BannerFans.com

SUZAN KIWANGA, LIJUALIKALI WAONJA JOTO YA JIWE MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

SERIKALI, MBUNGE LIJUALIKALI WAWAVIMBISHA KICHWA KLABU YA SHUPAVU FC LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KITUO CHA LINDI

Mkuu wa wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, James Ihunyo kushoto akikabidhiwa jezi na mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuichangia ya timu ya Shupavu FC inayoshiriki ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Lindi iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri wilayani humo na wa kwanza kulia ni msaidizi wa mbunge Anthony Mwampunga


Juma Mtanda, Morogoro.
Serikali ya wilaya ya Kilombero pamoja na mbunge wa jimbo la Kilombero mkoani Morogoro imeanza kuzitisha timu zitakazoshiriki ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Lindi baada ya kujibebesha mzigo nzito wa kuihudumia timu yao ya Shupavu FC kwa kupitisha bajeti ya sh60.9 Mil ili iweze kushiriki vyema ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi leo Mei 28 mwaka huu.

Akizungumza na wadau wa soka wakati wa chakula cha hisani ya kuhamasisha na kuichangia timu hiyo katika Mji wa Ifakara, Mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo alisema kuwa serikali, mbunge Peter Lijualikali pamoja na wadau mbalimbali wamedhamilia kuipiga jeki ya nguvu Shupavu FC ili iweze kushiriki vyema ligi ya mabingwa wa mikoa na kurejea na ubingwa.

Ihunyo alisema kuwa katika chakula hicho ilipatikana kiasi cha fedha sh24,390,000 mil ikiwa ni ahadi ambazo zitakusanywa kabla ya leo Mei 28 ili kuwezesha bajeti ya timu hiyo kushiriki bila kuwa na changamoto za aina yoyote katika ligi hiyo.

“Tumeipitisha bajeti ya kuichangia Shupavu FC kiasi cha sh60,910,000 ili kuiwezesha kushiriki ligi ya mabingwa wa mikoa Lindi lakini bajeti hii tumeijumuisha kabisa na ile ya ligi daraja la pili maana tuna uhakika kwa kiasi kikubwa kuwa vinara na kuingia ligi inayofuata.”alisema Ihunya.

Mbunge wa jimbo hilo, Peter Lijualikali katika hafla hiyo alikabidhi vifaa za michezo ikiwemo jezi pea nne, bips nne, mipira 10, viatu pea 25 pamoja na kuwalipia posha za miezi sita jopo zima la benchi la ufundi ili na wao waweze kutekeleza majukumu yao bila vikwazo vyovyote vikiwa na thamani ya sh11.8 Mil.

“Sina wasiwasi na timu yetu ya Shupavu FC lakini nina imani kubwa timu kurudi Ifakara na furaha ya kufuzu ligi daraja la pili na hii sio kwa Ifakara pekee bali na mkoa wa ujumla kwani wamefanya maandalizi ya nguvu ya kujiandaa na ligi hii na sioni sababu ya kutofanya vizuri.”alisema Lijualikali.

Wengine waliochangia timu hiyo ni pamoja na vyama vya siasa wilaya hiyo wakati Chadema ikitoa sh500,000, CCM sh600,000 na taasisi za fedha zikiwemo NMB, CRDB na makampuni ya simu za mikononi.

Katibu tawala wa wilaya ya Kilombero, Robert Selasela alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya Kilombero na Mji Ifakara zimechangia kiasi cha sh6Mil pamoja na mahitaji mengine ikiwemo usafiri wa kuisafirisha timu.

Selasela alisema kuwa timu ina mahitaji ya aina nne kikiwemo cha vifaa ambacho kimetekelezwa na mbunge, Peter Lijualikali posho za wachezaji na benchi la ufundi, usafiri na chakula huku kazi iliyobakia ikiachiwa wachezaji wenyewe kusaka ushindi katika michezo yao.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads