BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS WA URUSI PUTN ALIJITOLEA KUMSAIDIA DONALD TRUMP KUSHINDA UCHAGUZI WA MAREKANI DHIDI HILARY CLINTON


Donald Trump alikutana na wakuu wa ujasusi siku ya Ijumaa

 Maafisa wa ujasusi wa Marekani wamemlaumu Rais Putni wa Urusi kwa kuamuru binafsi shughuli za udukuzi nchini Marekani kwa juhudi za kupendelea au kumsaidia Donald Trump ashinde katika Uchaguzi wa Urais uliofanywa mwaka uliopita.

Ripoti iliyotolewa na maafisa hao ilisema kuwa Urusi ilikusudia kuchochea ili wananchi Wamarekani wakose imani katika katika demokrasia ya nchi yao na pia kumdhalalisha mpinzani wa Trump, Bi Hillary Clinton.

Ripoti hiyo kwa mara ya kwanza inamshirikisha Putni katika shughuli za udukuzi moja kwa moja katika uchaguzi wa Marekani.

Makamu wa Rais Mteule, Mike Pence, alisema baadaye kuwa Donald Trump baadaye atachukua hatua kali dhidi ya udukuzi wo wote unaokabili Marekani kutoka kwa taifa lo lote lile.

Baada ya kukutana na maafisa wa ujasusu, Trump alisema kuwa amejifunza mengi kuhusiana na shughuli za udukuzi lakini akakanusha kuwa udukuzi huo ulibadili mkondo wa matokeo ya uchaguzi wa Urais kwa njia ye yote.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment