BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA RAIS DK JOHN MAGUFULI YASHTAKIWA

Rais John Magufuli alitia saini sheria hiyo tarehe 16 Novemba, 2016

Baraza la Habari nchini Tanzania limewasilisha kesi mahakamani kupinga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo Novemba mwaka jana.

Baraza hilo limewasilisha kesi hiyo katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) likishirikiana na mashirika mawili ya kutetea haki za kibinadamu; Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.

Baraza hilo linakana baadhi ya vifungu vya sheria, ambavyo wanasema vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza vifutwe.

Wanasema vinakiuka matakwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zinataka nchi wanachama kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba wa kuundwa kwa jumuiya hiyo.

"Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unahimiza umuhimu wa kufuata kanuni za utawala bora, utawala wa kidemokrasia, utawala wa sheria, uwajibikaji, uwazi, haki kwa wote, usawa wa kijinsia na kuheshimu haki za binadamu," baraza hilo linasema kupitia taarifa iliyotiwa saini na Katibu Mtendaji, Kajudi Mukajanga.

"Tanzania inatakiwa kuchukua hatua za kuhakikisha haki zote zilizotajwa katika mkataba huo zinafuatwa na kutekelezwa."
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: