BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAOKWAMISHA VITA YA MADAWA YA KULEVYA TANZANIA NDIO HAWA


Maendeleo katika nchi yoyote hayawezi kuja bila jitihada za kuyafikia, Ikiwa kiongozi yoyote anayepigania maendeleo ya watu wote atagusa maslahi ya wachache wenye nia mbaya basi kiongozi huyo uchafuliwa na pengine anaweza kufanyiwa njama za kupoteza maisha yake. 


VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA. 

Siku zote na duniani kote, vita hii huwa ni ngumu sana ikizingatiwa kuwa mara nyingi biashara hii mbovu hufanywa na wakubwa ,ambao siku zote ujali maslahi binafsi kuliko utu na muda wowote huwa tayari kwa kutimiza maslahi yao ikiwa na maana kuwa wako radhi kwa lolote lile mpaka matakwa yao yatimie anaandika Sharifu Mtanda.

VYOMBO VYA HABARI. 

Ukweli ni kuwa kama kuna kitu kinanachoweza kumfanya mtu au kitu kisifike au kichafuke, basi ni vyombo vya habari na kama kuna watu waongo au wakweli duniani basi ni waandishi na watangazaji wa habari. 

Kwa mfano vyombo vya habari vimewafanya viongozi wengi wenye sifa na wasio na sifa kuwa maarufu sana na kwa upande mwingine vimewachafua watu kutokana na maslahi ya wachache hivo basi niwataadhari juu ya vyombo vya habari (ikiwa amani itatoweka sehemu yoyote duniani, basi waulizwe kwanza wanahabari). 

WITO KWA WATANZANIA.
Watanzania wanapaswa kuwa makini sana na vyombo vya habari na madawa ya kulevya hayakubaliki kwani uua nguvu kazi ya taifa na kudumaza maendeleo.. 

Unapokuwa kiongozi lazima utumie hekima, maarifa, busara na mbinu (Any successful business needs the strong strategies, procedures and leadership). 

WATANZANIA, lazima tuunge mkono jitihada za kupambana na madawa ya kulevya na tukitambua kuwa hili ni jukumu la kila mtu kuanzia katika nafasi zetu na taifa kwa ujumla. Tutambue walanguzi wa madawa ya kulevya wanazo mbinu nyingi ambazo kwanza lazima tuzikwepe. 

Lazima tuwaunge mikono na miguu viongozi wetu katika jitihada za kuleta maendeleo katika taifa letu. Tutambueni kuwa viongozi ni binadamu wala sio malaika hiyvo wakikosea tuwakosoe au wakosoleke katika njia sahihi kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment