BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LOWASSA, MBOWE KUTUA MORO KAMPENI ZA KUMNADI MGOMBEA WA UDIWANI CHADEMA

Mbunge wa viti maalumu Chadema mkoa wa Morogoro, Devotha Minja akihutubia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea udiwani wa chama hicho, Salumu Milindi (Hayupo pichani) katika eneo la msikiti wa mungu mmoja na dini moja kata ya Kiwanja cha Ndege.

Juma Mtanda, Morogoro.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga mikakati mizito ya kumuita aliyekuwa mgombea urais kupitia Ukawa mwaka 2015, Edward Lowassa ili kuongeza nguvu katika kumpigia debe mgombea udiwani wa chama hicho katika kampeni za uchaguzi mdogo wa kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.


Akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika kampeni za udiwani, Mbunge wa viti maalumu Chadema mkoa wa Morogoro, Devotha Minja alisema kuwa wapo katika mikakati ya kuwaita, Lowassa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kuongeza nguvu kwenye mikutano ya kampeni ya mgombea wao, Salum Milinda.

Devotha alisema kuwa licha ya kuwaita Mbowe na Lowassa na mwanasiasa mwenye ushawishi kubwa nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru huku lengo kuu likiwa kuongeza nguvu za kuwashawishi wananchi ili kumchagua mgombea wao katika uchaguzi huo unaotarajia kufanyia januari 22 mwakani.

“Lengo la Chadema ni kuongeza nguvu katika kampeni hizi na tunafanya mipango ya kuwaleta Lowassa, Mbowe na mzee wetu Ngombale-Mwiru ili waweze kunadi sera za chama na mgombea wetu aweze kuibuka kidedea katika uchguzi huu mdogo.”alisema Devotha.

Aliongeza kwa kusema kuwa kata ya Kiwanja cha Ndege imekuwa masikini katika sekta mbalimbali zikiwemo za miundambinu ya barabara, afya na kudai kuwa hata uwepo wa kiwanda cha kusindika Tumbaku bado hakina tija kwa wakazi wa kata hiyo na Milinda nduye anayefaa kuingia kwenye baraza la madiwani halmashauri ya Manispaa ili asukume magurudumu hayo na wananchi wanufaike.

Devotha alisema kuwa CCM imeshindwa kupata mgombea mwenye sifa za kuiletea maendeleo kata ya Kiwanja cha Ndege hivyo chagua sahihi kwa kata hiyo ni mgombea wa Chadema, Salum Milindi na sio wagombea wengine.

“Ni jambo la kushangaza kuona baadhi walioshika nyasfa za ngazi ya umeya Manispaa ya Morogoro kufanya upendelea kwa kujali maendeleo kata wanazotoka ikiwemo kata ya Boma, Mazimbu, Mwembesongo ambapo miundombinu ya barabara ina kiwango cha lami na viongozi hao wametoka kata hizo.

Kwa upande wa mgombea wa udiwani kupitia chama hicho, Salum Milindi alisema kuwa anagombea nafasi ili kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoshindwa kutekelezwa na madiwani waliopita.

Milindi alisema alidai kuwa yeye atasimamia vyema miradi yote ukiwemo mradi wa zahanati ambao umedorora ujenzi wake kwa kipindi kirefu licha ya fedha kutolewa na serikali lakini zimekuwa zikiingia kwenye matumbo ya baadhi ya viongozi.

“Wananchi naomba mniamini na mnichague januari 22 mwakani ili niwe diwani wenu na nina ahidi kusimamia vyema miradi yote ya maendeleo ukiwemo mradi wa zahanati ya Kiwanja cha Ndege ambao umedorora kufuatia fedha za ujenzi kutafunwa na baadhi ya viongozi wa kata hii.”alisema Milindi.

Malindi alisema kuwa moja ya mikakati yake ni kusimamia kikamilifu fedha za serikali na nyingine katika kata hiyo endapo atachaguliwa na kuahidi kuwa kuanzia kipindi cha miaka nne zahanati iliyoshindikana kukamilika itakamilika.

“Miundombinu ya barabara katika kata hiyo hakuna hata moja yenye kiwango cha lami licha ya kuwa kata kongwe Manispaa ya Morogoro”.alisema Milindi.

Uchaguzi mdogo wa kata ya Kiwanja cha Ndege unafanyika baada ya diwani wa kata hiyo, God Nkyondya kufariki dunia na vyama vitatu vimesimamisha wagombea ikiwemo CCM, Chadema na Cuf.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment