BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FREEMAN MBOWE ASHINDWA KUMZUIA LUCY OWENYA ASICHANGIE LOLOTE BUNGENI BAADA YA KUPATA TAARIFA ZA KIFO CHA NDESAMBURO

Dodoma. Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe amesema alipopata taarifa ya kifo cha Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alijaribu kumzuia mtoto wa marehemu, Lucy Owenya asichangie bungeni lakini alishindwa.

Mbowe ameyasema hayo leo Jumatano wakati akilitangazia bunge kuhusu kifo cha Mwenyekiti huyo wa Chadema, mkoa wa Kilimanjaro.

Owenya ni mbunge wa viti maalum wa chama hicho na mtoto wa kada huyo mkongwe wa Chadema. "Ilipofika zamu yake kuchangia nilimruka hata akalalamika inakuwaje wakati alitakiwa atoe maoni yake. 


Tushirikiane na familia ya marehemu ambaye alihudumu kwenye bunge hili kukamilisha taratibu zilizobaki," amesema Chenge./Mwananchi.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment