BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUU WA WILAYA AOGOPA KUTUMBULIWA JIPU NA RAIS MAGUFULI


Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa ametoa mwezi mmoja kwa kila kaya isiyo na choo kutozwa faini ya Sh200,000 wilayani humo kwa malengo ya kuepuka mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kipindi cha mvua.

Madusa ametoa maagizo hayo akiwa katika ziara maalumu ya kuhimiza maendeleo na ujenzi wa vyoo kwenye Kata za Chokaa na Sangambi ambako alijionea kaya nyingi zikiwa hazina vyoo.

Akizungumza leo amesema hatakubali ugonjwa wa kipindupindu uwe chanzo cha yeye kutumbuliwa kwenye wadhifa wake na kwamba lazima kila kaya iwe na choo safi ili kuepuka kusambaa kwa uchafu wakati wa mvua. 


Kauli hiyo anaitoa huku kukiwa na agizo la Rais John Magufuli alilolitoa kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha maeneo yao yanakuwa salama bila kipindupindu kuepuka kutumbuliwa.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: