BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JAMBAZI SUGU WA KIKE APIGWA RISASI NA POLISI KISHA KUFARIKI DUNIA

Mwanamke anayedaiwa kuwa jambazi sugu, ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi jijini Nairobi.

Kijana huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alfajiri na mapema Jumatano katika mtaa wa Kayole.

Gazeti la kibinafsi la Daily Nation linasema mwanamke huyo alikuwa na majambazi wengine wanne wa kiume pale walipofumaniwa na polisi wakitekeleza wizi katika eneo la Lower Chokaa, mtaa wa Kayole.

Anadaiwa kufyatulia risasi maafisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini wawili hao wakauawa na wenzao walifanikiwa kutoroka eneo la tukio.

Taarifa katika gazeti la Daily Nation inasema polisi waliwaandama baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wenzao kupitia WhatsApp kwamba majambazi hao walikuwa wamekwepa mtego waliokuwa wamewekewa.

Polisi walijiandaa na kisha wakawakabili katika mtaa wa Lower Chokaa.

Mkuu wa polisi wa mtaa wa Kayole Joseph Gichangi amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema: "Kwa mujibu wa wadokezi wetu, mwanamke huyo alikuwa mke wa mshukiwa wa ujambazi ambaye anafahamika vyema, ambaye bado anasakwa na polisi."

Alisema visa vya wanawake kujihusisha na magenge yanayotekeleza wizi wa kutumia mabavu vinaongezeka.

Wakenya mtandaoni wamekuwa wakisambaza picha za Mwaniki na kumjadili sana mtandaoni.

Katika Facebook, mwanamke huyo anajitambulisha kama mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu cha Nairobi na mtu anayependa kufurahia maisha.

Kuna wakati alipakia picha yake, ya mwanamume na mtoto, na kuongeza kwamba hiyo ni "familia".

Mkuu wa polisi Nairobi Japheth Koome anasema magenge mengi ya wahalifu huwa na wanawake.

"Wanawake hutumiwa kusafirisha silaha, kukusanya habari na hata kushiriki katika ujambazi," Bw Koome alisema.

Aliongeza kuwa wakati mwingine hutumiwa na majambazi wa kiume kuwapelekea chakula mafichoni.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: