BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI WANAVYOWATIA HASARA WAKULIMA WA ZAO LA BHANGI MKOA WA ARUSHANa Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Pamoja na Jeshi la Polisi polisi kufanikiwa kuongeza takwimu za ukamataji wa madawa ya kulevya, mbinu za wahalifu zimezidi kufichuliwa baada ya jeshi hilo kufanikiwa kuharibu maelfu ya miche ya bhangi na kuteketekeza mkoani Arusha.


Ikishirikiana na vyombo vingine vya Usalama pamoja na Tume ya Kuratibu na Kudhibiti dawa za kulevya nchini, imefakiniwa kuthibiti kilimo cha madawa ya kulevya aina ya bhangi ambacho kinalimwa baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru mapema mwaka huu 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi mjini hapa, baada ya operesheni ya kutokomeza bhangi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alieleza kuwa jeshi hilo pamoja na vyombo vingine limeharibu mimea ya bhangi iliyopo mashambani baada ya kuoteshwa na kuteketeza.


Kamanda Mkumbo alisema kuwa katika operesheni hiyo jumla ya hekari 31 za mimea ya bhangi ziliharibiwa na gunia 58 na kilogramu 210 ziliteketezwa kwa moto katika maeneo ya kijiji cha Kismiri Juu kata ya Uwiro tarafa ya King’ori na katika kijiji cha Engalaon kata ya Mwandeti tarafa ya Muklati wilayani Arumeru.
“Siku ya kwanza Januari 10 mwaka huu, Operesheni yetu ilifika kijiji cha Kismiri Juu ambapo jumla ya magunia 31 ya bhangi na kilogramu 210 za mbegu zilipatikana huku hekari 19 za mimea hiyo ziliharibiwa”. alisema Kamanda huyo.

Aliiongeza kwa kuwa kuwa Januari 13 pia katika kikosi kazi cha operesheni hiyo iliendelea kijiji cha Engalaon na kufanikiwa kupata magunia 27 kisha kuharibu hekari 12 za mimea ya bhangi ambapo  jumla ya magunia 58 yalipatikana, mbegu kilogramu 210 na hekari 31 za mimea hiyo kuharibiwa,aliseza Mkumbo.

Kamanda Mkumbo alitoa onyo kali kwa viongozi wanaoishi au kufanyia kazi maeneo hayo, kuacha mara moja kuwaunga mkono wakulima wa bhangi.

“Viongozi watambue kuwa wao ni walinzi wa amani katika maeneo yao na washirikiane na Jeshi la Polisi katika kutokomeza kabisa kilimo hicho cha bhangi ambayo inaleta madhara makubwa kwa jamii hasa kundi la vijana”. alisema Mkumbo.

Kwa upande wa mkuu wa kitengo wa kuthibiti dawa za kulevya nchini, Mihayo Msikhela alisema kuwa Jeshi la Polisi nchini limejipanga hasa kwenye kuzuia kuliko kutibu ndio maana wameamua kuharibu mapema mimea ya zao hilo haramu kabla ya kukomaa na kusambaa.

Msukhela alisema kuwa kiwango cha uteketezaji wa dawa za kulevya hapa nchini kwa mwaka 2016 kiliongezeka ikilinganishwa na mwaka juzi 2015.
 

Afisa sheria mkuu toka Tume ya Kuratibu na Kuthibiti dawa za kulevya Bi. Christina Gervas alisema kuwa kadri bajeti itakaporuhusu watazidi kushirikiana na vyombo vya Usalama kufanya operesheni mara kwa mara katika maeneo ambayo bhangi inalimwa.

Bi Christina alieleza kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wakulima na viongozi wa maeneo hayo ili waweze kuachana na zao hilo haramu na kujikita kwenye mazao halali ya chakula na biashara ili kupata kipato kisicholeta madhara kwa binadamu.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment