BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAMUZIKI WA MAREKANI P, DIDDY NI TAJIRI KIFEDHA LAKINI NI MASKINI WA MAPENZI

 
Na Ndimi Luqman Maloto.
UNAWEZA kuwa tajiri upande mmoja na ukawa maskini katika mkono wa pili. Kila mmoja na utajiri wake, Mungu hamnyimi mtu vyote, vivyo hivyo hampi mtu kila kitu. Huwapa waja wake kwa kadirio.

Mtu anaweza kuwa maskini wa mali lakini Mungu akamjalia watoto wenye upendo na wakamuondoa kwenye dhiki. Kampa mtu umaskini wa mali na watoto lakini akamjalia hekima. Maskini anakuwa kisima cha kuchota hekima. Mungu na kudura zake!

Rapa Sean John Combs ‘P Diddy’ ni tajiri mkubwa. Ndiye rapa anayeongoza kwa utajiri kuliko wale ma-tuff wallet wote wa Hip Hop unaowajua. Akina Shawn Carter ‘Jay Z’, Andre Young ‘Dre’ na wengine, wote wanafunga tela. Diddy yupo juu yao.

KAMA HUMJUI P DIDDY
Kwa taarifa tu ni kwamba Diddy anatajwa kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 750 ambazo kwa madafu ya Kitanzania ni shilingi trilioni 1.6.

Rekodi zake zinaonesha kuwa kupitia kampuni zake za muziki, mavazi na kadhalika, hujilipa mshahara wa dola milioni 60, ambazo ni shilingi bilioni 132 za Kitanzania kwa mwaka.

Hesabu hiyo inaonesha kuwa mshahara wake kwa mwezi ni dola milioni 5, ambazo ukizileta kwenye madafu unapata shilingi bilioni 11.
 
Hamasika kidogo, mtu ambaye anajilipa mshahara wa shilingi bilioni 11 kwa mwezi, anakuwa ni tajiri kiasi gani?

Vurugu za P Diddy; Mtoto wake aliyemuasili, Quincy, alipofikisha umri wa miaka 16 ambao ndiyo unaruhusiwa kisheria kuendesha gari Marekani, alimfanyia party la kisupastaa kisha akamzawadia magari mawili. Hiyo ilikuwa mwaka 2007.

Mwaka 2009, mtoto wake wa kiume anayeitwa Justin alitimiza miaka 16. Kama kawaida alimfanyia party la kitajiri ambalo mastaa kibao walishiriki, kisha Diddy alimpa zawadi ya gari bei mbaya aina ya Maybach lenye thamani ya dola milioni 360,000, ambazo kwa Bongo ni takriban madafu milioni 800.

Diddy anamiliki majumba ya kifahari yenye kila aina ya starehe. Ni mtoa misaada kwa jamii, akitokeza kuahidi mchango huwa ahadi zake zinaanzia milioni ya dola ambazo ni mabilioni ya shilingi.

ONA SASA MAISHA HAYANYOOKI

Pamoja na utajiri wote ambao Diddy anao lakini upande wa mapenzi ni maskini asiye na bahati.

Miaka 47 lakini hana mke, yeye ni mtu wa kuhangaika na wanawake tangu akiwa kijana mdogo na hata sasa umri unakwenda bado anaumizwa tu mapenzi.

Mwaka jana Diddy alijikuta analazimishwa kibuti na mpenzi wake ambaye alikuwa amepanga kuzeeka naye, mwanamuziki aliye pia mwanamitindo Casandra Elizabeth Ventura ‘Cassie Ventura’.

Diddy alijitahidi mno kumbembeleza Cassie abaki kwenye maisha yake lakini mrembo huyo alisema hataki tena.

Nini kinamsumbua Diddy mpaka kusababisha wanawake wasitulie naye? Mtu na pesa zake, anajua kula bata tena bata zisizo na mawazo kwa sababu fedha si tatizo, ni black soft handsome ambaye kwa macho ya nje wadada lazima wanadata naye, ongezea umaarufu mkubwa alionao. Kwa nini watoto wa kike wanamgwaya?

Amini kuwa Mungu hakupi vyote. Ana watoto sita kutoka kwa mama tofauti, alishakuwa kwenye mapenzi na wanawake 21 ambao eti wote hawakuona kama kwa P Diddy kuna mapenzi ya kuendelea. Umaskini wa Diddy kwenye mapenzi unasababishwa na nini?

Hawa wote wamepita kwenye maisha ya Diddy; Kate Upton, Diana Bianchi, Cameron Diaz, Aubrey O’Day, Sienna Miller, Noemie Lenoir, Claudia Jordan, Naomi Campbell, Sky Nellor, Alicia Douvall, Emma Heming, Karrine Steffans na Jennifer Lopez ‘J Lo’.

Wengine ni Kim Porter, Sarah Chapman, Misa Hylton-Brim, Salli Richardson-Whitf, Shanina Shaik, Penelope Cruz, Yasmeen Ghauri na Cassie mwenyewe.

Je, kwa wanawake wote hao imeshindikana nini Diddy kupata mke wa kuendana naye ili wafunge pingu za maisha? Hiyo ndiyo dunia.

Katika watoto wake sita, Justin mama yake ni Misa. Quincy mama yake ni Kim ambaye pia walizaa watoto wengine watatu, Christian (alizaliwa mwaka 1998) na wasichana mapacha, D’Lila Star na Jessie James (walizaliwa Desemba 21, 2006).

Miezi mitano kabla ya D’Lila na Jessie hawajazaliwa, Diddy alipata mtoto wa kike Chance kutoka kwa Sarah Chapman. Alipoachana na J Lo, kwa maumivu aliingia studio na kuachia ngoma mbili, I Need a Girl Part I na II.

Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment