BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AYAHESABIA SIKU MAGAZETI MAWILI YANAYOIKOSOA SERIKALI


Rais John Magufuli amesema vyombo vya habari vinavyopotosha ukweli na kuleta uchochezi siku zake zinahesabiwa kwani Serikali yake anayoiongoza haiwezi kukubali kuvurugwa kwa amani ya nchi.


Amesema mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 chanzo chake ni vyombo vya habari, hivyo hawezi kukubali hali hiyo itokee nchini.


Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha Jambo Food Plant mjini Shinyanga na matangazo yake kurushwa mubashara na Star Tv, Rais Magufuli amesema magazeti yote isipokuwa mawili, vituo vyote vya televisheni na redio nchini vinafanya kazi nzuri ya kuelimisha wananchi.


Rais Magufuli amesema Serikali yake haikatai kukosolewa na kwamba, magazeti mengine yanakosoa na kusaidia kutatua matatizo ya jamii, lakini hayo mawili (bila kuyataja) yamekuwa ni kupindisha kila kitu.


“Hayo magazeti kila ukisema hivi yanapindisha, siyataji kwa sababu yanajifahamu lakini yajue kwamba siku zake zinahesabika. Serikali ninayoiongoza haiwezi kukubali amani kuvurugwa,” amesema.Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment