BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS DONALD TRUMP AMTIMUA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UJASUSI LA FBI JAMES COMEY

Rais Donald Trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua yake ya kuliangazia swala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat Hillary Clinton, mamlaka imesema.

Ikulu ya Whitehouse iliishangaza Washington kwa kutangaza kwamba James Comey amefipigwa kalamu. Rais Putin wa Urusi

Lakini wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.

Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita.

Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.

Bwana Sessions alisema kuwa idara ya haki ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika. Donald Trump

Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa utafutaji wa mrithi wake unaanza mara moja.

Naye kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Bwana Chuck Schumer, amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua kiongozi maalumu wa mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na Urusi.

Alisema kuwa hatua hiyo isipochukuliwa raia wa Marekani wana haki ya kuwaza kuwa Bwana Comey amefutwa ili kupunja juhudi za kukamilisha uchunguzi huo.

Ikulu ya White House imekanusha kuwa kutimuliwa kazini kwa Bwana Comey kuna uhusiano wowote na maswala ya kisiasa.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: