BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

WALIMU WASITISHA MGOMO KWA KUPEWA CHAI YA SH 1,000/-

MGOMO wa walimu wanaoendelea na mafunzo katika Chuo cha Ualimu cha Kleruu mjini hapa, umemalizika.

Mratibu wa mafunzo ya walimu hao, Laudensi Mnambi, alisema kuwa baada ya walimu hao kugoma juzi kuingia darasani kuendelea na mafunzo hayo, wamekubali kuendelea na mafunzo kama kawaida.

Mnambi alisema tatizo lililojitokeza, lilikuwa ni la kueleweshana tu.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Mnambi alisema:

"Tangu siku ile, mambo yalikwisha, tuliyaweka sawa, walimu wapo darasani wanaendelea na mafunzo kama kawaida,” alisema Mnambi.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads