsApp haitumiki tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zinazotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.

Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema inataka kuangazia kustawisha "huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi."

WhatsApp, ilipangiwa kuacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu mwishoni mwa Desemba 2016.

Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka jana.

Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.

Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

"Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema. WhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja duniani.


Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
Android 2.1 na Android 2.2
Windows Phone 7
iPhone 3GS/iOS 6

Simu ambazo wateja wake hawataweza kutumia Whatsapp ifikapo Juni 30, 2017 ni:
BlackBerry OS and BlackBerry 10
Nokia S40
Nokia Symbian S60

Wanaotumia simu za aina hiyo wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.

Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia. Simu ya Blackberry

Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: