BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWILI WA PHILIMON NDESAMBURO WAFANYIWA UCHUNGUZI ILI KUBAINI CHANZO CHA KIFO CHAKE KATIKA HOSPITALI YA KCMC

Moshi. Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Bazil Lema amesema mwili wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi mjini Phillemon Ndesamburo unafanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake cha ghafla.

Akizungumza na Mwananchi leo, Lema amesema Ndesamburo alifika ofisini kwake asubuhi kama ilivyo kawaida yake lakini aliugua ghafla mnamo saa nne asubuhi.

Bazil alisema baada ya Ndesamburo kujisikia vibaya, alichukuliwa na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC na wakati madaktari wanakifanya jitahada za kumpa matibabu alifariki dunia.

“Baada ya mwili kufanyiwa uchunguzi taarifa rasmi kuhusu kifo chake zitatolewa na uongozi wa chama pamoja na familia,” amesema

Wakati huo huo wanachama wa Chadema wamekusanyika kwa makundi katika eneo la hospitali wakionekana kuwa sura za huzuni.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment