BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

IBADA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI AJALI YA BASI KUAGWA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABED ARUSHA LEO
WAKATI Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akitoa taarifa kwa umma kuwa ibada ya kuaga miili ya wanafunzi waliofariki kwenye ajali iliyotokea huko wilayani Karatu itafanyika kesho saa 4 asubuhi katika uwanja wa Sheikh Amri Abed, Serikali imegharamia Sanda pamoja na majeneza.

Kwa upande wa Meya wa Jiji la Arusha , Calist Lazaro amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

Aidha, Lazaro amesema kuwa viongozi mbali mbali wakiwemo mawaziri pamoja na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vicent kwa ajili ya kikao na baadae majira ya saa tisa au kumi taarifa rasmi ya serikali itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment