BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AWASHA MOTO UPYA KWA WATUMISHI WA UMMA WENYE VYETI FEKI MEI MOSI


RAIS Dk. John Magufuli, akihutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani.
RAIS Dk. John Magufuli amesema serikali itawachuguza na kuwachukulia hatua baadhi ya wafanyakazi ambao wamebadili umri wao ili waendelee kuwepo kwenye ajira serikalini.

Akizungumza leo kwenye sherehe ya sikukuu ya wafanyakazi dunia zilizofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanajaro, alisema wapo wafanyakazi ambao wamebadilisha umri wao na wanaendelea kuwepo kwenye ajira licha ya kwamba wamezeeka na walistahili kustaafu.

“Wapo watumishi ambao wamebadilishi umri wao wa kuishi wamebadilisha miaka yao, unakuta ni mzee kabisa lakini yeye hastaafu tu huyo naye hana utofauti sana na mfanyakazi hewa, kwa sababu ameshamaliza muda wake hataki kutoka kazini awaachie wengine nao wafanye kazi anaendelea kukaa pale kubadilisha miaka,”alisema.

“Mimi hapa nilipo nilikuwa nimebakiza miaka miwili tu kustaafu lakini hebu kaangalieni kwenye maofisi yenu wapo watu ambao ni wazee kuliko mimi bado wanafanya kazi na wanasema ndio wakati umefika, hawa nao dawa yao tunaichunguza” Rais Magufuli alisema kimsingi kazi ya kuondoa wafanyakazi hewa imeenda vizuri na limefikia asilimia 98 lakini bado halijaisha. 


Aliongeza kuwa katika fedha tu za watumishi hewa, ukichukulia tu mshahara serikali ilikuwa inapoteza Sh. bilioni 19.8 kwa mwezi na kwa mwaka ni zaidia Sh. Bilioni 230.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: