BannerFans.com

WABUNGE SUZAN KIWANGA, PETER LIJUALIKALI NA WENZAO 37 WAREJEA URAIANI BAADA YA KUKAA RUMANDE

Millionaire  Ads

RUBANI MLEVI ASHINDWA KURUSHA NDEGE BAADA YA KUANGUKA NA KUZIRAI


Polisi huko Canada wamemkamata rubani mmoja aliyepatikana ,ndani ya ndege ya abiria kwenye chumba cha marubani akiwa amelewa chakari kwa mujibu wa vipimo alivyofanyiwa.

Rubani huyo alikuwa amepangiwa kuendesha ndege hiyo kwa safari ya kutoka uwanja wa ndege wa Calgary Canada hadi nchini Mexico ndipo lakini wafanyakazi wenzake wakamuona hakuwa katika hali sawa na kupiga ripoti.

Kisha punde baadae akaanguka na kuzirai.

Sasa amezindukia mashtaka ya kutaka kuendesha ndege akiwa mlevi na utovu wa nidhamu kazini.

Baadae rubani mwengine aliendesha ndege hiyo ya shirika liitwalo Sunwing iliyokuwa inaelekea Cancun mjini Mexico, ikiwa na abiria zaidi ya 100.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads