BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TUMBILI AONEKANA AKIFANYA MAPENZI NA JAMII YA SWALA


Tumbili mmoja kutoka Japan amerekodiwa katika kanda ya video akijaribu kufanya mapenzi na paa.

Watafiti walimuona mnyama huyo akijaribu kufanya mapenzi na paa wawili (wanaofanana na swala) mnamo mwezi Novemba 2015 wakati wa msimu wa uzalishaji wa tumbili.

Tumbili hao wamekuwa wakionekana wakijaribu kuwapandia paa hao katika mchezo.

Tabia hiyo imeorodhshwa katika utafiti uliochapishwa katika jarida kuhusu nyani.

Tumbili huyo wa kiume asiye na hamu ya kufanya mapenzi na tumbili wenzake na amekuwa akiwafukuza tumbili wengine waume ambao wamekuwa wakimkaribia.

Mwanzilishi mwenza wa utafiti huo Alexandre Bonnefoy alisema: Tumbili huyo alimpanda paa huyo na kuonyesha tabia za kujamiana zilizoshirikisha tabia 15 tofauti za kufanya tendo la ngono katika kipindi cha sekunde 10 kabla ya kufanya mapenzi.

Sio mfano wa kwanza kwa wanyama tofauti kutekeleza tendo hilo.

Mwaka 2014, ripoti ya Seal kujamiana na Penguin iligonga vichwa vya habari.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment