BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS AMTEUA MWANAYE KUWA MKUU WA KIKOSI MAALUMU CHA JESHI CHA KUMLINDA RAIS

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemteua mwanawe Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuwa mshauri mkuu wa rais kuhusu operesheni maalum.

Mke wa Museveni, Bi Janet Kataaha Museveni ni Waziri wa Elimu na Michezo, wadhifa ambao alikabidhiwa Juni mwaka jana.

Jenerali Kainerugaba amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi (SFC) chenye jukumu la kutekeleza operesheni maalum za kijeshi.

Kikosi hicho husimamia ulinzi wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali Uganda.

Luteni kanali Don Nabaasa amepandishwa cheo na kuwa kanali na akateuliwa kaimu kamanda wa SFC.

Rais Museveni pia amemteua mkuu mpya wa majeshi, Meja Jenerali David Muhoozi ambaye amepandishwa cheo na kuwa jenerali.

Mkuu wa majeshi wa awali, Jenerali Edward Katumba Wamala amehamishwa na kuteuliwa waziri wa ujenzi.

Kwenye mabadiliko hayo yaliyotangazwa na msemaji wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF) Luteni Kanali, Rais Museveni amempandisha afisa mkuu wa majeshi aliyeongoza operesheni ya kushambulia ikulu ya mfalme wa Rwenzururu, magharibi mwa nchi hiyo.

Watu 100 walifariki wakati wa operesheni hiyo. Mfalme wa Rwenzururu Charles Wesley Mumbere alikamatwa na bado anazuiliwa Meja Jenerali Peter Elwelu aliongoza wanajeshi walioshambulia kasri la mfalme wa Rwenzururu

Brigidia Peter Elwelu, aliyekuwa mkuu wa kikosi cha wanajeshi hao wenye kambi yao kuu Mbarara, amepandishwa cheo na kuwa meja jenerali na akateuliwa kamanda wa majeshi ya nchi kavu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: