BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKAMU WA RAIS AWASILI ARUSHA, KUONGOZA KUAGA MIILI 32 AJALI WANAFUNZI KUTUMBUKIA KATIKA KORONGO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha jioni leo ambapo hapo kesho ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali jana tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule  iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.

Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hapo kesho.

Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo.

Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment