BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YAZIMA MITAMBO YA MAWASILIANO YA HUDUMA ZA INTERNET KWA SIMU ZA MKONONI

Serikali ya Ethiopia imezima mawasiliano yote ya huduma za mtandao wa Intaneti kwenye simu za mkononi bila kutoa sababu ya uamuzi huo.

Mnamo mwaka jana, nchi hiyo iliripotiwa kubana mawasiliano ya mitandao ya kijamii mara baada ya mitihani ya chuo kikuu kuvuja kwenye mitandao.

Kuna tetesi kuwa kufungwa kwa mitandao hiyo hivi sasa inatokana na sababu ileile ya mwaka jana ingawa taarifa hiyo inakanushwa.

Hali ya hatari iliyopo nchini Ethiopia tangu mwezi Oktoba mwaka jana imesababisha maamuzi hayo kufanyika.

Huduma ya intaneti kupitia simu za mkononi imekuwa ikifungwa mara kwa mara nchini humo.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment