BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS AKWAPUA FEDHA HAZINA YA SERIKALI NA KUKIMBIA NAZO

Aliyekuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anasemekana kuondoka madarakani na zaidi ya dola za kimarekani milioni 11 kutoka katika hazina ya serikali.

Hayo ni kwa mujibu wa Mshauri maalumu wa Rais wa Gambia Adama Barrow, Mia Ahmad Fatty ambaye aliongea na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar.

Fatty aliongeza kuwa wataalamu wa masuala ya fedha wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea.

Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.

Pamoja na hilo, kwa sasa Rais Barrow amekuwa akifanya kazi na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha na wengine kutoka Benki kuu ya nchi hiyo kupata kiasi halisi kilichopo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: