BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MHARIRI WA GAZETI LA MWANANCHI APAMBANA NA MAJAMBAZI KWA DAKIKA 10


Mhariri wa Mafunzo wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Allan Lawa akiwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) baada ya kuvamiwa na majambazi nyumbani kwake Kimara usiku wa kuamkia Alhamisi. Picha na Said Khamis.

 
Mhariri wa Mafunzo wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Allan Lawa amesimulia jinsi alivyopambana na majambazi kwa dakika 10 kabla ya kumkatakata kwa mapanga baada ya kuvamia nyumbani kwake Segerea– Bonyokwa usiku wa kuamkia Alhamisi.

Lawa ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) akipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata, alisema siku hiyo alikuwa amerejea nyumbani kwake akitokea Iringa.

“Tulikuwa tumelala, wakaingia kwenye chumba cha watoto walipotoka huko wakaja chumbani kwangu tukaanza kupambana mpaka sebuleni,” alisema Lawa ambaye amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo kukatwa vidole.

Alisema kwa dakika hizo 10 watu hao walikuwa wakimuamuru awape Dola za Marekani ambazo waliamini anazo licha ya kuwaambia hana.

“Wao walikuwa wananilazimisha niwape Dola lakini niliwaambia sina, wakasema nikiendelea kupambana nao watamuua mjukuu wangu nikawaambia nitapambana mpaka mwisho. “Walinikatakata kwa mapanga mikononi kwa kuwa wakati wote nilikuwa nakinga yasinipate usoni. 


Mkono wa kushoto ndiyo ulioumia zaidi, niliutumia kujikinga ndiyo maana una majeraha mengi. Kidole kimoja cha mwisho walikikata kabisa na kidole cha kati mkono wa kulia kimekatika nusu, nilipoteza damu nyingi sana,” alisema Lawa ambaye alikuwa na Sh1.5 milioni ambazo wezi hao walizichukua.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment