BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA JIMBO LA KILOMBERO ABEBESHWA MZIGO NA WANANCHI WA NAKAFULU IFAKARA


Mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali (Mwenye sharti nyekundu) akiwa na baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Nakafulu-Milola kijiji cha Kibaoni katika Mji wa Ifakara wakati wa ziara ya kutembelea eneo litakalo jengwa gereza la mahabusu huku wakazi zaidi ya 40 wakisubiri kulipwa fidia na serikali jumla ya sh11.1milioni tangu mwaka 2013 baada ya utathimini kufanyika.

Na Juma Mtanda, Morogoro.

Familia zaidi ya 40 kitongoji cha Nakafulu-Milola kijiji cha Kibaoni, Mji wa Ifakara wamempigia magoti mbunge wa jimbo la Kilombero wakimwomba kuwasaidia kuwasirisha malalamiko yao kwa waziri wa ardhi, nyumba na makazi ili kurejeshewa eneo lao la ardhi la heka 30 lililopangwa kujengwa gereza la mahabusu baada ya serikali kushindwa kulipa fidia jumla ya sh11.1milioni mkoani hapa.

Mbunge huyo alielezwa kuwa serikali imeshindwa kujenga gereza la mahabusu tangu mwaka 2013 licha ya kazi ya utathimini kufanyika huku ikibakia kazi ya wananchi kulipa fidia kiasi cha jumla ya sh11.1milioni.

Akizungumza mbele ya mbungu huyo aliyewatembelea kusikiliza kero mbalimbali, Mwenyekiti wa kijiji cha Kibaoni Mji wa Ifakara, Kassim Libenanga alisema kuwa serikali imechukua jumla ya heka 30 za ardhi za familia za 42 ili kujenga gereza la mahabusu tangu mwaka 2013 katika eneo la Nakafulu-Milola.

Libenanga alisema kuwa eneo hilo lilikuwa na wakazi 42 na wakati tisa walikuwa wakiishi yenye wakazi zaidi ya watu 70 wameingia gharama za kupanga nyumba sehemu nyingine ili kupisha ujenzi wa gereza la mahabusu.

“Tunakuomba mbunge ufikishe kilio chetu kwa waziri Lukuvi ili aweze kuturejeshea eneo letu la heka 30 ili tuendeleze kwa kilimo na makazi maana inaonekana serikali imeshindwa kujenga gereza la mahabusu licha ya utathimini kufanyika na wananchi hawajalipwa mpaka leo.”alisema Libenanga.

Mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji Nakafulu-Milola, Vicent Lukumbo alisema kuwa serikali imewazuia wakazi hao kusitisha shughuli zozote za kuendeleza eneo hilo kwa namna yoyote mpaka hapo watapowalipwa fidia zao.

Msipaendeleze kwa njia ya aina yoyote na mkiona nyumba zetu zinabomoka chukueni mahema mlale humi, Lukumbo alisema akinukuu maneno ya Waziri Lukuvi wakati alipotembelea Kilombero na kamati hii kuwasirisha malalamiko yetu kwake.

Kwa upande wa, Amina Hashim alisema kuwa eneo hilo walikuwa na nyumba mbili wakiishi na kufanya shughuli za kilimo lakini kwa sasa nyumba zote zimeboka kutokana na mvua.

“Tulikuwa tunaishi hapa miaka mingi na wazee wetu na tulifanya shughuli zetu za kilimo lakini mwaka 2013 serikali ilitueleza kuwa eneo hili wanataka kujenga gereza la mahabushu na watatulipa fidia lakini mpaka leo hakuna malipo yoyote yaliyofanyika.”alisema Amina.
Mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali aliwaeleza wakazi hao kuwa malalamiko yao atawasilisha kwa waziri mwenye thamana na majibu atayopewa atayaresha kwao.

“Nimepokea malalamiko yetu isipokuwa kwa sasa itawabidi kuwa na moyo wa subira wakati tunaendelea kufuatilia kwa njia zilizosahihi.”alisema Lijualikali.

Lijualikali alisema kuwa serikali tayari imeshindwa kuwalipa fidia kwa wakati na sheria ipo wazi italazimika kufanya mambo mawili ili kuwatendea haki wananchi wake.

“Sheria ya ardhi Na 4 ya mwaka 1999 na kanuni, taratibu za ardhi ya mwaka 2001 imetamka kuwa kama fidia imechelewesha zaidi ya miezi sita tangu utathimini ufanyike upya au kulipa fidia.”alisema Lijualikali.

Akitolea ufafanuzi juu ya kusuasua kwa ujenzi wa gereza la mahabusu eneo la Nakafulu na wakazi kushindwa kulipwa fidia na serikali, Mkuu wa wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro, James Ihunyo alieleza kuwa bajeti ndio iliyokwamisha kila kitu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: