BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA YAIPELEKA YANGA KWENYE PENALTI NGAO YA JAMII DAR ES SALAAM

NGAO YA JAMII
Simba imetwaa ngao ya jamii kwa kuifunga Yanga kwa penati 5-4 baada ya kwenda suluhu ya 0-0 katika mchezo mkali wa kufungua panzia ya ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa mwaka 2017/2018 uliofanyikwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa na presha kwa timu zote zikitaka ushindi ndani ya dakika 90 lakini ulimalizika kwa suluhu hiyo huku kila 4imu ikiwa na nyota wapya.

Simba ilikiwa na baadhi wa nyota wake akiwemo Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima aliyesajiliwa akitokea Yanga wakati Yanga nao ilikuwa na nyota Ibrahim Ajibu aliyetokea simba na Tshishimba.

Mchezaji Mohamed Ibrahim wa simba ndiye aliyeamua ushindi kwa timu yake baada ya kufunga penalti iliyoamua matokeo katika penalti sita kufuatia penalti tano kumalizika kila timu ikiwa imepata nne na kukosa mmoja wakati katika penalti moja moja Yanga walipoteza kupitia kwa Juma mahadh na kufanya matokeo kuwa 5-4.

Simba wamekabidhiwa ngao.

Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment