BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TETEMEKO LA ARDHI LILIVYOZUA HOFU TENA KWA WANANCHI WA BUKOBA


Tetemeko la ardhi limetokea tena mkoani Kagera na kusababisha hofu kwa wananchi.

Hofu hiyo inatokana na tetemeko la ukubwa wa 5.7 kwa vipimo vya Richter lililotokea mkoani hapa Septemba mwaka jana na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 10 majeruhi takriban 200 na mamia wengine kukosa makazi.

Wananchi waliozungumza na gazeti hili, katika Manispaa ya Bukoba, wilaya za Missenyi, Muleba na Karagwe wamesema tetemeko hilo lilitokea saa saba usiku wa kuamkia leo. 


Baadhi ya wananchi mjini Bukoba walilazimika kulala nje ya makazi yao kutokana na kishindo cha tetemeko hilo.Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment