BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMO WA DALADALA WATIKISA KWA ZAIDI YA SAA 5 MOROGORO

 
Mgomo wa daladala umetikisa Manispaa ya Morogoro leo kufuatia madereva na makondakta kusitisha kutoa huduma ya usafiri kwa zaidi ya saa 5 wakipinga kulipa jumla ya ushuru  wa sh3000 kwa siku unaotozwa katika stendi tatu tofauti na kuwa kero kwa watoa huduma hao katika sekta ya usafirishaji mjini hapa.

Kutokana na mgomo huo viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood aliweza kuongea na madereva na makondakta hao ili kuona namna bora ya kusitisha mgomo huo na kufanyika kwa mazungumzo yenye kuleta tija pande zote mbli.

Mgomo huo ulisitishwa majira ya saa 5 asubuhi kwa daladala kuanza kazi ya usafirishaji huku viongozi wakiendelea na mazungumzo ya kuweka mambo sawa.


Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment