BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UGONJWA WA HOMA YA INI NI ZAIDI YA UGONJWA WA UKIMWI


Ugonjwa wa homa ya ini maarufu kwa jina la hepatitis B umetajwa kuwa maambukizi yake ni makubwa na haraka zaidi ya Ukimwi.

Takwimu za Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) zinaonyesha kuwa kiwango cha maambukizi ya homa ya ini B kwa Tanzania ni wastani wa watu wanane katika kila watu 100. Maambukizi ya VVU, ni wastani wa watu watano katika kila watu 100.

Takwimu za wachangiaji damu katika kitengo cha uchunguzi wa magonjwa cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, (MNH) kwa kipindi cha siku 14 za Desemba 2016, zinaonyesha kuwa kati ya sampuli 480 za damu zilizopimwa, 18 zilikutwa na VVU.

Lakini, katika sampuli 480 zilizopimwa katika kipindi hicho hicho, 56 zilikutwa na virusi vya homa ya ini B, huku watu 20 kati yao wakiwa na ini C (hepatitis C). 


Katibu Mkuu wa Serikali, Dk Mpoki Ulisubisya amesema Serikali imeanza kuwatumia watafiti wake kuangalia kwa undani kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment