BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BIA MPYA ZA PISNER ZATENGENEZWA KWA KUTUMIA MKOJO WA BINADAMU


Kiwanda kimoja cha pombe nchini Denmark kimetengeneza bia mpya kwa kutumia shayiri ambayo imekuzwa kwa kutumia lita 50,000 za mkojo.

Kampuni ya Norrebro Bryghus inayomiliki kiwanda hicho hata hivyo imesema bia hiyo haitakuwa na masalio yoyote ya mkojo wa binadamu.

Pombe hiyo imepewa jina Pisner na imeandaliwa kwa kutumia kimea cha pombe kutoka wka shayiri iliyokuzwa kwa kutumia mkojo huo badala ya mbolea ya kawaida.

Mkojo huo ulikusanywa kutoka tamasha ya Roskilde ambayo ndiyo hafla kubwa zaidi ya muziki Ulaya kaskazini miaka miwili iliyopita

"Wakati habari kuwa tulikuwa tumeanza kutengeneza pombe zilifichuka, watu walidhani kuwa tulikuwa tukiweka mkojo huo moja kwa moja kuenda kwa pombe," alisema mkurugenzi wa kampuni ya Norrebro Bryghus.


Mkojo ukikusanywa kutoka kwa wanaume.

"Kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi," alisema mtu moja ambaye alihudhuria tamasha hiyo ya muziki mwaka 2015.,

Lita hizo 50,000 za mkojo zilizokusanywa kutoka kwa warsha hiyo ya muziki zilitosha kuunda chupa 60,000 za bia.

Kutumia kinyesi au mkojo wa binadamu kwa kiwango kikubwa hivyo ni jambo ambalo si la kawaida, baraza la kilimo na chakula nchini Denmark linasema.

Baraza hilo ndilo lililotoa wazo hilo la kutumiwa kwa mkojo kama mbolea ya kurutubisha shayiri ambayo baadaye inatumiwa kutengeneza pombe.Mashine iliyotumika ilitengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji,

Lakini usishangae, tayari kuna mtambo wenye uwezo wa kubadilisha mkojo moja kwa moja na kuwa bia.

Mashine iliyotengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji, inabadili mkojo wa binadamu na kuwa maji ya kunywa pamoja na mbolea ikitumia nguvu za miali ya jua.

Maji hayo, kutoka kwa mkojo uliokusanywa kwa siku kumi katika tamasha moja la muziki Ghent kisha yalitumiwa kutengeneza bia.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: