BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

YANGA SC YATAWAZWA MABINGWA KWA KIPIGO MWANZA KATIKA PANZIA LA LIGI KUU TANZANIA BARA 2016/2017.

Klabu ya Yanga SC imetawazwa mabingwa kwa kutwaa kombe la ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2016/2017 baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbao FC katika mchezo mkali kufunga panzia ligi hiyo uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Kutokana na kipigo hicho, Yanga SC imeweka historia nyingine ya kutwaa kutwaa kombe hilo mara tatu mfululizo huku Simba SC ikiambulia nafasi ya pili baada ya kuifunga Mwadui FC bao 2-1 katika mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Mara ya mwisho kutwaa kombe hilo ilikuwa mwaka 2012 huku Toto Afrika ya Mwanza ikiaga ligi kuu Tanzania bara baada ya kufungwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro bao 3-1.


Mshmabuliaji wa Mtibwa Sugar, Hussein Juvu alifunga bao mbili pekee yake katika ushindi wa bao 3-1.

Mabao hayo alifunga 16 na 61 huku bao la tatu la Mtibwa Sugar likifungwa na Stamil Mbonde 73 wakati Toto Afrika walipata bao la kufutia machozi dakika ya nane ya kipindi cha kwanza kupitia, Waziri Shentembo dakika ya nane.

Kikosi Cha Yanga SC dhidi ya Mbao FC.
GK-Beno Kakolanya-24
2-Juma Abdul-12
3-Oscar Joshua-3
4-Nadir Haroub-23
5-Vincent Bossou-9
6-Thabani Kamusoko-13
7-Saimon Msuva-23
8-Justine Zulu-14
9-Obrey Chirwa-7
10-Haruna Niyonzima-8
11-Geoffrey Mwashiuya-19.

SUBS
GK-Geogratius Munishi-30
2-Hassan Hamis-25
3-Pato Ngonyani-15
4-Deus Kaseke-4
5-Matheo Anthony-10
6-Emmanuel Martin-18

BENCHI LA UFUNDI
Kocha: George Lwandamina
Kocha msaidizi: Juma Mwambusi.

Katika matokeo mengine Majimaji FC ilipata ushindi wa bao
2-1 mbele ya Mbeya City FC ya Mbeya, Tanzania Prison ilicheza na Africa Lyon na kumaliza kwa 0-0 wakati Ndanda FC ya Mtwara ilipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu, Azam FC ilikubali kipigo cha bao 0-1 na Kagera Sugar uwanja wa Chamanzi jiji Dar es Salaam.

Michezo mingine Stend United ya Shinyanga walichuana na Ruvu Shooting ya Pwani huku Stend ikiibuka na ushindi wa bao 2-1.

Timu zilizoshuka kutoka ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2016/2017 hadi ligi daraja la kwanza ni pamoja na African Lyon, Toto Africans na JKT Ruvu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: