BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HATA TIMU YA WAAMUZI FC NAYO INABEBWA NA WAAMUZI NA KUTWAA KOMBE LA PASAKA MORO

Baadhi wa mashabiki wa soka wakiwazuia mashabiki wa timu ya Sultan Rangers waliokuwa wanakwenda eneo la vurugu kwa lengo la kumshambulia mshika kibendera Rajab Ally baada ya pambano kati ya timu hiyo na Waamuzi la mchezo wa nusu fainali ya Pasaka Cup kuvunjika dakika 75 kwa madai ya kupindisha sheria 17 za soka katika mchezo huo uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.

Juma Mtanda, Morogoro.
Timu ya soka ya Waamuzi Manispaa ya Morogoro Frat FC imetwaa ubingwa wa kombe la Pasaka Cup 2017 kwa kuilaza Moro Kids kwa bao 1-0 huku mashabiki wakiibuka na manung’uniko kibao baada ya kumalizika kwa mchezo mkali wa fainali uliopigwa katika dimba la uwanja wa Sabasaba mkoani hapa.


Kumalizika kwa mchezo huo, mabingwa hao walikabidhiwa seti moja ya jezi na mgeni rasmi Mwenyekiti wa chama cha soka Manispaa ya Morogoro (MMFA), Emmanuel Kimbawala kufuatia bao la ushindi lililofungwa kwa njia ya penalti na, Abraham Nahoda.

Wakizungumzia juu ya mashindano hayo na MTANDA BLOG mjini hapa walisema kuwa timu ya Waamuzi FC hawakustahili kutwaa ubingwa bali waamuzi waliochezesha michezo yao ndio waliosaidiwa kutwaa kombe hilo la Pasaka Cup 2017.

Mmoja wa shabiki wa soka, Moses Chawala alieleza kuwa kiujumla mashindano hayo yalikuwa mazuri hasa kwa michezo iliyokuwa haihusishi na timu ya Waamuzi lakini michezo ilikuwa inahusisha timu ya Waamuzi FC dhidi ya wapinzani wake ilikuwa inapungua msisimuko wa burudani ya soka kutokana na waamuzi wa mchezo husika kuonyesha mapenzi ya wazi na upendeleo kwa timu ya Waamuzi FC na pinzani kuminywa.

Chawala alieleza kuwa michezo iliyohusisha timu ya Waamuzi FC na wapinzani iliisha kwa kunung’uniko kutokana na waamuzi wa mchezo kuonyesha mahaba na kupelekea kushinda katika mazingira yoyote na kujikuta wakiambulia kutupiwa lawama kutoka kwa timu pinzani wao na mashabiki.

“Mchezo wa nusu fainali mshika kibendera namba moja alijeruhiwa juu ya jicho la kushoto kwa kupigwa baada ya kuzuka vurugu wakati wa mchezo baina yao na Sultan Rangers FC kutokana na madai ya kupindisha sheria 17 ambapo Waamuzi FC walipata bao 1-0 na mchezo huo kuvunjika dakika ya 75 sasa hii ni hata kwa maendeleo ya soka .”alisema Chawala.

Aliongeza kwa kusema kuwa mashabiki wanapenda kuona timu inashinda kwa uwezo wake kutokana na ubora wa wachezaji wake lakini timu hii ya Waamuzi FC sijaona mwamuzi akiichezea timu yake zaidi ya kuona wachezaji mamluki wakichezea timu hiyo katika hatua ya awali hadi fainali iliyokuwa imejaa wacheza wa Mawenzi Market FC iliyopanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Katibu wa klabu ya soka ya Black Viba FC, Asante Charles alieleza kuwa michezo yote iliyohusisha na timu pinzani ilikumbwa na malalamiko na kudai kuwa haikushangaza mwamuzi wa pembeni, Rajab Ally kujeruhiwa katika mchezo wa nusu fainali na wachezaji pamoja na mashabiki.

Charles alieleza kuwa alistushwa kuiona timu ya Waamuzi FC imeingia kwenye mashindano hayo na na kukumbwa na wasiwasi endapo waamuzi wanaochezesha michezo yao wataweza kufuata sheria 17 za soka bila kupindisha na kutoa upendeleo ?alihoji.

“Waamuzi waliochezesha michezo ya timu ya Waamuzi FC hawakuweza kuchezesha kwa kufuata sheria 17 na badala yake wamekuwa wakitoa upendeleo kwa timu Waamuzi FC na kuwaminya wapinzani wao na ndiyo wamefika hatua hii na kutwaa ubingwa wa Pasaka Cup 2017 na zawadi ya jezi.”alisema Charles.

Mwenyekiti wa chama cha Waamuzi Manispaa ya Morogoro (Frat), Mainda Joseph alieleza kuwa waamuzi wamechezeshaa mashindano hayo kwa kufuata sheria zote 17 bila ya kuwa na upendeleo kwa timu ya Waamuzi Manispaa ya Morogoro Frat FC.

Joseph alieleza kuwa wengi wa mashabiki hawaelewi sheria za soka na kuwataka kuhudhuria kozi za waamuzi ili kuufahamu mchezo huo wenye wapenzi wengi duniani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: