BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HUU NDIO UPENDO ULIOJIFICHA KWA MTOTO DHIDI YA WATU WA KARIBU YAKE

 
MARA nyingi watoto hugawanya wazazi kihisia kulingana na jinsi anavyompa uzito na upendo mzazi mmoja na kumwacha mwingine.

Upendo wa mtoto kwa mzazi fulani mara nyingi humuumiza mzazi mwingine kihisia, mara nyingi watoto huwa wanakuwa wazi kujipambanua kihisia, hivyo muhusika anajua hata kama asipoongea mbele za watu.

Tatizo hili halipo tu kwa watoto bali hata wazazi wapo ambao wanaoonyesha upendo moja kwa moja kwa mtoto fulani kati ya watoto alionao kwa sababu ya kushindwa kuficha hisia zake.

Wapo ambao wanaweza kuwalea watoto wao kwa kuwaonyesha upendo sawa na kumpenda mtoto fulani bila kuweka wazi kwa wengine.

Katika familia mara nyingi watoto hugawanyika kwa wazazi katika upendo, wapo ambao wanakuwa wanampenda baba na wengine watampenda mama hilo ni suala la kawaida.

Upendo wa mtoto kwa mzazi husababishwa na ukaribu baina ya mtoto na mzazi katika masuala mbalimbali.

Baadhi ya watoto wanampenda mzazi fulani upendo wa kawaida kwa sababu ni mzazi wake na anamuona kila siku, mwingine anampenda kwa sababu anamjali.

Upendo wa mtoto hujengwa na hisia jinsi unavyomchukulia na kutilia uzito baadhi ya mambo yanayomhusu ndivyo na yeye atakavyoweza kuonyesha mapenzi.

Zipo changamoto zinawakuta baadhi ya wazazi wanaofanya kazi kwa sababu kutumia muda mrefu ofisini na kukosa muda wa kukaa karibu na watoto.

Wapo wazazi ambao wanafanya kazi lakini wanapendwa na watoto kwa sababu wanaishi kwa kuwajali, utakuta mtoto katika familia kila kitu anamwambia baba au mama tu. Hii inatokana na mtu husika jinsi anavyomjali na kumchukulia.

Katika malezi ya watoto wapo wazazi ambao wanakosea na kudhani kuwa kuwatolea watoto ukali, kuwasema vibaya ni sehemu ya kutafuta heshima yake kama mzazi bila kujua kama anapaoteza upendo wake kwake.

Wazazi lazima tujifunze kupenda watoto, ni ngumu sana kama utakuwa unamchukia yeye kurudisha upendo, lazima atakutengeneza kama sehemu ya adui hata bila kukwambia.

Pia kuna haja ya kuwaheshimu watoto, kuwasilikiza na kuheshimu hisia zao, endapo utaishi na mtoto kwa utaratibu huo hakuna atakayekuchukia wala kukuona mbaya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: