BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 7.2 MILIONI KUFARIKI DUNIA KILA MWAKA KUTOKANA NA UVUTAJI TUMBAKU PEKEE

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema watu 7.2 milioni sawa na asilimia 80 hufariki dunia kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya tumbaku.

Taarifa iliyosomwa leo na mwakilishi wa mkurugenzi wa WHO nchini, Neema Kileo inaonyesha kuwa watu 146,000 wenye umri chini ya miaka 30 hufariki dunia barani Afrika kutokana na magonjwa yanayotokana na matumizi ya tumbaku.

"Magonjwa yanayouwa zaidi kutokana na matumizi ya tumbaku ni pamoja na saratani ya mapafu, kisukari, magonjwa sugu ya mapafu, kuzaa watoto njiti, na kuharibika kwa mimba kwa mama mjamzito" amesema Kileo

Pia amesema watu 600,000 ambao si watumiaji wa sigara hufariki dunia kila mwaka kutokana na kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa wavutaji wa sigara./Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: