BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MOROGORO YAKUMBWA NA VIASHIRIA VYA UPUNGUFU WA CHAKULA KWA KIPINDI CHA JANUARI-MARCHI 2017.

HALMASHAURI za wilaya ya Morogoro, Gairo, Kilosa, Mvomero pamoja na Manispaa ya Morogoro zimeripotiwa kuwa na viashiria vya upungufu wa chakula kuanzia kipindi cha robo ya tatu ya Januari hadi Machi, 2017, imefahamika.

Pamoja na kuwepo kwa viashiria hivyo, kwa sasa hakuna halmashauri ya wilaya iliyoripoti uwepo wa njaa na tathimini ya kina ya hali ya chakula na lishe inaendelea kufanyika.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe, juzi alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya chakula katika Mkoa wa Morogoro kwa mwaka 2016/2017.

Hivyo aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na akiba ya chakula na kuanza kuuza chakula chote walichovuna na kukitumia kuchezea ngoma ama kupikia pombe.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa , msimu wa kilimo wa 2015/2016 , mkoa ulilenga kulima hekta 756,295 za mazao ya chakula ili kuvuna tani 2,762,316 na katika utekelezaji wa malengo hayo zililimwa hekta 563,826 na kuvuna tani 1,597,895 sawa na asilimia 58 ya lengo.

Dk Kebwe alisema msimu wa mwaka 2016/2017 mkoa ulilenga kulima hekta 736,723 ili kuvuna tani 2,895,823 za mazao ya chakula.

Alisema hali ya chakula katika mkoa huo kwa mwaka 2016/2017 ni ya wastani kutokana na uzalishaji wa tani 1,569,885 na mazao ya chakula na umevuna tani 955,255, mazao ya mizizi tani 570,115 na mazao ya mikunde tani 44, 514.

Mahitaji ya chakula ni tani 526,622 kwa makadirio ya watu 2,430,442 mwaka 2016/2017 hivyo, mkoa kuwa na ziada ya tani 993,263 za chakula.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: