BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMPUNI YA MAGARI YA FORD KUWATIMUA WAFANYAKAZI 1,400


KAMPUNI kubwa duniani ya kutengeneza magari aina ya Ford yenye makao makuu nchini Marekani, imetangaza azma ya kupunguza wafanyakazi 1,400 kutoka katika orodha ya watumishi 200,000 iliyowaajiri.

Hao ni walioajiriwa huko Marekani na Bara Asia, sababu kuu ni kwamba mauzo ya magari hayo yamekuwa yakishuka kwa kasi. Haikufafanua kwa kina.

Mtendaji Mkuu wa Ford, Mark Fields, anasema kwamba kampuni inaelekeza nguvu za kujihami kibiashara katika upunguzaji gharama, ajira ikiwa sehemu mojawapo.
Kampuni ambayo imekuwa ikishikilia asilimia saba ya soko la magari duniani katika miaka ya karibuni, hivi karibuni ilipanua ajira maradufu kutokana na kupanuka soko lake kwa kasi ya.

Inaelezwa, mauzo ya Ford katika makao makuu yake Marekani yamepungua kwa asilimia saba na Ulaya imefika asilimia 11. Hiyo ni hadi mwezi uliopita, huku ikidai gharama za uendeshaji zinaongezeka.

Janga hilo, pia imezifikia hisa zake kuanguka thamani kwa kiwango cha asilimia 15, ndani au kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Hata hivyo, maamuzi hayo mazito ya sasa, yanaelezwa hayatazikumba Bara la Ulaya na Amerika Kusini.

Msemaji wa Mtendaji Mkuu, anafafanua kuwa undani wa dokezo hilo linalohusiana na upunguzaji kazi, litaanikwa kwa kina mwezi ujao na mchakato utakamilika, Septemba ijayo.

Kati ya wafanyakazi 200,000, iliyowaajiri duniani kote, wale watakaoathirika ni 101,000 kutoka makao makuu nchini Marekani na wenzao 23,000 walioko katika matawi ya Bara Asia.

Hiyo ina maana watumishi walio salama ni 76, 000 waliko katika maeneo mengine ya dunia ikiwamo Ulaya na Marekani Kusini.

Mwaka 2013, kampuni hiyo ilipunguza jumla ya wafanyakazi 3,000 katika tawi lake lililoko nchini Afrika Kusini.

Pia mwaka jana, ilipunguza mamia ya ajira huko Ulaya na Asia, ikiwa sehemu ya kufikia lengo la kuokoa Dola za Marekani milioni 200 (Sh. bilioni 440). 


Hata katika siasa, kupitia kampeni za uchaguzi kuwania urais nchini Marekani, Rais Donal Donald Trump, alishauri kuachana na mkakati wa kuwa na tawi nchini Mexico, ili kulinda ajira ya Wamarekani na kampuni hiyo iliridhia, jambo lililozua mjadala mkubwa kuhusu kuwapo utashi wa kisiasa.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: