BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KWAHERI YA KUONANA RC SAID THABITH MWAMBUNGU, UMETUTOKA


Mkuu wa mkoa mstaafu wa Ruvuma, Saidi Mwambungu.

Na
Nickson Mkilanya 
Amefariki leo katika hospitali ya taifa ya muhimbili, hatunaye tena, Said Thabith Mwambungu mkuu wa mkoa mstaaf na miongoni mwa wanasiasa wabobezi na wakongwe katika zama hizi.

Ameripotiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa figo kwa siku kadhaa hata akapelekwa kutibiwa nchini India na kurejea na nafuu ambayo pia haikupata kumrejesha katika majukwaa ya siasa na hata hadharani.

Kuugua huko pasipo kutajwa kuwa ndiyo sababu iliyopelekea rais Magufuli kumhamishia ofisi ya waziri mkuu na kuahidi kumpangia kazi zingine toka juni 26 mwaka jana lakini nafsi yangu yakiri kuwa pengine hiyo ndiyo sababu kuu.

Alilitamka kwa ufasaha jina lake la Saidi Thabith Mwambungu enzi za uhai wake hasa pale nilipofanyakazi naye mimi nikiwa kama mwanawa luninga, radio na hata magazeti, ni mzaliwa wa Malinyi mkoani Morogoro ambaye kwangu mimi ni miongoni mwa wanasiasa bora, baba Bora na kielelezo cha watu wema na wastaarabu niliopata kukutana nao.

Wakati wa uhai wake alipata kuwa kada mwandamizi katika ccm, katibu wa chama cha mampinduzi mkoa, mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa achilia mbali nafasi zingine nyeti ndani ya nchi hii, Na ameacha watoto watatu, Hamidu Said Thabith Mwambungu, Khalid na Abiba Thabith mwambungu na mjane.

Mtoto wa mtoto mkubwa wa marehemu aitwae Hamidu Mwambungu anasema haijaamuliwa bado kama baba yao atazikwa Morogoro au kwingineko.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment