BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKE WA RAIS DONALD TRUMP SASA KUCHUNGWA NA FBI SAKATA LA URUSI KUJIHUSISHA NA KAMPENI ZA UCHAGUZI MAREKANI

Mkwe wa rais Donald Trump na mshauri mkuu Jared Kushner anachunguzwa na shirika la FBI ikiwa ni miongoni mwa uchunguzi wa Urusi kulingana na vyombo vya habari nchini Marekani.

Ripoti zinasema kuwa wachunguzi wanaamini ana habari muhimu lakini sio mshukiwa wa uhalifu.

FBI linachunguza hatua ya Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa 2016 nchini humo na ushirikiano wa kundi la kampeni la rais Trump.

Rais Trump amekana madai yoyote ya kujihusisha na Urusi wakati wa kampeni.

Wakili wa bwana Kushner amesema kuwa mteja wake atashirikiana na wachunguzi hao kuhusu uchunguzi wowote.

Rais Trump ametaja hali hiyo kuwa 'uwindaji' mkubwa wa kiongozi katika historia ya Marekani.

Vitengo vya ujasusi vinaamini Moscow ilijaribu kukisaidia chama cha Republican kushinda uchaguzi huo dhidi ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton.

Maafisa wa Marekani waliotajwa waliambia chombo cha habari cha NBC kwamba hatua ya kumchunguza bwana Kushner mwenye umri wa miaka 36 haimaanishi kwamba wachunguzi wanamshuku kuhusu uhalifu fulani na kwamba wanataka kumshtaki.

Kwengine ,gazeti la Washington Post limeripoti kwamba wachunguzi hao walikuwa wakiangazia mikutano aliofanya mwaka uliopita na balozi wa Urusi nchini Marekani ,Sergei Kislyak na mfanyikazi mmoja wa benki kutoka Moscow.Jared Kushner na mkewe Ivanka Trump.
Robert Mueller aliyekuwa kiongozi wa shirika la FBI wiki iliopita aliteuliwa na shirika la haki nchini Marekani kuongoza uchunguzi huo wa Urusi.

Bunge la Congress pia linachunguza hatua hiyo ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani na ushirikiano wowote na rais Trump.

Bwana Kushner tayari amekubali kuzungumzia kuhusu uhusiano wake wa Urusi na kamati ya kijasusi ya bunge la seneti.

''Bwana Kushner hapo awali alijitolea kuzungumza kuhusu kile anachokijua kuhusu mikutano hiyo'', wakili wa Kushner, Jamie Gorelick aliambia BBC.

''Atafanya hivyo iwapo atahitajika kuhusiana na uchunguzi mwengine wowote'' ,aliongezea.

Wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru umeongezeka tangu rais Trump alimpomfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey mapema mwezi huu.

Ikulu ya Whitehouse imekumbwa na mizozo kufuatia madai kwamba rais Trump alimtaka aliyekuwa mkuu wa FBI kuwacha uchunguzi kuhusu uhusiano kati ya aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama Michael Flynn na Urusi.

Bwana Flynn alilazimishwa kujiuzulu mnamo mwezi Februari baada ya kumdanganya makamu wa rais kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi kabla ya rais Trump kuchukua mamlaka. Mnamo mwezi Januari.

Urusi mara kwa mara imekana kuhusishwa na uchaguzi wa urais nchini Marekani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: